Kilimo cha vitunguu kwa mikoa ya Singida na Manyara

mkuu usemacho ni kweli kaabisa. lakini kaa ukijua kuwa kilimo ni target hiyo m45 kwa heka 10 alipata hasara au faida kidogo imagine kuna watu wameuzia gunia moja laki4? kiasi kwamba heka moja tu ukipata magunia 60 kwa bei hiyo una m24.

mimi mwaka jana nililima nyanya mkuu nimeuzia bei ya 26k shambani kwa dumu lita 20 na hadi namaliza mavuno bei ilikuwa 22-24k shambani na nilipata dumu 411 wastani wa m10 na sehemu nilipata gharama hazikufika m2. mtu ukimwambia haya anakataa ni basi tu watu hatujaamua kuwa serious na kilimo chenye tija
 
Mkuu ni heka ya nyanya makadirio nichume ndoo700-1000 bei iliyopita Kwa Sasa ni 17-20. Matarajio yangu nikute bei hata Iko 10k tu manake Bado Nina uhakika wa m7+
 
Attachments

  • IMG_20240509_142915_223.jpg
    2.5 MB · Views: 24
Heka ya vitunguu hiawezi kukupa gunia 60 mkuu.

KIkawaida ukifaulu sana heka itakupa gunia 40 au 45, au 50 kwa wanao loga πŸ˜…

Na ukifeli sana heka inakupa gunia 25
 
Heka ya vitunguu hiawezi kukupa gunia 60 mkuu.

KIkawaida ukifaulu sana heka itakupa gunia 40 au 45, au 50 kwa wanao loga πŸ˜…

Na ukifeli sana heka inakupa gunia 25
kipindi namaliza form 4 nilikimbilia pwani kisarawe mkuu sehemu mopja inaitwa vizembe hapo ni mtoni kijiji jina huwa linanitoka nakumbukum,buka tu vizembe mto ruvu. nilikutana na mkulima mmoja alikuwa anavuna gunia zaidi ya 70 kwa heka. na sisi ndo tulikuwa vibarua wake kuvuna hadi kupakia kwenye gari.
 
nyanya ukiipatia ina hela... mkuu
 
Maybe 😁😁😁

Lakini mimi nilizungumzia kwa singida na manyara.

Mkuu nitakuja pm unipe raman ya huko rufiji na mimi niende nikajaribu maana kitunguu kimeoanda sana bei mjini saivi
 
Usiweke matumani sana ukifanya kilimo hiki fanya tu kama hiyo pesa ya kufanya kilimo uliibiwa.
 
mkuu sipo rufiji nipo geita kwa sasa na ndo nyumbani kule nilienda kwenye kazi nyinyine tu ya kuchomaa mkaa. ndo nikawa kibarua wa mashambani tu

shida kubwa iko hapa mkuu wengi wanaingia kwenye kilimo kwa matamanio ya kuwa mamilionea kwa muda mfupi tena hawa wanasoma na ku google siju heka moja ya vitunguu inatoa magunia mangapi theni akiona gunia 100 anaona kuna pesa za bure hapa
 
mkuu sipo rufiji nipo geita kwa sasa na ndo nyumbani kule nilienda kwenye kazi nyinyine tu ya kuchomaa mkaa. ndo nikawa kibarua wa mashambani tu
Mimi ramani tu unitajie kijiji then research nitaenda kufanya mwwnyewe.

Maana hapa nipo kisarawe tayari ila sijawa mwenyeji bado
 
Mkuu huyo bado alikua mshindi Sana, kosa alilofanya ni kutoendelea na miaka mingine. Kuna faida nyingi Sana alizipata ambazo zipo inform of "experience". Hakuna utajiri wa halalali na wa kudumu utakaoutengeneza ndani ya mwaka 1.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…