Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa kitabu cha ukulima wa matunda Kama matikiti maji,embe,chungwa,Migomba,nanasi,papai na pensheni unaweza kuniPM
Weka bei basi mkuu
Bei ni 5,000/= Kwa kimoja cha matunda i.e matikiti maji ila ukichukua vitatu ufugaji wa kuku,mboga na matunda utapata Kwa bei ya 12,000/=
Ntahitaji cha matikiti mkuu I will contact you
Mimi nalima aina ya Sugar baby inachukua siku 60 tu kuvuna tangu plus siku 3-5 za kukaa ardhini, kwa hiyo kwa mwaka nalima mara 4 tu nina ekari 5 na kila eka napata kuanzia 2M-3M.
Spacing ni 2mx2m na kila shimo naweka mbegu 2 ambazo zinazaa matunda 2-3 kwa maana kila shimo napata matunda 4-6 ( wastani matunda 5).
Hivyo kwa spacing hiyo napata mashimo 1000-1200
Idadi ya matunda: Mashimo x Matunda kwa shimo x ekari [1,000 x 5 x 5 = 25,000]
Mapato: wastani wa shilingi 500 kwa tikiti x idadi ya matikiti kwa eneo la ekari 5 [25,000 x 500 = 12,500,000]
Mapato kwa mwaka: 12,500,000 x 4= 50,000,000
Gharama za uendeshaji wa shamba ni Tsh 25,000,000
Faida Kuu ni Tshs 25,000,000 M.
Tujenge taifa letu kwa kilimo
NASHAURI TU JAMANI,
Badala ya kulima heka tano jaribu kulima heka moja tu ila fanya yafuatayo.
Badala ya kuruka mita mbili otesha mtikiti kila baada ya nusu mita.
kwa heka moja utapata mashimo 19,800.
mtikiti ukitoa tunda moja tu ukate kwa mbele ili usiendelee kuzaa.
kwa hiyo tunda moja kwa mche mmoja utanenepa vizuri badala ya kuuza 500= uauza 2,000.
Tufanye ukaua 1,000= utapata 19,800,000 badala ya 2m.
NASHAURI TU JAMANI,
Badala ya kulima heka tano jaribu kulima heka moja tu ila fanya yafuatayo.
Badala ya kuruka mita mbili otesha mtikiti kila baada ya nusu mita.
kwa heka moja utapata mashimo 19,800.
mtikiti ukitoa tunda moja tu ukate kwa mbele ili usiendelee kuzaa.
kwa hiyo tunda moja kwa mche mmoja utanenepa vizuri badala ya kuuza 500= uauza 2,000.
Tufanye ukaua 1,000= utapata 19,800,000 badala ya 2m.
tena mbegu za pata negra ninauza bei ni sh 45000 kwa 1000 seeds
Mkuu jaribu kuputia walichouliza wenzako na majibu yake. Swali km lako limeulizwa sana na kujibiwa kwahiyo jipe muda wa kusoma kuhusu wengine km unataka elimuWana JF naomba mniambia kilimo cha matikiti maji kwa heka moja unaweza ukavuna kiasi gani? Pia naomba kuuliza heka ya matikiti mauzo yake yanaweza kuwa kiasi gani? Msaada jamani.
Rafiki yangu mmoja kutoka Israeli anasema matikiti haya ya Tz. ni madogo sana. Ikiwa mtu atazingatia ubora wa kiulimo cha water melon anaweza kuvuna matikiti makubwa mara mbili zaidi ya haya tunayoyaona. Kumbe inabidi yawe yananing'inia. Unaweka viatlu imara na kupauwa kwa miti ambayo itatoa njia ya mmea kutambaa na matunda yatakuwa yananing'inia, Then majani ya mmea yanatoa kivuli kwa matunda. halafu pale kwenye shina unaweka system ya kudondoshea maji kwa awamu. kwa mfano unaweza kuweka chombo cha maji kinachodondosha matone machache sana pale shinani.. bcoz..matikiti hayahitaji kumwagiliwa maji mengi (yatapasuka) ndio maana hayalimwi wakati wa mvua. Hata wakati wakumwagiliwa haishauriwi kumwagia majani bali shina tu.. Kuhusu mbolea wanadai Samadi hasa ile ya kinyesi cha kuku ndiyo nzuri.. Binafsi bado najifunza na kutafuta mtaji..........