OgwaluMapesa
JF-Expert Member
- May 24, 2008
- 10,942
- 434
Usijisumbue kilimo hakiwez kukupa utajiri ww. Hiyo ni sawa na mwalimu kuwa billionaire; bibi yko kaanza kulima since hamsin kweusi but mpk leo choka mbaya, jaribu biashara nyingine tu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Usijisumbue kilimo hakiwez kukupa utajiri ww. Hiyo ni sawa na mwalimu kuwa billionaire; bibi yko kaanza kulima since hamsin kweusi but mpk leo choka mbaya, jaribu biashara nyingine tu.
Kwa wale wenye uzoefu, utaalamu, au taarifa ya kilimo cha Matikiti Maji ninaomba taarifa zifuatazo:
(I) Mtaji unaotakiwa kulima hekari 1;
(ii) Muda unaochukua kutoka kupanda mpaka kuvuna;
(iii) Upatikanaji wa soko;
(iv) Kipindi gani ndani ya mwaka kinafaa kwaajili ya mradi huu; na
(v) Eneo gani matikiti yanastawi zaidi ndani ya mipaka ya Dar es Salaam.
chonde chonde kaka,usizilete hizo mbegu,it may cause GM contamination,wasiliana na wataalam wa kilimo watatoa ushauri mzuri.ila bora uziache huko huko,hizi za kwetu ni poa sana tu.
wajapan wametengeneza watermelon la square kama box ili iwe rahisi kusafirisha matunda hayo,Mh! madhara yatajulikana baadae,ktk cancer na magonjwa mengineyo.
Mbegu za matikiti maji zinapatikana wapi?
Je nyie mnaolima mnanunua mbegu kila msimu? au yenyewe yanatoa mbegu?
Kaka, upo Dar?
Kama upo Dar nenda pale kwenye soko la kaiakoo, panda ghorofa ya kwanza ulizia mbezu za matikiti maji, zipo nyingi tu.
Usipande mbegu ulizotoa kwenye matunda, haishauriwi kitaalam.
wadau mimi natafuta wataalam wa ku design a simple drip irrigation system kwaajili ya kilimo cha tikiti. kama kuna mtu ana namba za wahusika plz niPM
wadau mimi natafuta wataalam wa ku design a simple drip irrigation system kwaajili ya kilimo cha tikiti. kama kuna mtu ana namba za wahusika plz niPM
Mwenye kutaka information zaidi kuhusu drip irrigation system - design na supply ni PM.
Mkuu kwanini usizimwage humu?
Drip irrigation ni somo refu sana, so inabidi nijipange sana ili kuelezea kitu kinachoeleweka. Ila kwa kifupi, kuna mambo machache ya kuzingakita kama ifuatavyo:
1) Umbali kati ya mche na mche (Plant Spacing)
Umbali kati ya mche na mche kwa zao la matikiti maji hutofautiana kutokana na ulimaji. Kuna wengine huacha umbali wa 1.8 - 2.0m kati ya shimo na shimo na kila shimo wanaacha miche mitatu hadi minne. Kuna wengine wanaacha nafasi ya 1.0m na wanaweka miche miwili kila shimo.
Binafsi nilikua nataka kujaribu kuacha nafasi ya 0.5m na kuacha mche mmoja kila shimo, ingawa kuna wengine wanasema unaweza ukaacha umbali wa 0.3 - 0.4m kwa kila mche. Mimi nimeshawahi kuacha nafasi ya 1.5m kati ya shimo na shimo na kila shimo niliacha miche mitatu.
Unapochagua drip tapes (ambayo ni mipira midogo yenye matundu) unatakiwa uzingatie umbali kati ya mmea na mmea kutokana na ulimaji wako. Kuna drip tapes zenye umbali wa 10cm ~ 30cm na kuendelea. Ila ambazo zinapatikana sana ni zile za 20cm and 30cm.
Hivyo, kama unataka uache umbali wa 1.5m kati ya shimo na shimo basi utapata wakati mgumu sana kupata drip tapes zenye umbali huo.
Kama unataka kulima tikiti maji, tafuta drip tapes za 30cm spacing na unaweza ukaruka tundu (dripper) moja kila baada ya mche. Hii itafanya umbali kati ya mche na mche kuwa 60cm.
2) Ukubwa wa mabomba (Main and Sub-main Pipe Sizes)
Kwenye drip irrigation unatakiwa utumie mabomba kuendana na kiasi cha maji kinachohitajika shambani. Kadiri maji yanavyohitajika kwa wingi ndio unavyolazimika kutumia mabomba makubwa. Kwa ekari moja unaweza tumia sub-main yenye ukubwa wa 2" hadi 2.5" kutegemeana ma mwinuko wa shamba.
3) Kiasi cha maji kinachohitajika (Water consumption)
Unalazimia kukokotoa kiasi cha maji kinachohitajika shambani ili uweze kutengeneza ratiba yako ya umwagiliaji. Kwa mfano, kama shamba lako lina miche 4,000 na kila mche mmoja unatakiwa kiasi cha maji cha lita 2 kwa siku, basi shamba lako kwa siku litahitaji lita 8,000. Kama unamwagilia mara mbili, basi asubuhi lita 4,000 na jioni lita 4,000. Hii itakufanya uwe na ratiba mbili kwa siku.
Kama ratiba ya asubuhi hufanyika ndani ya saa moja, basi inabidi uwe na mabomba (main and sub-main) ambayo yanaweza kupitisha lita 4,000 za maji kwa saa. Pia lazima uwe na pump yenye uwezo wa kusukuma kiasi hiki cha maji kwa saa katika presha inayotakiwa. Drip system nyingi hutumia pressure ya 0.7 - 1.0bar. So pump yako lazima iweze kusukuma kiasi cha lita hizo kwa saa kwa msukumo wa 1.0bar.
Pia, drip tapes zako lazima ziwe na matundu yenye flow rate ya 1 litter per house (1lph) at the operating pressure. (could be 0.7 ~ 1.0bar depending on dripper construction)
Kama nilivyokwisha sema, mambo ni mengi kwenye drip irrigation. Ila kwa leo naomba niishie hapa. Kama una swali uliza tuelimishane taratibu.
Ubarikiwe sana mkuu kwa nondo hizo za ukweli guys like makes JF more meaningful
Naomba kujua costs za kuset up Drip irrigation system kwa ekari moja approximate ni kama sh ngapi?
Asante sana mkuu
Ili kupata gharama ya kufunga drip irrigation system kwenye shamba, unabidi ujue vitu vifuatavyo:
1) Urefu wa drip tapes unaohitajika
2) Urefu na ukubwa wa main na sub-main pipes
3) Connectors and other fittings
4) Filters, valves, pump, water tank
5) Other necessary accessories depending on your land
Urefu wa drip tape unategemea na plant spacing, row-to-row distance, and the number of drip lines per bed/row. Mazao mengi kama Matango, pilipili hoho, spinach etc unaweza kutumia 30cm spaced drip tapes, 2 drip lines per row. Kwa mfano, kwa pilipili hoho, ukiamua kupanda kwa vipimo vifuatavyo:
- 30cm dripper spacing
- 2 drip lines per row
- 1.8m row/bed spacing (center-to-center)
Assume your land is 50x100m size (a bit larger than 1 acre), and your beds are 100m long, then you will have 50/1.8 = 28 beds/rows of 100m length
Since each bed has 2 drip lines, then the total length of drip tape required is 28 x 2 x 100m = 5600m ~ 6,000m
Sasa bei inategemea unanunua toka wapi. Ukinunua toka kwa suppliers hapa bongo, tegemea kutoa kitu kama 2,000,000 - 5,000,000/= kwa ekari.
Ila kama unataka kwa ekari mbili au zaidi, nakushauri uagize toka nje. Ukiagiza 3,000,000/= inaweza tosha kwa kila kitu kwa ekari mbili. Kadiri ukubwa wa shamba unavyozidi ndio bei huwa raisi zaidi kutokana na gharama za usafiri kuwa nafuu zaidi.
Kuna vitu vingi sana sijavizungumzia hapo, lakini natumaini unaweza pata mwangaza kidogo kwenye suala la gharama.
Okay Thanks
Ntakutafuta kwa msaada zaidi