Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

ahsante mkuu pale unapootesha hamna haja ya mbolea? na mbolea ya aina gani mkuu DAP, CAN, UREA,SA,..... kuna mdogo wangu huwa analima huko huwa anajitahidi sana ila anapata mazao kidogo
 
kiongozi hongera sana

Na pole kwa changamoto hizo kilimo ndivyo kilivyo,

KILIMO kinahitaji, 1. elimu sahihi ya hilo zao unalotaka kulima, 2. ulime kwa kutime soko,

Naomba nikusaidie kidogo hapo katika RED NILIPOBOLD huyo mdudu wakulima wanyemuita Kanitangaze, SI KANITANGAZE (Tuta Absoluta). Kanitangaze harisi (Tuta Absoluta) hashambulii vitunguu yeye anashambaulia mimea ya jamii ya Solanacea family, kama Nyanya, viazi mviringo, bilinganyi, hoho,mnavu etc

ISIPOKUWA HUYO MDUDU MUHARIBIFU WA VITUNGUU HASA VIKIWA VIMEHAMISHIWA SHAMBANI NI CUTWORM/CATEPILLER/AMERICAN BOLLWORM, YEYE HUKATA MAJANI YA KITUNGUU MPAKA SHINA-MDUDU HUYU KWA MENEO YA RUAHA MBUYUNI-IRINGA NI MAARUFU SANA KWA JINA LA NG'ONYO.

DAWA ULIYOTUMIA NI SAHIHI, MAANA HUYO NI KIWAVI (LARVA), NA HATA HUYO WA NYANYA NAYE ANAPOKUWA KATIKA HIYO STAGE YA KIWAVI (LARVA) WANAFANANA SANA NA HUYO LARVA WA KITUNGUU. NA DAWA HIYO ULIYOTUMIA YA BELT NI MOJA WAPO YA DAWA ZINAZOANGAMIZA HAO VIWAVI

SIKU NYINGINE UKIKOSA BELT, TAFUTA MOJAWAPO YA HIZI DAWA , MATCH, AU EVISECT, AU DURSBAN, AU FURADAN, KARATE 5EC, RAMDEX 5%EC, NINJA, NIMBECIDENE, PEGASUS AU PROVE 1.92 EC, METHOMEX, BLAST, AU DIMETHOATE, AU ATTAKAN ETC... ZIPO NYINGI


NAKUTAKIA MAFANIKIO

 
Check mwega/malolo-kilosa district kuna skimu ya umwagiliaji kule kitunguu inakubali saaana.mpaka mwezi wa nane 2010. Kitunguu gunia moja likiwa kijijini mwega 120,000-150,000
hayo ni moja ya maeneo yangu ya kazi
mkuu nitakutafuta, hii jamii forum version mpya inazingua kuku pm siwezi
 
aisee mkuu nitakucheki na nitakufanyia tour kwenye shamba lako, ushirikiano wako plz
 
HAHAAAAA HII NDIO TANZANIA MKUU, ALAFU UTASIKIA WATU WANASHABIKIA MPAKA 2020 TUTAKUA UCHUMI WA KATI! ETI MAGUFULI ATAFANYA MAMBO.........DUH NCHI YANGU HII
 
wadau mimi mgeni ndani ya jamii hii nahitaji kupata taarifa za jinsi ya kuingia katka kilimo cha kitunguu kupata gharama zote kwa yule anaejua maeneo ya mbalali au pengne kwa mkoa wa mbeya kwani ndo maeneo niliyopo
 
MKUUHASARA KAMA HIZI MTU HAWEZI KUZIKWEPA KWA KUPIGA HESABU MVUA ZITAANZA KUNYESHA BAADA YA MUDA GANI NA MAZAO YANGU YATAKUA YAMEFIKIA HATUA GANI ILI KAMA MVUA ZITAYAHARIBU USIPANDE UPANDE KATIKA MUDA AMBAO MVUA HAZITAYAKUTA BADO HAYAJAVUNWA? NA HAO KUKU LAYERS HASARA YAKE IMEKUJAJE MKUU HEBU TUFAFANULIE TUJIFUNZE TUJENGE NCHI TUACHE KUCHEKWA
 
Naomba lifunguliwe group la whatsapp, tujadili vizuri na kubadilishana mawazo kwa urahisi zaidi, wenye kujifanya ni ma-admin halafu kumbe matapeli haipendezi tunarudishana nyuma kimaendeleo na sio ungwana

Hilo group lishafunguliwa?
 
wadau mimi mgeni ndani ya jamii hii nahitaji kupata taarifa za jinsi ya kuingia katka kilimo cha kitunguu kupata gharama zote kwa yule anaejua maeneo ya mbalali au pengne kwa mkoa wa mbeya kwani ndo maeneo niliyopo

Huu uzi umeelezea mengi sana.
Ushauri: anza kupitia kuanzia page ya kwanza kabisa. Mpaka ukifika page ya mwisho utakuwa umejifunza mengi.
 
Water pump nakushauri utafute zile za kusukwa na mafundi, huwa zinauzwa kuanzia laki 9 ila huwa ni imara na inavuta maji mengi sana, ndan ya saa moja unakua ushamwagia eneo la ekari moja. Ila hizi za madukan za laki 3 hazifai kwa kilimo serious.
hizo pump za kusuka zinapatikana wapi?
 
Hilo group lishafunguliwa?
Habari zenu wakuu! Huu uzi ni mzuri kwa wale wakulima wa kitunguu ningependekeza na kutilia mkazo kweli lingeundwa group humu la whatsapp kwa wale wadau ili tuwe na umoja wetu tukutane tupange na kueleweshana mikakati juu ya kilimo cha kitunguu naona itakuwa jambo jema kwa wale wageni kama mimi kupata uelewa mpana wa kilimo hichi
 
Tafadhali sana kabla ya kulima ni vizuri sana ukafanya marketi analysis, kujua ni wakati gani bei inakuwa nzuri.

Napia uwe makini na eneo ulilopo,kwa mfano kama morogoro wanaanza Kuivisha nyanya nyingi mwezi wa 4, na wewe uko na nyanya zako nyingi mwezi huo huo Iringa au mbeya utapata bei mbovu maana wanunuzi wengi watavamia Morogoro mpaka ziiishe ndio watakuja hiyo mikoa mingine, mtu hawezi acha nyanya morogoro akaenda mbeya.

KATIKA KITUNGUU si kila wakati kitunguu kinakuwa na bei nzuri hizo tsh 100,000+ , miezi ya kuingiza kitunguu sokoni ni November (70,000tsh) to June 170,000+), baada ya hapo vingi vinaaza kutoka mabondeni, na mashamba ya mpunga, bei huporomoka sana
 
Nashukuru sana ndg kwa msaada wako.
 
Check mwega/malolo-kilosa district kuna skimu ya umwagiliaji kule kitunguu inakubali saaana.mpaka mwezi wa nane 2010. Kitunguu gunia moja likiwa kijijini mwega 120,000-150,000
hayo ni moja ya maeneo yangu ya kazi
Naomba ruhusa yako mkuu nikutafute
 
Wadau mim ni mkuwa wa vitunguu ila sijawahi kulima kipindi cha masika nataka nijaribu kipindi hiki nalimia mkoani dodoma naomba mwenye experience wa kulima kipindi hiki anipe ushauri nini changamoto risk ikoje na namna ya anavyokabiliana nayo
Ulikijaribu kitunguu cha masika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…