Ndo hivo, mimi kuna mshikaji wangu alitoka mkoa flan kaenda KATAVI kulima vitunguu, amekaa huko mwaka mzima akiwa ameacha mke na watoto mkoa mwingine huku akiwa amewaambia kuwa anaenda kutafta.
Alikaa huko mwaka mzima, akalima vitunguu akavuna akauza akapata milion 5, akaja kupiga hesabu ya gharama aliyotumia kuanzia kuanzia kukodi shamba, mbegu, vibarua, mbolea n.k akajikuta amepata faida ya laki 4 tu.
Imagine umeacha mke na watoto mwaka mzima ukiwa umeenda kutafta alafu unarudi laki nne ya faida, yaani ilibidi hadi mke akaenda kumshtaki kwa baba ake mzazi (Baba mkwe wa mwanamke).