Kilimo cha Mihogo (Cassava): Mbinu, Ushauri, Changamoto na Masoko yake

Changamoto kubwa ya kilimo cha muhogo huku kwetu ni fuko.Kama kuna mtu anajua njia rahisi ya kupambana na fuko msaada tafadhari.
 
Soko likoje kwa sasa?
 
Kwetu kilimo cha mihogo kili haribiwa na virus sijui alitokea wapi, ukilima wanavamia wanatapakaa kwenye shina wanatoa unga mweupe, huko ardhini kila kitu kina oza. Sijui aliitwa Cassava mealybug, alihariubu maisha kabisa.
 
Kwetu kilimo cha mihogo kili haribiwa na virus sijui alitokea wapi, ukilima wanavamia wanatapakaa kwenye shina wanatoa unga mweupe, huko ardhini kila kitu kina oza. Sijui aliitwa Cassava mealybug, alihariubu maisha kabisa.
Kwa sasa hali ipoje?
Mlibadilisha mbegu wadudu waliendelea kuwepo?
Je mlitumia dawa ya wadudu?
 
Mbegu bora zinazohimili magonjwa zipo.
Pia dawa za kuangamiza wadudu zipo zinapatikana maduka ya pembejeo.
Hili tatizo lilishindikana, ni ardhi ya mkoa mzima inashida hiyo, ni aina zote za mihogo zinaathirika, chini muhogo unaoza, juu unakuwa kama umemwaga unga.

Hao virus waliathiri hadi mtama, unatoka unakuwa kama una utando wa baibui halafu umegandamana,,shamba zima.

Labda hiyo dawa inyunyiziwe mkoa mzima na ardhi ipigwe sindano.
 
Mkoa mzima umeathirika??
Mkoa gani vile
 
Mkoa mzima umeathirika??
Mkoa gani vile
Hahaha usije niteka tu mkuu, ila mikoa yote kanda ya ziwa, ukijumuisha na huku kwetu "Mara" mkoa mzima zao la Muhogo limeathirika sana, tuliambiwa kuna virusi anaitwa "cassava mealybug" ki biologia "Phenacoccus manihoti" kama sijakosea.

Waliwahi kuleta watafiti wakaenda maporini huko wakapiga picha wakaondoka hawakurudi tena, nikajua hili hawakuliweza.

Mkuu njoo ufanye utafiti utuletee tiba, wao walisema tukibadirisha mazao kwa muda litaisha, lakini haikuwa hivyo.

Karibu kibara Bunda, twende na ukerewe a.k.a UK.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…