Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Vuna na kuvihifadhi uje kupiga pesa mwezi wa Kwanza na wapili. Sasa hivi bei ni mbaya sana.

Mkuu hivi vitunguu vinaweza kutunzwa hadi miezi mingapi bila kuharibika? Mwezi wa kwanza na 2 bei huwa kiasi gani Kwa gunia? Asante.
 
Naomba niingizwe kwenye group please 0777476795.
 
mkuu naomba nikufate PM
 
sorry wadau! naona wadau mnatumia kitu inaitwa PM! nielewesheni mana cjui ninawezaje kuitumia
 
Wakuu naomba nitoe mrejesho wa kilimo cha vitunguu. Nililima ekari 3 na mavuno ni gunia 80 tu. Gharama nilizotumia kuvitunza vitunguu hadi kuvuna ni kama milioni 9 hivi.

Bei iliyoko huku shambani ni Tshs. 40,000 Kwa gunia la ndoo 8 a.k.a lumbesa. Kwa maana hiyo nikiuza Kwa bei hiyo nitaambulia kupata Tshs. milioni 3 na laki mbili tu. Kwahiyo sasa nimeamua kuvitunza Hadi mwezi wa pili mwakani na nitakuwa nauza rejareja Kwa ndoo elfu ishirini ili kurudisha pesa yangu niliyotumia.

Kwa kifupi ni kwamba mkulima anapunjwa sana. Muuzaji wa mwisho anapiga faida kubwa mno bila kutaabika. Kwa mfano naambiwa hilo gunia la ndoo 8 laweza kuwa na kilo zaidi ya 120 na bei ya kilo Kwa uchache Kwa sasa ni Tsh. 1500. Sasa 1500x120 = 180,000.

Kwa uzoefu huu nitaacha kulima niwe naenda kununua tu nakuja kuuza huku Dar. Mfano hizo milioni 9 zangu ningepata gunia 225 badala ya hizi 80 nilizovuna na taabu ya kuhudumia shamba n.k. Nimejifunza kitu.
 
Nilitaka kulima kitunguu ila nikaonaaa ujinga mtupu.
Bora kufuga KuKu...kilimo kazi sana...has a cha onion.
 
Nilitaka kulima kitunguu ila nikaonaaa ujinga mtupu.
Bora kufuga KuKu...kilimo kazi sana...has a cha onion.

Mkuu kitunguu kina gharama nyingi sijawahi kuona. Vile vile wanasema ekari moja unaweza kuvuna hadi gunia 80 sijuwi zinatoka wapi. Tulijitahidi kuvitunza Kwa kila hatua na mwisho wa siku mavuno ndo hayo.
 
Pole sana Mashauri kumekuwa na changamoto kubwa ya wadudu kwa maeneo ya mvumi mpaka Rudewa watafute jamaa wako pale Rudewa wanafahamika kama wachaga watakusaidia swala la soko
 
Mkuu kitunguu kina gharama nyingi sijawahi kuona. Vile vile wanasema ekari moja unaweza kuvuna hadi gunia 80 sijuwi zinatoka wapi. Tulijitahidi kuvitunza Kwa kila hatua na mwisho wa siku mavuno ndo hayo.

Umeonaa eee mkuuu..ni upotoshaji aiseeee...sitaki tena kusikia ishu za onion....bora ufugaji hauna longolongo
 
.Mkuu ingelikuwa vyema kama ungeweka mchanganuo wa namna hiyo 9M ilivyotumika, tujuze wapi palikuwa pagumu na mtiririko wa utendaji wako toka kupanda mpaka kuvuna, ulipanda majira gani, eneo gani, kwa mbolea gani?..lengo ni kutaka kujiridhisha na kujua kwanini imekuwa hivi.
 
Umeonaa eee mkuuu..ni upotoshaji aiseeee...sitaki tena kusikia ishu za onion....bora ufugaji hauna longolongo

Nataka nihamie kwenye nyanya nione inakuwaje ila vitunguu sina hamu navyo. Ni bora nikadunduliza pesa nikaja kununua huko mashambani na kuja kuuza Dar.
 
Mpaka nikae nianze kuviunganisha kimoja kimoja kwenye excel yangu. Maana orodha ni ndeeeeefuuuu
 
Mpaka nikae nianze kuviunganisha kimoja kimoja kwenye excel yangu. Maana orodha ni ndeeeeefuuuu

.itakuwa vyema Mkuu, ntakuwa hapa hapa nikingoja kukamilika kwa report yako, nasi tuna kiu ya kujifunza toka kwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…