Druggist
JF-Expert Member
- Nov 10, 2010
- 439
- 528
Naunga Mkono hoja:Ukiingia biashara yoyote mpya sharti ulipe school fees.Unatoa Pesa unapata Elimu:Na Elimu ni pamoja na kuangukia pua.
Pale ulipoanguka ndiyo kujifunza.Haijalishi umeplan Kwa Makini Kiasi gani, utakutana na Mambo hukuyatarajia.Msimu unaofuata,Amka,Anza tena.Utapunguza makosa kisha mafanikio yatakuja.Kama kila ukipata hasara unakimbia utakuwa mwanafunzi Hadi Kufa bila kuhitimu.Rafiki yangu aliamua kwenda kuchimba dhahabu.Yeye ni Mkandarasi mzoefu,aliweza kukusanya Mtaji mzuri.Akaniomba Ushauri,nikamwambia binafsi nimeshafanya Kazi hiyo nikiwa Shule,Kwa sasa hainivutii tena.Nikamshauri aingie ila ategemee hasara Mwaka wa Kwanza kisha Mwaka wa pili ataanza kupata Faida.Alipigwa hasara kama 85m hivi.Kila akipata hasara alikuwa ananitarifu.Nikawa nampa Moyo Akaze buti,ajifunze mbinu,wale wenye crushers,wenye elution plants,wale wa Maabara walikuwa wanamtega.Hatimaye akagundua mitego yote na sasa anazalisha 1Kg kila Mwezi.Hakuna Jambo jipya Chini ya mbingu.Kanuni ni Ile Ile,unapoanza Jambo jipya itakupasa kupata maarifa Kwa Njia chungu,ikiwemo kupoteza Pesa.Kama hutaki kupata hasara kaa na Pesa yako mfukoni.Wale wenye kupenda Kusoma Kuna kitabu Kinaitwa Midas Touch,kimeandikwq na Trump&Kiyosaki.Hawa Jamaa Katika baadhi ya sura wanaeleza jinsi walivyoingia chaka Katika biashara zao.Waweza download,ni free.