Muda muafaka wakati was mvua usie JAn Feb pandikiza March Aptil panbana na magonjwa vuna June July faidi bei kubwa!!!
Mkuu Kubota nimependa mchanganuo wako, mimi niliwahi kulima vitunguu misimu miwili, msimu wa kwanza nilipata hasara ya shilingi laki tatu kwa kilimo cha heka moja.
Msimu wa pili ndio ilikuwa funga kazi maana nilipata hasara ya 2 million kutoka kilimo cha heka mbili!! Changamoto nilozokutana nazo huku Arusha, bei ya kukodisha shamba ni kubwa, tulikuwa tunakodisha shamba sh 300,000 kwa heka. Bei ya pembejeo nayo iko juu sana kulinganisha na soko. Kuuza mazao wakati mzigo umejaa sokoni, yaani mali kuzidi mahitaji (demand na supply).
Mwanzoni niliambiwa naweza kupata gunia 70-100 kwa heka, lakini sikuwahi kupata idadi hiyo ya magunia japo niliweka mahitaji yote kama inavyotakikana na kitunguu kilitoka vizuri sana kwa misimu yote.
Tatizo kubwa nililiona wakati wa mauzo, hapa ndio mahali nilijua kilimo ni mwanaharamu na wakulima wataendelea kuwa maskini mpaka mwisho wa maisha yao kwa mtindo huu. Kitunguu hakipimwi kwa kilo huku bali kwa mtindo wa rumbesa. Unakuta gunia moja linabeba mpaka kilo 150. na bei yake haivuki 60,000 kwa gunia.
Na mazingira yalivyo huuzi bila dalali, yaani pale ndio nilijua kwanini watu wengi wanalazimisha kubakia kwenye ofisi za kuajiriwa kuliko kujichanganya na kilimo. Na viongozi wetu hawana msaada wowote kwa huu uhuni tunaofanyiwa wakulima hasa wakati wa mauzo.
Tatizo hili ni sugu na litaendelea kumfanya mkulima wa nchi hii kuwa maskini na kudharaulika daima (nadhani mmewahi kusikia msemo wa kejeli kama maisha yamekushinda kalime) Yaani kilimo kimegeuzwa kama sehemu ya kumkomoa mtu, eti utasikia ili kumkomoa mtu inabidi arudhishwe akalime, na ukijaribu kuangalia kama kweli mimi katika misimu yangu miwili ya kilimo cha kitunguu nimepata hasara unategemea nini?
Nini kifanyike, kama tunataka kweli kilimo iwe ni sehemu ya ajira inayolingana na jasho unalovuja ni lazima serekali iingilie kati na kusiwepo tena na manunuzi ya mazao ya mkulima kwa njia ya rumbesa bali kipimo iwe ni kwa kilo.
Pembejeo zishushwe bei hata kama ni kwa ruzuku toka serekalini japo sidhani kama hili linawezekana kwani watunga sera za kilimo wao sio wakulima bali wafanya biashara. Iwapo sera haziboreshwa na kusimamiwa kwa umakini ni dhahiri wakulima hasa wadogo wadogo wataendelea kuwa maskini na mimi sintowashauri watu waache kazi za ajira huko maofisini hata kama wananyanyasika kwani huku kwenye kilimo ni kutafuta kufa siku si zako.
CC: Bavaria