ulifikia wapi mkuu na tafiti yako?Safi sna mkuu,
Haya ndio mawazo tunataka hapa JF,
Kuna technolojia mpya na rahisi mno nimeinyaka sehemu juu ya huu ulimaji bado naimalizia resecrh yake nafikiri baada ya miezi sita itakua imekamilika nitaimwaga hapa jamvini.
Kifupi inawezekana kabisa kuchagua ukubwa wa kitunguu chako, kukuza ndani ya miezi miwili tu na kuchangua shape ya kitunguu.
Hii nikiikamilisha nitaileta hapa maana nafikiria kuteka soko lote la Comorro, Kenya na Zanzibar kwa vitunguu bora kabisa na vya bei nafuu na hakuna atakaye shindana na mie.
Pole kwa yaliyokukuta. Bado unaendelea na kilimo cha vitunguu?Wakuu naomba nitoe mrejesho wa kilimo cha vitunguu. Nililima ekari 3 na mavuno ni gunia 80 tu. Gharama nilizotumia kuvitunza vitunguu hadi kuvuna ni kama milioni 9 hivi. Bei iliyoko huku shambani ni Tshs. 40,000 Kwa gunia la ndoo 8 a.k.a lumbesa. Kwa maana hiyo nikiuza Kwa bei hiyo nitaambulia kupata Tshs. milioni 3 na laki mbili tu. Kwahiyo sasa nimeamua kuvitunza Hadi mwezi wa pili mwakani na nitakuwa nauza rejareja Kwa ndoo elfu ishirini ili kurudisha pesa yangu niliyotumia. Kwa kifupi ni kwamba mkulima anapunjwa sana. Muuzaji wa mwisho anapiga faida kubwa mno bila kutaabika. Kwa mfano naambiwa hilo gunia la ndoo 8 laweza kuwa na kilo zaidi ya 120 na bei ya kilo Kwa uchache Kwa sasa ni Tsh. 1500. Sasa 1500x120 = 180,000. Kwa uzoefu huu nitaacha kulima niwe naenda kununua tu nakuja kuuza huku Dar. Mfano hizo milioni 9 zangu ningepata gunia 225 badala ya hizi 80 nilizovuna na taabu ya kuhudumia shamba n.k. Nimejifunza kitu.
Mkuu zile mbegu huwa mavuno yake siyo mazuri sana.....chukua hiyo ya dukan uwezekano wa kuota ni 90%Hivi wadau kuna mbegu ya red Bombay huuzwa kwa lita 20, 200000? Me nilipata dukani gram 250,30000 ila kuna mshikaji wangu akaniambia Singida huwa zinapatikana 200000 kwa lita 20, mwenye kujua anijulishe tafadhali
Ahsante mkuu kwa mrejesho. mimi ndio nataka kuanza. nilishangaa sana eti mbegu lita 20 kwa ekari. kwanza mbegu kipimo ni kilo sio lita mbegu za vitunguu sio majikiukweli waliokuwa wanatushawishi kulima niwaongo, ni vigumu kupata hizo gunia 100 wastan ni gunia 40. pia nimeamin wengi wao nahisi niwafanyakaz wa maeneo hayo kwa hiyo wanakuwa wanakupiga kwenye mbegu. mimi mwaka jana nimejaribu ila nilikuwa tofauti na wenzangu mimi nilinunua lita moja tu za mbegu. kiukweli ni mbegu nyingi sana kwa ufupi wasiozijua ni vimbegu vyenyewe ni saiz ya mbegu ya nyanya . na baada ya kuzihudumia nilifanikiwa kupanda zote na chache zilibaki, pia sikutaka kubana sana kama wengi wetu wanavyoshauri humu eti size ya kiberiti.
kuhusu dawa mara nyingi nilipulizia dawa ya kuzuia wadudu tu tena mara moja kwa wiki kopo nilikuwa nanunua buku tano mpaka navuna nilitumia kopo kumi ambayo total ilikuwa 50000.
mbolea kwetu huku zipo za kununua mchanganyiko ila mimi nilinunua mfuko mmoja mmoja kwa kila mbolea na bei zake kwa mbeya ni
urea 48000
can48000
npk nilikuwa nanunua ya unga inauzwa 5000 na kila baada ya siku 14
sa 45000
uchumi haukuwa mzuri sikununua dap
kuandaa kitalu mpaka kupandikiza jumla ya matumizi ilikuwa35000 na mimk mwenyewe nilikuwa nashiriki.
nilivuna jumla gunia25 kwa eka moja.
NILICHOJIFUNZA
watu wanadanywa kuhusiana mbegu hivo wanajikuta wananunua mbegu nyingi na kumwaga shamban. hata wakati wakupandikiza vitunguu vinabanwa sana hivyo mbegu nyingi inakufa au mkulima anajikuta anapata vitunguu vidogovidogo vingi sana badala ya vile vya wastan. pia mbolea inatakiwa iwekwe kila baada ya siku ishirini na moja na ingependeza upandikize kwa mstari hata wakat wa kumwaga mbolea ufuatishe mstari badala ya kumwaga ovy sabab ukimwaga onyo wakati wakumwagilia mbolea inaweza sombwa na kujikuta ni sehem moja ndo imenawili tena kwa muono wangu ni vyema kupitisha mstari wa kishimo pembeni ya mstari wa vitunguu na uksha mwaga ufukie.
kwa ushauri wangu ni vyema kama ndo unaanza ushiriki mwenye kwa usaidiz wa wafanyakazi kuna uongo mwingi sana unaenezwa ambao ndo unawaliza wengi humu. mtu anakwambia unahukika wa kuvuna gunia 100. wadau gunia linalozungumzwa hapa sio kilo mia ni debe nane ambalo si chini ya kg 130 sasa hata ukiingia kenyanseed.com hizo mbegu za red bombay na redcreole wamekadilia kg 10000 per hectare ambazo ni acre 2.5 pia kitunguu kwa jinsi nilivoona ukijitoa mwenyewe kwa usimamizi mzuri hupaswi kufikisha gharama ya milion. pia tusikariri maeneo mfano lumuma wenyeji washakuwa matapeli wanapokuona mgeni wenyewe wanachofikiria ni kukukamua tu. pamoja na kuwa bei haikuwa nzuri lakini nashukuru gharama yangu ilirudi na faida pia. twenden shamban lakini kabla ya yote tutafute information bila kukurupuka. love you all. sikuwahi kulima ila mwaka huu mungu bariki ntalima kila kitu mpaka nyanya
Natamani sana nianze kilimo cha vitunguu maji,nahitaji msaada wa watu wanaolima vitunguu maji maeneo ya Mto RUVU ( nimesikia kuna watu wanalima Ruvu) au kama kuna watu wanaolima kitunguu maeneo ya Kilwa Masoko sehemu iitwayo Makangaga. Kama kuna mtu analima katika haya maeneo naomba tuwasiliane pia ningependa nifahamu kuhusu Masoko
[ATTACHView attachment 330346=full]330346[/ATTACH]View attachment 330346