Kilimo cha Tangawizi - Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Mkoa wa kigoma - Cost
Mbegu: 1000kg*700 = 700,000/=
Kukodi shamba = 200,000/=
Kulima =200,000/=
Palizi ya kwanza =200,000/=
Palizi ya pili = 200,000/=
Palizi ya tatu = 200,000/=
Note: Hili ni kadirio la juu,bei ya mbegu kwa sasa ni kati ya shs:500/= na 700/=, kuanzia mwezi wa nane itakuwa juu ya shs:1,000/=
 
KILIMO CHA TANGAWIZI
Imebidi nirudie mara mbili mbili kuamini darasa hili limeletwa na mwanangu Joseverest, safi sana kamanda hapa umetisha.

Sasa turudi shambanj kidogo hebu tudadavulie kama unajua bei ya mbegu ni kiasi gani,nataka nikajaribu kulima kwa mababu huko Tukuyu nahisi sifa zinaendana na ulizozitoa hapo juu.
 
Nipo Songea mbegu kwa mkulima Roba ninkama laki 4,Hekari inahitaji roba 4..=1600000
 
Wapendwa, mbona watu wanaogopa Kulima hili zao, wanadai ukivuna soko lake ni changamoto sana, maana kwamba kupata sehemu ya kuuza hiyo tangawizi ni shughuli nzito.
 
Sasa sijui hizo taarifa za ugumu wa soko ni za kweli au siyo kweli ,je soko lake kuu ni wapi? Mfano mtu aliyelima kigoma soko analipata wapi?
 
Uzi mzuri, ahsante mkuu na mimi nimepata fursa ya kujua mawili matatu kupitia uzi huu. Kule mkoani Tanga kuna eneo linaitwa Mbaramo, naskia tangawizi inakubali sana huko
 
Uzi mzuri, ahsante mkuu na mimi nimepata fursa ya kujua mawili matatu kupitia uzi huu. Kule mkoani Tanga kuna eneo linaitwa Mbaramo, naskia tangawizi inakubali sana huko
Mbaramo Heka wanakodisha sh ngapi mkuu
 
Mmh hichi kilimo kwenye masoko ndo changamoto ilipo. Me nimelima lkn soko limekuwa gumu nimeona bora niiache kwanza shambani. Mwenye uhitaji tuchekiane

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kwa mfano bei ipo chini nnaona nikivuna kwa bei iliypo inaweza kunikata je nikichelewa kuvuna tangawizi haiwezi kuharibika?
 
Mkuu maelezo mazuri sana. Soko ni mtihani mkubwa. Kuna tangawizi zipo shambani mwaka sasa kwa kukosa soko si ndani au nje soko ni shida. Mwenye uhitaji wa tangawizi tuwasiliane.
Bei unafanyaje Mkuu? Zipo kiasi gani?
 
Naombeni utaalam, gharama, na soko la tangawizi wataalam, na zaidi tujumuike kubadilishana mawazo. Naiona fursa hii mazingira niliyopo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…