Kilimo cha vitunguu kwa mikoa ya Singida na Manyara

upo sawa mkuu kuna mbuga sana wasukuma wameshalewa na ndegu pekee na mahindi mazao ya umwagiliaji hawana habari nayo
 
Mkuu namtafu
Mkuu naomba unisaidie kumjua jamaa yangu sana anaitwa kisendi pastory huyu jamaa alikuwa anasomea mbeya (Afya) wadogo zake ni akina kushoka(shoka alikuwa na saloon hapo senta mahando.)

Kuhusu bikoni ni kweli lakini Kuna maeneo Bado hawajaweka pia Kuna maeneo yenye mito ambayo hukausha maji mwezi 10.

Nilikuwa huko mwezi huu mwanzoni na nimebahatika kupata heka2 zipo vzr tu wenyeji wangu ni family ya nyasi na kulwa msabato. Nadhani kama umesomea hapo umepata picha kamili mkuu.
 
hongera jamaa heka ulpata za kukodi ama kununua? na bei ya kukodi huwa ikojee....? maana mpka sasa sijaenda ila nkipata mda ntaendaa lazima
 
Njia ya Hydom kuna kijiji kinaitwa MWANGA ni maarufu sana kwa kulima vitunguu.


Manyara ni MANG'OLA ndiyo wanalima
 
hiyo njia naijua aisee kuna dr pale hydomu hospital alilima pale vitunguu alipata ml45 mkuu
Lakini biashara/project yeyote huwa rahisi/nyepesi sana ukiwa unasimuliwa.

Ila ingia ndani ukajionee mwenyewe, mambo huwa si rahisi kama watu wanavyosimulia hapa.

Hakunaga pesa inapatikanaga kirahisi, hapo kwenye milion 45 huenda mwenzio alitumia gharama hadi milion 30
 
jamaaa alitumia mtaji mkubwa sana sema hakuweka mambo yote hadhari..
 
jamaaa alitumia mtaji mkubwa sana sema hakuweka mambo yote hadhari..
Ndo hivo, mimi kuna mshikaji wangu alitoka mkoa flan kaenda KATAVI kulima vitunguu, amekaa huko mwaka mzima akiwa ameacha mke na watoto mkoa mwingine huku akiwa amewaambia kuwa anaenda kutafta.

Alikaa huko mwaka mzima, akalima vitunguu akavuna akauza akapata milion 5, akaja kupiga hesabu ya gharama aliyotumia kuanzia kuanzia kukodi shamba, mbegu, vibarua, mbolea n.k akajikuta amepata faida ya laki 4 tu.

Imagine umeacha mke na watoto mwaka mzima ukiwa umeenda kutafta alafu unarudi laki nne ya faida, yaani ilibidi hadi mke akaenda kumshtaki kwa baba ake mzazi (Baba mkwe wa mwanamke).
 
jamaa kuna sehemu alifeli kilimo nacho ni hesabu kali... yani uweke ml5 upate faifa lak4 kuna sehemu jamaa hakufanya inavyotakiwa
 
sijawahi lima kitunguu...ila ninaexperience furani kuhsu kilimo cha umwagiliaji... hiyo hela ingepata mchakarikaji ktk kilimo cha umwagiliaji jamaa angekuwa mbali sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…