Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Mkuu tindo tatizo lako dogo tu. Ilikuwa mara ya kwanza kulima ulipaswa uanze kidogo ili ujifunze kwa gharama kidogo. Biashara yoyote unapoianza mara ya kkwanza mieleka ni kawaida, kama unapojifunza kuendesha baiskeli.

Mtu asitarajie anapoanza jambo kwa mara ya kwanza apige bingo haiko hivyo. Pia ukae ukijua kuwa kunapokuwa na mafuriko ya zao sokoni wanunuzi wote na si madalali peke yao hunyanyasa sana wakulima. Hali hiyo ipo katika kilimo cha nyanya pia.

Mkoa wa Morogoro ukilima nyanya za kiangazi mwezi wa nane hadi wa kumi na moja huwa kuna mafuriko ya nyanya. anaevuna miezi hiyo na kkama ni mara yake ya kwanza ataapa kwamba nyanya si biashara. Kuna msemo huku NYANYA NINYANYUE NYANYA NINYANYASE. Soko zuri la vitunguu ni mwwezi March hadi June. Ukiweza kuwa na kitunguu majira hayo huna maumivu. wateja wanakutafuta na unaweza kuuza kwa utaratibu unaotaka wewe. wakati huo wewe mwenye mali ndio mjanja. suala la madalali linakuwa halina umuhimu na wala si lazima upeleke sokoni na hata ukipeleka sokoni mzigo wako utagombaniwa.

Tumia utaallam uweze kuhifadhi kitunguu uweze kulifikia soko la Mwezi March, au lima vitunguu uvune February au uvune kuanzia mwezi May hadi July. Ukilima kitunguu cha msimu ambacho kila mtu analima maumivu yake ndiyo hayo.

Kwenye suala la soko kunapokuwa na mafuriko hakuna serikali itakayokusaidia hapo utakuwa umeumia tu. wewe mkulima ndiyo unatakiwa uchemshe bongo kuona utalifikia vipi soko la mwezi March hadi July. Hii miezi hakuna dalali atakae kunyanyasa. Na pia sio lazima upeleke mzigo sokoni kunawanunuzi wazuri tu hufuata mazao mashambani. watu wengi wanafanikiwa sana kwa kuuzia mashambani. kama huna uzoefu afadhari ukauzia shamba ukapata bei utakayoridhika nayo kuliko kwenda mjini ukakutana na madalali wajanja ukarudi kijijini na story tu huna pesa mfukoni.

Kwa hiyo Mkuu kila biashara inachangamoto zake. Tumia muda mwingi kujifunza kwa wazoefu badala ya kulalamika hivyo. Ulikosea kuanza kwa kulima pakubwa ukapata hasara ukarudia makosa yaleyale kwa kulima pakubwa zaidi huku hujarekebisha kilichokutia hasara ulipo anza. Ushauri wangu msimu wa kwanza jifunze mbinu za kilimo cha vitunguu uzijue changamoto zake.

Msimu unaofuata boresha uzalishaji kwa kutatua changamoto, pata ushauri kwa wazoefu. Panua eneo kadri unavyopata uzoefu. Hata kama unauwezo mkubwakifedha usianze kuwekeza eneo kubwa kama huna uzoefu. Usivutiwe na takwimu tamu unazosikia nyingi hufikiwa na wazoefu na nyingi ni exagerated.

Ukizalisha eneo dogo inakupa picha halisi itakayokufanya uamue iwapo kilimo hicho kinalipa au la. Na hapo ndiyo utaamua kupanua eneo la shamba kwa kutokana na picha halisi uliyoiona na changamoto zake.
 

Asante mkuu. Hii inamaanisha heka 1 naweza pata magunia 100. Je vipi bei ya vitunguu sokoni?
 
Wadau thid year nililima na nimevuna hivi punde nitarudi kuwapa experience ndogo niliyojifunza.
 

Mkuu...asante sana kwa maelezo yako. Hii mimi naichukulia kama ndiyo notisi "desa" la kilimo cha vitunguu, especially kwa hapo Ruaha Mbuyuni.
 

Thanks... very useful information.
 

Mkuu...miezi 6 ishapita, vipi mrejesho wa hiyo research yako?
 
Hongera Mkuu Kwa Kufikia Hapo Maana Najua Haikuwa Kazi Rahisi
Sio kazi rahisi kweli, lakini there should always be a starting point. Na hapa ndio nilipoanzia na nimejifunza kwa kweli na nitawashirikisha nanyi wenzangu najua kipo cha kujifunza.
 
Habari zenu wadau.
Kama nilivyowaeleza hapo awali nita share experience ndogo niliyoipata katika kilimo cha kitunguu nilichoingia kufanya mwaka huu katika kijiji cha Igawa Mbalali.

Kwanza kabisa shamba langu lilikuwa na ukubwa wa 0.6 eka(Nililipima kwa kutumia GPS) hapa kitu nilichopata ni kwamba kwa ukubwa huu ambao kabla sijalipima niliambiwa ni eka moja, bahati mbaya nilipima wakati nimeshalilipia na kupanda tayari.

Katika shamba hili nilifanikiwa kukata vijaruba 202, na nilipanda mwezi wa saba mwanzoni na nimevuna mwezi huu wa 11 mwanzoni, gharama za kuendesha shamba hili ambapo kwangu ni kama shamba darasa ilifika 2.9m

Lesson learnt
1. Kitunguu ambacho wenyeji wanasadiki kuwa ni chenye faida mara nyingi ni kile kinacholimwa kuanzia mwezi wa 3 au 4 na kutolewa mwezi wa 6 au 7. Au kinacholimwa mwezi 7 au 8 na kutolewa wa 11 au 12 kwa ajili ya kuhifadhi kwenye Ghala.

2. Upandaji, kutokana na ugeni na kutofahamu mambo mengi, upandaji haukufuata utaratibu kwa baadhi ya jaluba na hivyo kubananisha vitunguu. Upandaji unaotakiwa ni ule maarufu wanasema upandaji wa umbali wa kiberiti.

3. Kitunguu nilichopanda mimi ni cha umwagiliaji, hapa napo kuna changamoto lukuki, ukimpata kijana mwaminifu gharama huwa chini kwani mara nyingi wanachakachua sana mafuta. Kijana aliyesimamia shamba langu alikuwa ni majanga tu.

4. Utunzaji wa shamba unahitaji ukaribu sana hasa kipindi chs kupiga dawa na kupiga mbolea. Usipoangalia utakuwa unanunulia wengine mbolea. Pia dawa, kwa kipindi ambacho nilipanda mimi huhitajika dawa nyingi kwa kuwa ni kipindi ambacho kunakuwa na wadudu wengi. Pia nilishambuliwa na wadudu wanaitwa kantangaze hawa wadudu kwa kweli ni balaa ila niliwatuliza kwa dawa moja inaitwa Belt.

5. Uvunaji, kwa kweli kama walivyochangia wadau wengine kipindi cha uvunaji hutakiwi kuingiza maji mengi kwenye jaluba, pia ukivuna omba mungu mvua isikukute maana vikinyeshewa na vikiwa vimesha katwa basi hapo ndio mwisho wa hadithi.

6. Uuzaji, ndugu zangu kama nilivyosema hapo juu kuhusu mvua, vitunguu vyangu vilinyeshewa, ila nashkuru ilikuwa bado havijakatwa ndio kwanza vimetoka kung'olewa. Hapo kwa kweli thamani ya kitunguu changu ilishuka, hata hivyo niliuza gunia kwa 50,000 na vile vilivyopasuka gunia 30,000. Ukweli ni kwamba kipindi hiki ambacho nimevuna vitunguu ni vingi sokoni, hivyo baadhi kipindi hiki vitunguu vyao huhifadhi gharani hadi Januari ambapo bei huwa juu kidogo na ya kuridhisha.

7. Mwisho ningependa kuwashirikisha wenzangu na kuwaambia ya kwamba vitunguu vina pesa ila ukilima kwa wakati sahihi, sehemu sahihi, kilimo na usimamizi sahihi.

Kwa kipindi hiki kitunguu kimenikata, sijapata faida ila kwa niliyojifunza katika awamu hii naamini ni silaha muhimu katika msimu ujao na lazima nifanikishe endapo Mungu akipenda nikawa hai, nitatoboa tu. Nitajitahidi mwezi wa tatu nitakuwa nishapanda Mungu akipenda.

Kwa wale wanaolima maeneo haya hasa kilimo cha umwagiliaji nasema nimeshakaribia tuendeleze mapambano.

Aluta kontinua, daima mbele nyuma mwiko.
davidson689@hotmail.com
 
Hongera sana. Hiyo sasa ndio nature ya biashara. Baada ya hapo utafanikiwa. Ushauri wangu uangalie hayo uliyojifunza na ubashiri changamoto nyinginezo ambazo zinaweza kutokea na jinsi ya kuzikabili. Kila lakheri
 
Kilimo cha vitunguu kinaweza kukutoa kama kutakuwa na usimamizi mzuri, binafsi nililima hekari 3 maeneo ya Mtandika lakini wenyeji walichonifanya sitaki hata kukumbuka, mimi natuma hela kama wanavyotaka kwa ajili ya dawa, mbolea na matunzo mengine kumbe jamaa hawana habar na shamba, siku nimeenda nikakuta kwanza hekar moja ilishakufa nilitamani niite trekta lisafishe mpaka vile vilivyopo.

Kama unataka hiki kilimo tafuta vijana waaminifu na sio wenyeji halafu ujitahid kutembelea hata mara moja kwa wiki ila ukilima kwa simu utajuta.
 
Binafsi nina plan ya kuanza kilimo hiki maeneo ya Butuja, mkoani Mwanza. Ila ningependa kufahamu kama kuna mtu ana uzoefu na eneo hilo ama alishawahi fanya zoezi hilo katika kijiji hiko! Msaada wenu nitaendelea kushukuru sana.

Maana tangu mwanzo mwa thread hii hadi hapa kuna mengi mno ya kujifunza.

Kilimo niinue.
 

Pole kwa changamoto mkuu. Naamin mrejesho wako ujao panapo uhai utakuwa ni wa mikakati ya jinsi gani uliliendea soko na faida lukuki. Kaza buti mkuu wengine tupo nyuma yenu.
 
Pole kwa changamoto mkuu. Naamin mrejesho wako ujao panapo uhai utakuwa ni wa mikakati ya jinsi gani uliliendea soko na faida lukuki. Kaza buti mkuu wengine tupo nyuma yenu.

👍🙏 thanks mkuu harakati zinaendelea.
 
Naomba lifunguliwe group la whatsapp, tujadili vizuri na kubadilishana mawazo kwa urahisi zaidi, wenye kujifanya ni ma-admin halafu kumbe matapeli haipendezi tunarudishana nyuma kimaendeleo na sio ungwana
 
Naomba lifunguliwe group la whatsapp, tujadili vizuri na kubadilishana mawazo kwa urahisi zaidi, wenye kujifanya ni ma-admin halafu kumbe matapeli haipendezi tunarudishana nyuma kimaendeleo na sio ungwana
Umeongea point toxic
 
wadau naomba mdau anayefaham kilimo hiki aniambie mbegu ikashatoka kwenye kitalu kwenda shambani ni wakati gani wa kuweka mbolea na aina gani kwa eneo la mkoa wa Dodoma na mpangalio wa dawa ni ipi inaanza na kias gani mpaka kuvuna.
 
Mkuu wiki ya pili au ya tatu inafaa kutia mbolea lakini pia inategemeana na mtiririko wa mvua,kwa mpangilio wa dawa pia utaangalia kama kuna mashambuliza ya wadudu ambao mara nyingi husababishwa na uotaji wa majan shambani so ili kuAvoid inabid shamba liwe safi mda wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…