Ni Kilimo rahisi kisicho na gharama sana. Kwa huku Makete na kule Kilolo ninapolima, roughly gharama zake ni kama ifuatavyo kwa Ekari 1:
1. Kukodi Shamba Tsh 50,000
2. Kulima Ekari 1 Tsh 70,000
3. Mbegu Kilo 50-75@2500
4. Kupanda Tsh 50,000
5. Mbolea Pandia 1bg Tsh 75,000
6. Kiuagugu(2,4-D) Tsh 24,000
7. Viuatilifu(Lumps) Tsh 50,000
8. Uvunaji Tsh 50,000
9. Kubeba/safirisha Tsh 50,000
10. Vifungashio 10-12@1000
Jumla kuu Tsh 550,000/=
Mavuno: 10-12 bgs@100Kg Tuchukue 10 tu sawa na Kilo 1000
Kilo 1 Sokoni inacheza 1500 hadi 2000. Tukichukua minimum 1500×1000=1,500,000/=
Faida= 1,500,000-550,000
Roughly 950,000 ndani ya miezi 3.
Hapo ni kila kitu kikiwa sawa. Nina uzoefu wa Kilimo hiko kwa miaka 6 sasa.