Kilimo cha Tangawizi - Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Nimependa hayo matangawizi pichani. Kumbe mtu akikwambia "midole kama tangawizi" hajakutendea haki kabisa.

Wataalamu wa hili zao mje jamani kutuelimisha.

Asante mtoa mada.
 
Kwa wingi linalimwa alikokuwa mbunge mke wa Malechela. Ameweka initiative kubwa sana na kuna kiwanda cha tangawizi kilikuwa kianzishwe huko.
 
Tangawizi ya pili kwa ubora maana ina maji inatokea Mkongotema wilaya ya Madaba. Bei inategemea na msimu kwa kuanzia 800 tsh mpaka 1200 tsh
Madaba ruvuma, same. Muda wa kuvuna miezi 6-8-12. Bei ya shambani kilo 1000-1500
 
Maeneo yanayolima Tangawizi sehemu kubwa ni maeneo ya mwinuko aidha kwa mlimani au kutokea usawa wa bahari na udongo maeneo hayo ni ule wa kivolkano au asidi mfano ni Madaba-Ruvuma,kilosa,Moro vijijini-Morogoro,muheza,lushoto-Tanga,Mamba,Same-Kilimanjaro.
Tafadhalini wadau naomba kupata maelezo juu ya kilimo cha tangawizi kwa vipengele vifuatavyo:-
1/ Maeneo yanakolimwa hapa Tanzania. 2/ Muda wa kulima hadi kuvunwa 3/ Soko lake likoje hapa nchini
 
Kilimo cha viungo mara nyingi hatutumii sumu za viwandani na mbolea pia.
Point to note.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…