Nusu ekari nahitaji mtaji wa kiasi gani?
Mkuu,
Kwanza samahani sana kwa kuchelewa kujibu swali lako. Nimekua mvivu sana wa kuingia JF kutokana na kutingwa kwa shughuli za hapa na pale.
Kwanza kabisa nisingependa kukushauri silime nusu ekari, ni kidogo sana. Kama upo karibu sana na soko, basi haina shida, ila kama unaishi mbali na soko, kulima eneo dogo kunaweza kukufanya upate hasara kutokana na gharama kubwa ya usafiri.
Kadiri unavyokua na mzigo mkubwa, gharama kwa tonne (cost per tonne) ndivyo inavyoshuka na kukuwezesha kupata faida zaidi. Hivyo ukilima eneo dogo, gharama ya kusafiri itakuumiza.
Pili, gharama za kilimo zinategemea sana na aina ya kilimo unachofanya. Maswali ya kujiuliza ni kama ifuatavyo:
1. Je, unatumia kilimo cha kisasa au bora liende?
2. Je, unamtumia bwana shamba?
3. Hapo unapolima, unatumia trekta? Trekta lipo umbali gani toka shambani?
4. Unatumia mbolea ya namna gani? Mbolea inapatikana umbali gani toka shambani?
5. Hapo unapolima kuna vibarua wa kutosha wanaojua kuhudumia matikiti maji?
6. Eneo unapolima, hali ya uchumi ipoje? Hali ya uchumi ikiwa juu, gharama ya vibarua itakua juu pia.
7. Unafanya kilimo cha umwagiliaji au unategemea mvua?
8. Kama unamwagilia, je unatumia mashine ya aina gani? Au unamwagilia kwa mikono?
Na mambo mengineyo mengi.
Kwa ujumla, mambo kama hayo hapo juu hufanya maeneo tofauti kua na gharama tofauti. Hivyo uchaguaji wa eneo ni kitu muhimu sana kabla ya kuanza kulima.
Mimi nilishalima mkuranga mara kadhaa, na za kilimo kwa ekari zilikua around laki saba hadi nane.
Kama wahitaji kujua zaidi, niulize.
I hope that helps.