Mkuu nililia bugurun pale kama mtoto nimepeleka mzgo bei tuliyokubaliana asubuh na dalali ilishuka jion nilivyopeleka mzigo alafu akaniambia kama hujaridhika na bei hii njoo tuuze wote ...kiruuuu hapo ni SAA kumi na mbil jioni yani madalali wanaua wakulima ..
hujalia peke yako Mamy,ngoja nikupe yangu.:A S cry:
nililima Viazi vitamu na ilitoka sana,basi nikatafuta dalali nikampeta hapo hapo Buguruni,nikampeleka hadi shamba akaukubari mzigo.kesho yake akanipa mtu niende nae ili tuvichimbe mapema yeye akija aje kuvipakia na gari.
mtoto wa kike acha nijitutumue na mie kusaidia kuchimbua hadi nikatokwa na vigimbi vya mkono,kufika jioni tulikuwa bado hatujamaliza kuchimbua yaani ilibaki kisehemu kidogo sana,basi jamaa akapiga cm akadai hadi tumalize ndiyo aje na gari na hayo maviroba.nikamwambia advance akakata kutoa hadi yeye avione.
kesho yake ilikuwa j3 mimi nipo kazini,sasa jamaa kaenda na gari kavichukuwa viazi yani kajaza canter hadi vinamwagika na hela yangu hakunipa.nampigia cm ananiambia viazi vyenyewe vimeoza nimechagua chagua nimepata viroba vi4 na gharama yangu ya usafiri unafikiri mie napata nini,kama vipi njoo hapa sokoni Buguruni uone jinsi navyouza kwa bei ya hasara ili nirudishe gharama ya usafili.
jioni nikapita sokoni,daah! jamaa ananiambia viazi vyako haviuziki nimepata elfu50 tu ,sasa ntakulipa nini.uuuuwiii! yani hakuna siku mbaya kama ile yani nilihisi kuzimia mbele yake.nikamwambia naenda POLISI,
alinijibu POLISI nenda tu maana viazi vyako vimeniingizia hasara.ilibidi nikubari matokeo.
SASA KWENYE TIKITI NILIKUWAJE MKALI ,YAANI HELA MBELE NDIYO UTOE TIKITI SHAMBANI.BILA HELA CASH ZAO LANGU HALITOKI.
ILA KUNA WATU WANAROHO MBAYA SANA,NAWAOGOPA SANA MADALALI NA NAWACHUKIA SANA SANAAAA.