Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Asante sana na mimi nimeipenda , ngoja nijipange nitakutafuta nimechoka kuajiriwa kwa kweli.
 
Nimeipenda, nipo mwanza natamani kufanya hivyo, mkuu maelezo tafadhali au nikupigie unipe maelekezo?
 

Mkuu Bagamoyo unalimia maeneo gani? Nina shamba langu Fukayosi sijuwi kama kunafaa kulima vitunguu huko.
 

Mkuu ulishawahi kuvuna mwezi wa 9 au wa 10 bei zake zikoje? Maana naona ndo sehemu nyingi wanalima na kuvuna muda huo.
 
Mkuu ulishawahi kuvuna mwezi wa 9 au wa 10 bei zake zikoje? Maana naona ndo sehemu nyingi wanalima na kuvuna muda huo.

Salama mkuu, huwa navuna miezi hiyo pia ila huwa ni maalumu kwa storage na sio kuuza manake bei yake huwa ndogo sana, kwa shamba huwa gunia linarange 45 - 55. Me vitunguu vya biashara huwa napanda mwezi wa tatu na kuvuna wasaba katikati.
 
Mkuu Bagamoyo unalimia maeneo gani? Nina shamba langu Fukayosi sijuwi kama kunafaa kulima vitunguu huko.

Bagamoyo nililimia pale mtoni mwaka jana nikavuna mwez wa tatu mwaka huu. Vilitoka poa sana.
 
Duka lipo wapi?

Ofisi ni kinondon studio ila biashara ya mbegu huwa nafanya kuanzia mwezi wa 11 mwishoni hadi mwezi wa 3 mwisho. Kwahiyo kwa sasa mbegu imekwisha mpaka mwezi wa kumi na moja manake kwa sasa ipo kwenye maandalizi. Ahsante na karibu.
 
Jamani hapo bagamoyo kuna mto?mnatumia nn kumwagilia?
 
mkuu asante kwa kutupa habari hiyo, nikirudi tena mvumi kilosa kulima vitungu ntakutafuta tena ngoja ni hifadhi contacts zako
 
Yah upo mto Ruvu, water pump ndo inayotumika.
Mkuu nataka kopo 10 kwanza za kujaribu. But nimekutumia meseji kwenye simu haijafika, ile namba pale juu ni sahihi?
 
Yah upo mto Ruvu, water pump ndo inayotumika.

mkuu ninampango wakununua water pup,ila sijajua ipi ni bora na kwa garama ipi?kwa shamba la hekari 1-2.pia vipi maji yakisima chakuchimba yanaweza yakafaa..naomb unisaidie kaka.
 
huo mto c unamafuriko kipindi cha mvua

Inategemea na shamba lako liko position gani kama liko usawa wa mto maji yatakusumbua, ila mimi shamba liko juu mto unapita mbali na shamba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…