kilimo kinalipa sana lakini ni bahati nasibu, nililima vitunguu, nyanya, tikiti, maharage na kufuga layers, mabadiliko ya tabia nchi, nyanya zikaharibiwa na mvua wiki la kwanza kuanza kuchuma, vitunguu hakuna uhakika wa kuvuna kwani huenda vikaenda na maji, vitakuwa tayari machi 20, tikiti zilioza baada ya mvua kujaza maji shamba, mahagwe ekari tatu yamekomaa, mvua inanyesha kupita kiasi-yataoza mengi,ekari mbili yanakaribia kukomaa pia. kuku wako wiki ya kumi
Zaidi ya milioni saba zimetumika, hasara tupu but najipanga upya kulima ekari tatu za nyanya(nimeshamwaga mbegu na kukodisha shamba) name kufuka broilers 300(wanakuja next wiki) ili kukuza mtaji, ukiingia kwenye kilimo jipange, vinginevyo utakufa kwa pressure.