Any place kwenye maji mengi Tanzania hii unaweza kulima vitunguu. Hata ukichimba kisima waeza kuanza kilimo cha vitunguu mkuu. Iringa kuna mashamba mengi yenye rutuba, Ruvu chini, Hata mikoani anywhere as long as una ardhi vitunguu yake maji tu.
nashukuru sana, vp khs upatkanaj wake? Mashamba n ya kununua au kukodi? Na gharama yake n ipi?
mkuu mashamba yako mengi tu ila inategemea wewe unatakaje. Yapo ya kukodi na ya kununua.
Kazi kwako.
Sasa kaka hekimatele, vipi kuhusu hizo gharama za kukodisha au kununua naweza kufahamu?
Wakuu wote nimewaelewa nimeongea na mtaalamu mmoja wa kilimo kaniambia joto sio ishu inawezekana kulima ila nizingatie haya mawili shamba lisiwe kwenye bonde linalohifadhi maji coz yataviozesha na pia ardhi isiwe ya udongo wa mfinyazi coz yatabana vitunguu kule chini na vitakua vidogo,research bado inaendelea thans sana wana jf
Hivi wadau kuna mbegu ya red Bombay huuzwa kwa lita 20, 200000? Me nilipata dukani gram 250,30000 ila kuna mshikaji wangu akaniambia Singida huwa zinapatikana 200000 kwa lita 20, mwenye kujua anijulishe tafadhali
Mkuu lita 20 kwa laki mbili wapi hyo, tupe ramani
Nimelima na nimenunua sina hamu kabisa na biashara hii wanaofaidi ni madalali wa pale kariakoo na kwingineko 10m ilikatika kama mchezo
Muda muafaka wakati was mvua usie JAn Feb pandikiza March Aptil panbana na magonjwa vuna June July faidi bei kubwa!!!
Mkuu Kubota nimependa mchanganuo wako, mimi niliwahi kulima vitunguu misimu miwili, msimu wa kwanza nilipata hasara ya shilingi laki tatu kwa kilimo cha heka moja. Msimu wa pili ndio ilikuwa funga kazi maana nilipata hasara ya 2 million kutoka kilimo cha heka mbili!! Changamoto nilozokutana nazo huku Arusha, bei ya kukodisha shamba ni kubwa, tulikuwa tunakodisha shamba sh 300,000 kwa heka. Bei ya pembejeo nayo iko juu sana kulinganisha na soko. Kuuza mazao wakati mzigo umejaa sokoni, yaani mali kuzidi mahitaji (demand na supply). Mwanzoni niliambiwa naweza kupata gunia 70-100 kwa heka, lakini sikuwahi kupata idadi hiyo ya magunia japo niliweka mahitaji yote kama inavyotakikana na kitunguu kilitoka vizuri sana kwa misimu yote. Tatizo kubwa nililiona wakati wa mauzo, hapa ndio mahali nilijua kilimo ni mwanaharamu na wakulima wataendelea kuwa maskini mpaka mwisho wa maisha yao kwa mtindo huu. Kitunguu hakipimwi kwa kilo huku bali kwa mtindo wa rumbesa. Unakuta gunia moja linabeba mpaka kilo 150. na bei yake haivuki 60,000 kwa gunia. Na mazingira yalivyo huuzi bila dalali, yaani pale ndio nilijua kwanini watu wengi wanalazimisha kubakia kwenye ofisi za kuajiriwa kuliko kujichanganya na kilimo. Na viongozi wetu hawana msaada wowote kwa huu uhuni tunaofanyiwa wakulima hasa wakati wa mauzo. Tatizo hili ni sugu na litaendelea kumfanya mkulima wa nchi hii kuwa maskini na kudharaulika daima (nadhani mmewahi kusikia msemo wa kejeli kama maisha yamekushinda kalime) Yaani kilimo kimegeuzwa kama sehemu ya kumkomoa mtu, eti utasikia ili kumkomoa mtu inabidi arudhishwe akalime, na ukijaribu kuangalia kama kweli mimi katika misimu yangu miwili ya kilimo cha kitunguu nimepata hasara unategemea nini?
Nini kifanyike, kama tunataka kweli kilimo iwe ni sehemu ya ajira inayolingana na jasho unalovuja ni lazima serekali iingilie kati na kusiwepo tena na manunuzi ya mazao ya mkulima kwa njia ya rumbesa bali kipimo iwe ni kwa kilo. Pembejeo zishushwe bei hata kama ni kwa ruzuku toka serekalini japo sidhani kama hili linawezekana kwani watunga sera za kilimo wao sio wakulima bali wafanya biashara. Iwapo sera haziboreshwa na kusimamiwa kwa umakini ni dhahiri wakulima hasa wadogo wadogo wataendelea kuwa maskini na mimi sintowashauri watu waache kazi za ajira huko maofisini hata kama wananyanyasika kwani huku kwenye kilimo ni kutafuta kufa siku si zako.
CC: Bavaria
Dah pole sana mkuu...nadhani ukitaka kulima usikodishe mashamba arusha ni gali sana...ungeenda manyara labdaMkuu Kubota nimependa mchanganuo wako, mimi niliwahi kulima vitunguu misimu miwili, msimu wa kwanza nilipata hasara ya shilingi laki tatu kwa kilimo cha heka moja. Msimu wa pili ndio ilikuwa funga kazi maana nilipata hasara ya 2 million kutoka kilimo cha heka mbili!! Changamoto nilozokutana nazo huku Arusha, bei ya kukodisha shamba ni kubwa, tulikuwa tunakodisha shamba sh 300,000 kwa heka. Bei ya pembejeo nayo iko juu sana kulinganisha na soko. Kuuza mazao wakati mzigo umejaa sokoni, yaani mali kuzidi mahitaji (demand na supply). Mwanzoni niliambiwa naweza kupata gunia 70-100 kwa heka, lakini sikuwahi kupata idadi hiyo ya magunia japo niliweka mahitaji yote kama inavyotakikana na kitunguu kilitoka vizuri sana kwa misimu yote. Tatizo kubwa nililiona wakati wa mauzo, hapa ndio mahali nilijua kilimo ni mwanaharamu na wakulima wataendelea kuwa maskini mpaka mwisho wa maisha yao kwa mtindo huu. Kitunguu hakipimwi kwa kilo huku bali kwa mtindo wa rumbesa. Unakuta gunia moja linabeba mpaka kilo 150. na bei yake haivuki 60,000 kwa gunia. Na mazingira yalivyo huuzi bila dalali, yaani pale ndio nilijua kwanini watu wengi wanalazimisha kubakia kwenye ofisi za kuajiriwa kuliko kujichanganya na kilimo. Na viongozi wetu hawana msaada wowote kwa huu uhuni tunaofanyiwa wakulima hasa wakati wa mauzo. Tatizo hili ni sugu na litaendelea kumfanya mkulima wa nchi hii kuwa maskini na kudharaulika daima (nadhani mmewahi kusikia msemo wa kejeli kama maisha yamekushinda kalime) Yaani kilimo kimegeuzwa kama sehemu ya kumkomoa mtu, eti utasikia ili kumkomoa mtu inabidi arudhishwe akalime, na ukijaribu kuangalia kama kweli mimi katika misimu yangu miwili ya kilimo cha kitunguu nimepata hasara unategemea nini?
Nini kifanyike, kama tunataka kweli kilimo iwe ni sehemu ya ajira inayolingana na jasho unalovuja ni lazima serekali iingilie kati na kusiwepo tena na manunuzi ya mazao ya mkulima kwa njia ya rumbesa bali kipimo iwe ni kwa kilo. Pembejeo zishushwe bei hata kama ni kwa ruzuku toka serekalini japo sidhani kama hili linawezekana kwani watunga sera za kilimo wao sio wakulima bali wafanya biashara. Iwapo sera haziboreshwa na kusimamiwa kwa umakini ni dhahiri wakulima hasa wadogo wadogo wataendelea kuwa maskini na mimi sintowashauri watu waache kazi za ajira huko maofisini hata kama wananyanyasika kwani huku kwenye kilimo ni kutafuta kufa siku si zako.
CC: Bavaria
Dah pole sana mkuu...nadhani ukitaka kulima usikodishe mashamba arusha ni gali sana...ungeenda manyara labda