Naona nondo za hatari sana humu,mpaka kichwa kina waka moto.Inafariji kwa kweli kuona vijana wakichakalika na zaidi wakiungana pamoja kufanya projects
mossad007,
Kubota na
Malila mnaonekana kuwa na uzoefu sana wa kilimo,binafsi nimependa kitendo cha kujiunga pamoja na moyo wenu wa kujitolea kutoa taarifa.
Ila nina mambo makuu mawili ambayo nafikiri yatasaidia wengi
1) humu jukwaani kumekuwa na taarifa nyingi za kilimo,mfano ni hii thread ya vitunguu.Lakini hamna sehemu ambayo mmeelezea kuhusu soko,kwa maana ya kwamba hizo sehemu mlizozitaja kuwa kitunguu kina Stawi vizuri wanunuzi huwa wanakuja mpaka shambani au inabidi kusafirisha mpaka sokoni,na soko lake lipo wapi hasa
2. Taarifa zimekuwa nyingi mno maana kila mtu anachangia kwa wakati wake,hivyo hakuna mtiririko sahihi.Mimi nilikuwa nawaomba mkuu
Malila na wenzako mliojiunga pamoja na wadau wengine mfanye mpango mtengeneze thread moja ambayo itatoa details kwa mtiririko mzuri kuanzia maandalizi,kupanda,kuvuna mpaka mategemeo ya soko,na pia mnapo kutana kwenye vikao au mnapoanza project fulani mtupe taarifa.Hili linaweza kuwa ni ombi lenye usumbufu kwenu lakini mkiona lipo ndani ya uwezo wenu basi mtusaidie wadau. Mnaweza kuanzisha group la whatsap ili iwe rahisi kufikisha taarifa.
Binafsi sipo kwenye position ya kuanza kilimo kwa sasa ila taarifa ni muhimu sana kwangu maana nategemea kuingia kwenye kilimo siku za usoni kwahiyo nahitaji taarifa nyingi iwezekanyo toka kwa wazoefu