Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Vuna na kuvihifadhi uje kupiga pesa mwezi wa Kwanza na wapili. Sasa hivi bei ni mbaya sana.

Mkuu hivi vitunguu vinaweza kutunzwa hadi miezi mingapi bila kuharibika? Mwezi wa kwanza na 2 bei huwa kiasi gani Kwa gunia? Asante.
 
Naomba niingizwe kwenye group please 0777476795.
 
Binafsi nalima kitunguu maeneo ya Kware Ruaha Mbuyuni hapa ni potential kw maana ya irrigation na ardhi ni nzur kw kitunguu. Hili zao linahitaj ujikamilishe kifedha unapoanza kulima ni muhimu ukaitenga pesa yake pemben kbsa kw heka inayohudumiwa vzur kila kitu inagarim million 3 ukiweka na lak 5 ya miscellaneous inakua vzur incase kuna mlipuko wa magonjwa km n'gonyo ambao wana athar kubwa na hugarim dawa kila baada ya siku kadhaa. Kware heka moja inakodishwa kw laki na nusu na pamp ya kumwagilia ni elf 50 jumla lak 2 mbegu huuzwa kw lita yale makopo yanayo nywewa mbege vilabuni ambapo kw kila lita ni elf 25 na heka moja inahitaj lita 10 ukiongeza mbili sio mbaya Kulima kw trekta ni sh elf 50 kw heka na ngombe ni 30 ila kw trekta ni nzur zaid cz inachimbua udongo vzur na hupunguza majan meng kuota halaf kuna kupengelenga hii ni kutengeneza majaruba kw ajili ya vitalu vya mbegu na yale ya kupandia shamban kw yale jaruba za mbegu hufanyaga sh 300 kw jaruba kw lita 10 unaweza pata jaruba 35 na zikizid bas kidgo sna halaf kw zile za shamban uwa wana charge kw heka ambapo kw heka wana pelenga laki na 20 hapo inabidi wasawazishe ardhi mana trekta linatifua sna ambapo kw heka wanafanya chini kbsa elf 10 ila wanaanzia elf 20.. Then kuna kupanda mbegu (Kuombeka) hapa ni sh 400 mpka 500 kw jaruba heka moja huwa na jaruba maxmum 400 halaf unapiga dawa ya kuzuia magugu weed stop na ile ya kuua majan yaliyo ota galgan au oxfan hizi ni elf 22 kw lita kw weed stop na unahitaj lita 4 kw heka kuna zile za kuua na kuzuia wadudu km DuDuba 13 kw ml 500 na unahitaj lita 1 kw heka na profercon elf 17 kw lita na unahitaj lita 2 kw heka na ile ya kuzuia ukungu kwenye majan ya kitunguu Amezeb elf 8 kw gram 500 na unahitaj kilo 1 kw heka then kuna mbolea apply after 2 wks urea elf 60 sehem nyngne mpka 66 kw mfuko na heka huitaj mifuko 4 then baadae CAN hii ni kw kukuzia mfuko elf 50-55 weka tena 4 ila dawa zinaweza kua constant kutokana na uwepo wa magonjwa pia gharama constant ni ya kumwagilia ambapo eka moja huitaj diesel lita 10-15 kutegemea na umbali wa shamba toka mtoni pia gharama za kijana atayemwagilia ambapo hudai elf 10-15 kw heka na pia wapiga dawa hudai elf 15 kw heka close supervision ni muhim sna inacse bajet inabana unaweza mwaga urea once then after 3-4 weeks ukapiga booster inaitwa super grow hii ni nzur sna kw kukikuza kitunguu jus elf 22 unapata lita nzima na inatosha kw heka nzima ukishapanda maji ni mara moja kw wiki kumwagilia na wakat wa kuvuna wanacharg 100-200 kw jaruba halaf kuna kukata majan ya kitunguu sh 2000 kw gunia. Eka moja iliyohufymiwa vzur hutoa gunia 70-80 na kila gunia ni elf 80 uwa inapanda mpka lak na 10 kikiwa adim na pia huweza kusguka mara chache mpka elf 70-75 ila average ni 80 kw shamban Vitunguu vya Ruaha Mbuyuni vinalimwa kiustad tofaut na singida au dodoma ivyo bei yake iko juu na huweza kulipa mara 3 mpka 4 zaid kw faida ila uhudumie vzur shamba.. Karibuni

mkuu naomba nikufate PM
 
sorry wadau! naona wadau mnatumia kitu inaitwa PM! nielewesheni mana cjui ninawezaje kuitumia
 
Wakuu naomba nitoe mrejesho wa kilimo cha vitunguu. Nililima ekari 3 na mavuno ni gunia 80 tu. Gharama nilizotumia kuvitunza vitunguu hadi kuvuna ni kama milioni 9 hivi.

Bei iliyoko huku shambani ni Tshs. 40,000 Kwa gunia la ndoo 8 a.k.a lumbesa. Kwa maana hiyo nikiuza Kwa bei hiyo nitaambulia kupata Tshs. milioni 3 na laki mbili tu. Kwahiyo sasa nimeamua kuvitunza Hadi mwezi wa pili mwakani na nitakuwa nauza rejareja Kwa ndoo elfu ishirini ili kurudisha pesa yangu niliyotumia.

Kwa kifupi ni kwamba mkulima anapunjwa sana. Muuzaji wa mwisho anapiga faida kubwa mno bila kutaabika. Kwa mfano naambiwa hilo gunia la ndoo 8 laweza kuwa na kilo zaidi ya 120 na bei ya kilo Kwa uchache Kwa sasa ni Tsh. 1500. Sasa 1500x120 = 180,000.

Kwa uzoefu huu nitaacha kulima niwe naenda kununua tu nakuja kuuza huku Dar. Mfano hizo milioni 9 zangu ningepata gunia 225 badala ya hizi 80 nilizovuna na taabu ya kuhudumia shamba n.k. Nimejifunza kitu.
 
Wakuu naomba nitoe mrejesho wa kilimo cha vitunguu. Nililima ekari 3 na mavuno ni gunia 80 tu. Gharama nilizotumia kuvitunza vitunguu hivi ni kama milioni 9 hivi. Bei iliyoko huku shambani ni Tshs. 40,000 Kwa gunia la ndoo 8 a.k.a lumbesa. Kwa maana hiyo nikiuza Kwa bei hiyo nitaambulia kupata Tshs. milioni 3 na laki mbili tu. Kwahiyo sasa nimeamua kuvitunza Hadi mwezi wa pili mwakani na nitakuwa nauza rejareja Kwa ndoo elfu ishirini ili kurudisha pesa yangu nuliyotumia. Kwa kifupi ni kwamba mkulima anapunjwa sana. Muuzaji wa mwisho anapiga faida kubwa mno bila kutaabika. Kwa mfano naambiwa hilo gunia la ndoo 8 laweza kuwa na kilo zaidi ya 120 na bei ya kilo Kwa uchache ni Tsh. 1500. Sasa 1500x120 = 180,000. Kwa uzoefu huu nitaacha kulima niwe naenda kununua tu nakuja kuuza huku Dar. Mfano hizo milioni 9 zangu ningepata gunia 225 badala ya hizi 90 nilizovuna na taabu ya kuhudumia shamba n.k. Nimejifunza kitu.

Nilitaka kulima kitunguu ila nikaonaaa ujinga mtupu.
Bora kufuga KuKu...kilimo kazi sana...has a cha onion.
 
Nilitaka kulima kitunguu ila nikaonaaa ujinga mtupu.
Bora kufuga KuKu...kilimo kazi sana...has a cha onion.

Mkuu kitunguu kina gharama nyingi sijawahi kuona. Vile vile wanasema ekari moja unaweza kuvuna hadi gunia 80 sijuwi zinatoka wapi. Tulijitahidi kuvitunza Kwa kila hatua na mwisho wa siku mavuno ndo hayo.
 
Pole sana Mashauri kumekuwa na changamoto kubwa ya wadudu kwa maeneo ya mvumi mpaka Rudewa watafute jamaa wako pale Rudewa wanafahamika kama wachaga watakusaidia swala la soko
 
Mkuu kitunguu kina gharama nyingi sijawahi kuona. Vile vile wanasema ekari moja unaweza kuvuna hadi gunia 80 sijuwi zinatoka wapi. Tulijitahidi kuvitunza Kwa kila hatua na mwisho wa siku mavuno ndo hayo.

Umeonaa eee mkuuu..ni upotoshaji aiseeee...sitaki tena kusikia ishu za onion....bora ufugaji hauna longolongo
 
Wakuu naomba nitoe mrejesho wa kilimo cha vitunguu. Nililima ekari 3 na mavuno ni gunia 80 tu. Gharama nilizotumia kuvitunza vitunguu hadi kuvuna ni kama milioni 9 hivi. Bei iliyoko huku shambani ni Tshs. 40,000 Kwa gunia la ndoo 8 a.k.a lumbesa. Kwa maana hiyo nikiuza Kwa bei hiyo nitaambulia kupata Tshs. milioni 3 na laki mbili tu. Kwahiyo sasa nimeamua kuvitunza Hadi mwezi wa pili mwakani na nitakuwa nauza rejareja Kwa ndoo elfu ishirini ili kurudisha pesa yangu niliyotumia. Kwa kifupi ni kwamba mkulima anapunjwa sana. Muuzaji wa mwisho anapiga faida kubwa mno bila kutaabika. Kwa mfano naambiwa hilo gunia la ndoo 8 laweza kuwa na kilo zaidi ya 120 na bei ya kilo Kwa uchache Kwa sasa ni Tsh. 1500. Sasa 1500x120 = 180,000. Kwa uzoefu huu nitaacha kulima niwe naenda kununua tu nakuja kuuza huku Dar. Mfano hizo milioni 9 zangu ningepata gunia 225 badala ya hizi 80 nilizovuna na taabu ya kuhudumia shamba n.k. Nimejifunza kitu.

.Mkuu ingelikuwa vyema kama ungeweka mchanganuo wa namna hiyo 9M ilivyotumika, tujuze wapi palikuwa pagumu na mtiririko wa utendaji wako toka kupanda mpaka kuvuna, ulipanda majira gani, eneo gani, kwa mbolea gani?..lengo ni kutaka kujiridhisha na kujua kwanini imekuwa hivi.
 
Umeonaa eee mkuuu..ni upotoshaji aiseeee...sitaki tena kusikia ishu za onion....bora ufugaji hauna longolongo

Nataka nihamie kwenye nyanya nione inakuwaje ila vitunguu sina hamu navyo. Ni bora nikadunduliza pesa nikaja kununua huko mashambani na kuja kuuza Dar.
 
.Mkuu ingelikuwa vyema kama ungeweka mchanganuo wa namna hiyo 9M ilivyotumika, tujuze wapi palikuwa pagumu na mtiririko wa utendaji wako toka kupanda mpaka kuvuna, ulipanda majira gani, eneo gani, kwa mbolea gani?..lengo ni kutaka kujiridhisha na kujua kwanini imekuwa hivi.
Mpaka nikae nianze kuviunganisha kimoja kimoja kwenye excel yangu. Maana orodha ni ndeeeeefuuuu
 
Mpaka nikae nianze kuviunganisha kimoja kimoja kwenye excel yangu. Maana orodha ni ndeeeeefuuuu

.itakuwa vyema Mkuu, ntakuwa hapa hapa nikingoja kukamilika kwa report yako, nasi tuna kiu ya kujifunza toka kwako.
 
Back
Top Bottom