Mtaalamu wa zao hili na Bwana shamba anayeishi Mwanhuzi -Meatu, alinishauri nilime mbegu iitwayo Red Bombay(Mang'ora) kama ulivyokuwa ikiitwa na wakulima wazoefu niliowakuta kwenye game, kwasababu shauku ilikuwa ni kufanikiwa niliulizia juu ya kipimo kinachotosha hekari Moja.
Mtaalamu wa kilimo hiki Samson Luzege ( afisa kilimo) alinishauri kuchukua angalau kilo 5 kwa mbegu hii ya kienyeji nilimwambia apime ndebe Zima kilo 9 hivi. Safari ya kilimo hiki ilianza mbegu ziliota zikapendeza kweli,hapo ndipo hesabu mezani za mamilioni ya pesa zilikuwa zikizunguka kichwani Mwangu niliwaza kukunja zaidi ya Milioni 10 Hadi 20 za Kitanzani maana mawazo makubwa yalilenga kupata gunia zaidi ya mia Moja kwa hekari Moja.tulijituma usiku na mchana tukifanya Kila linalowezekana kufanikisha zoezi hili,shamba likalimwa,safu zikatengenezwa.
Kwakweli kama ni ajira tulitoa kwa vijana, kwakuwa sikutaka kufeli hata kidogo nilisafiri kutoka ninapoishi kwenda kutafuta vijana wazoefu wa kupanda zao hili Semu( mto Semu) eneo maarufu kwa kilimo Cha vitunguu Wilaya ya Meatu-Simiyu tuliweka mikakati lini zoezi lifanyike, baadae hatukuwatumia vijana hao kwani walianza kuonyesha maringo huku mbegu zikiwa zimeshaanza kutuonesha dalili ya malalamiko kuwa zinahitaki kuhamishiwa shambani.
Tulipata ushauri wa wataalamu mbalimbali kuwa upandaji wa vitunguu na mpunga utofauti ni kidogo mno kuwa vitunguu visizamishwe angalau basi sm2 kama vilivyokuwa kwenye vitalu ,tulijitahidi kutoa taaluma hii hasa kwa kuwatumia akina mama wa pale kijijini kazi waliifanya vizuri upandaji wa vitunguu ukaenda vizuri, vikamea vizuri shamba likapendeza kweli,tulifika wakati wakuanza kupalilia kwahofu ya kuunguza vitunguu ilibidi kutuliza kichwa nilimuomba ushauri mtaalamu wa zao hili na muuzaji wa mbegu ya vitunguu kutoka Mwanza, Charles Mangula.
Alinishauri kununua dawa inayoitwa predator ni dawa ambayo huua majani na kuviacha vitunguu vikiwa na uhai wake kwenye uso wa ardhi, vilinyon'gonyea kwa muda wa wiki nzima ilibidi tuwekee mbolea ya Urea Kg 75 kwaajili ya kurudisha Ile ukijani uliotoweka baada ya kupulizia dawa hii ya kuua magugu, ikumbukwe pia hapo awali tuliweka mfuko mmoja na nusu wa mbolea ya DAP kg75.
Ndugu yangu unayenifuatilia katika Uzi huu nakutahadharisha ,si Kila eneo linafaa kulima vitunguu au zao lolote ,epuka kabisa kwenye mfumo wa maisha Yako kuwa mfano wa majaribio juu ya jambo fulani.Kwasababu ya kutaka mafanikio ya hara Mimi na kibarua wangu tulitegemea mvua zitakuwa msaada kwenye kumwagilia bahati mbaya sana mwaka huo mvua ziligoma.
Ardhi ya Meatu-Simiyu ilikuwa inatulazimisha kumwagilia angalau Mara tatu kwa wiki maana ukiacha ardhi inakuwa ngumu na vitunguu vinasinyaa mno tulipambana usiku na mchana tukihangaika Ili angalau tujikwamue katika shida Ile maana ake iligeuka kuwa shida badala ya fursa,ikumbukwe kuwa baada ya kuona mbegu zimebaki ililazimu kutafuta shamba la dharula Ili tuinusuru mbegu iliyokuwa kitaluni, tulikuwa tumejiandaa vya kutosha kwa vifaa na mtaji wakutosha hatukuwa na dhiki kabisa ya mahitaji.
Kwani kwa mkati tulio uweka tulitaka tupunguze usumbufu wa umwagiliaji wa mashamba yote mawili hivyo, ililazimu kuwa na Generator Moja iliyokuwa ikihudumia mashamba yote mawili, pipes mita 300 mita 150 Kila heka ,Mashine ya kupulizia dawa " kishani mariama"Moja ya pump nzuri sana, Mashine ya kutumia betri hivyo unapokuwa umechoka hunahaja ya kusukuma pump, pamoja na pump 6 manual "Matabi"Moja ya pump imara sana,na box la Kila aina ya dawa utafikiri tulitaka kuanzisha duka, tulikuwa tikijituma sana na kijana wangu wa kazi,rulishauriana kulala masaa kadhaa tu.
Ililazimu kulala saa 10 za jioni na kuamka saa 6 za usiku Ili kwenda kuwaangamiza wadudu waharibifu wa zao hili wanao anza mashambulizi nyakati za jioni na usiku mzima hivyo kuwapulizia dawa nyakati za usiku ni wazo lililo kuwa sahihi zaidi.
Hata hivyo mbali na changamoto hizi za kuvizia wadudu ililazimu Mimi nikamsaidie mfanyakazi wangu Ili asubhi niamkie majukumu mengine ya utumishi wa imma tulifanya hivyo kwa mafanikio makubwa lakini changamoto kubwa ikiwa ni kupishana na wanyama hatari na wakali kama vile tembo na fisi ukizingatia kuwa eneo la Meatu lote ni sehemu iliyomegwa kuwa makazi ambapo hapo awali ilikuwa ni makazi ya wanyama ( Maswa game reserve) hivyo wanyama kama tembo huwa wanaweka historia ya kurudia kupita eneo Moja kwa vizazi na vizazi.
Kwa historia Iko hivi tembo akipita eneo fulani akifa watoto wajukuu na vitukuu,watarudia kupita eneo hilohilo na njia Ile Ile walimopita ukoo wa mababu zao, hivyo ilikuwa hatari mno kwasababu hatukuweza kufahamu kuwa tembo anaweza kuwa wapi kwa wakati huo ukikumbuka kuwa tembo dume akisimama bila kukubughudhi unaweza kupita kwenye uvungu wa miguu yake ukidhani ni upenyo wa njia kwenye kichaka fulani.
Tulipambana kwa nguvu nyingi mno tukikabiliana na wanyama wadogo wadogo kama fisi ambao kwa mwanga wa tochi kali tulizikuwa tukizitumia wasingweza kuhimi maana zilikuwa na uwezo wa kumilika kilometers kadhaa kama hakuna kizingiti Cha vichaka na makazi ya watu.
ITAENDELEA...