Kilimo cha Mihogo (Cassava): Mbinu, Ushauri, Changamoto na Masoko yake

Kilimo cha Mihogo (Cassava): Mbinu, Ushauri, Changamoto na Masoko yake

Changamoto kubwa ya kilimo cha muhogo huku kwetu ni fuko.Kama kuna mtu anajua njia rahisi ya kupambana na fuko msaada tafadhari.
 
Mihogo ndio nilikuwa natafuta picha za kazi nimezikosa nadhani zilipotea kwenye simu yangu iliyoharibika.

Kama kuna kipindi ulisikia serikali imepata soko la Muhogo China basi kwa fursa hiyo nililima mihogo kama eka 6 na nusu. Mchina alitangaza bei nzuri sana kwa mhogo mbichi yaani alitangaza Tshs. 1,060/= kwa kilo moja.

Kwa hiyo nilijituma nikawekeza. Sasa baada ya miezi saba Mchina alianza kununua mhogo alianzia Handeni Tanga. Tatizo la mchina alikuwa ananunua mhogo mbichi halafu anaupeleka kwenye sait yake huko huko shamba kule alikuwa na mashine za kuuchakata. Yaani mashine ile muhogo unakatwa silesi silesi za cm 10. Halafu ukishakatwa wanaanika juani. Unakauka baada ya siku 2 wanaweka kwenye viroba vya kilo 50.

Kwa hiyo sisi wa Kisarawe huko vijijini tukawa tumekosa mashine ya kuch akata mhogo na msimu wa mvua ulikuwa unakaribia.

Kwa kweli Mchina nae alipata hasara sababu mhogo alionanika ulinyeshewa. Nasikia milioni 15 zilipotea.

Kilichotokea sasa akashusha bei toka 1,060/= kwa kilo mpaka Tshs. 600/= kwa kilo.

Hata hivyo hiyo bei ilikuwa bado nzuri sababu shina moja la mhogo mimi lachini ilikuwa 13 kwa shina na juu kilo 18 mpaka machache kg 20 kwa shina. Sasa kama miche iko 4000 kwa eka bado bi hela ndefu.

Tuliomba msaada kwa viongozi serikalini kupata mashine ya kuchakata ndipo Mh
Jokate Dc aliongea na wanunuzi ma agent wa mchina wako kule mwenge. Wakakubali kutuazimisha mashine za kuchakata bure na pale wilayani wakaniazimisha bure jenereta kwa muda wote mpaka nimalize mhogo wangu.

Picha ya hiyo mashine nitakuwekea hapo chini.


Kwa kifupi nilifanikiwa kuvuna eka 2 tu sababu mvua ilianza. Mzigo wa mhogo waliufuata wenyewe kule mule shamba kwa gharama zao, na pia walinipa mifuko ya kg 50 bure nijaze mhogo.

Walini lipa kupitia account ya bank bila utata wowote.

Kilichonifanya nisilime tena ni mchina kubadilisha bei anavyataka yeye.

Bei alipunguza tena.

Kwa hiyo soko langu alikuwa mchina kwa mbegu ya Kiroba nasikia wao walikuwa wanafuata starch au wanga kwenye hiyo mihogo. Soko la buguruni sina uzoefu nalo.
Soko likoje kwa sasa?
 
Kwetu kilimo cha mihogo kili haribiwa na virus sijui alitokea wapi, ukilima wanavamia wanatapakaa kwenye shina wanatoa unga mweupe, huko ardhini kila kitu kina oza. Sijui aliitwa Cassava mealybug, alihariubu maisha kabisa.
 
Kwetu kilimo cha mihogo kili haribiwa na virus sijui alitokea wapi, ukilima wanavamia wanatapakaa kwenye shina wanatoa unga mweupe, huko ardhini kila kitu kina oza. Sijui aliitwa Cassava mealybug, alihariubu maisha kabisa.
Kwa sasa hali ipoje?
Mlibadilisha mbegu wadudu waliendelea kuwepo?
Je mlitumia dawa ya wadudu?
 
Mbegu bora zinazohimili magonjwa zipo.
Pia dawa za kuangamiza wadudu zipo zinapatikana maduka ya pembejeo.
Hili tatizo lilishindikana, ni ardhi ya mkoa mzima inashida hiyo, ni aina zote za mihogo zinaathirika, chini muhogo unaoza, juu unakuwa kama umemwaga unga.

Hao virus waliathiri hadi mtama, unatoka unakuwa kama una utando wa baibui halafu umegandamana,,shamba zima.

Labda hiyo dawa inyunyiziwe mkoa mzima na ardhi ipigwe sindano.
 
Hili tatizo lilishindikana, ni ardhi ya mkoa mzima inashida hiyo, ni aina zote za mihogo zinaathirika, chini muhogo unaoza, juu unakuwa kama umemwaga unga.

Hao virus waliatjiri hadi mtama, unatoka unakuwa kama una utando wa baibui halafu umegandamana,,shamba zima.

Labda hiyo dawa inyunyiziwe mkoa mzima na ardhi ipigwe sindano.
Mkoa mzima umeathirika??
Mkoa gani vile
 
Mkoa mzima umeathirika??
Mkoa gani vile
Hahaha usije niteka tu mkuu, ila mikoa yote kanda ya ziwa, ukijumuisha na huku kwetu "Mara" mkoa mzima zao la Muhogo limeathirika sana, tuliambiwa kuna virusi anaitwa "cassava mealybug" ki biologia "Phenacoccus manihoti" kama sijakosea.

Waliwahi kuleta watafiti wakaenda maporini huko wakapiga picha wakaondoka hawakurudi tena, nikajua hili hawakuliweza.

Mkuu njoo ufanye utafiti utuletee tiba, wao walisema tukibadirisha mazao kwa muda litaisha, lakini haikuwa hivyo.

Karibu kibara Bunda, twende na ukerewe a.k.a UK.
 
Back
Top Bottom