Hello comrades
Naomba ushauri kwa yeyote mwenye utaalamu au uzoefu wa hiki kilimo
Baada ya kuona fursa kwenye kilimo cha vitunguu swaumu, nilishawishika kuanza kulima.
Baada ya uchunguzi wa awali kuhusu aina ya udongo, tabia nchi na upatikanaji wa maji, nilitafuta na kupata shamba maeneo ya Tunduma ambalo lilikuwa na sifa zinazotakiwa kwa kilimo cha vitunguu.
Nilianza maandalizi ya shamba, na nikaamua kupanda kwa batches, na batch ya kwanza vimeshatoka, vina wiki ya tatu. Kuna issue moja ambayo sikuiangalia vizuri wakati natafuta eneo, nayo ni jua. Recently nimegundua kuwa shamba langu liko kwenye ukanda wa jua kali hasa kipindi cha kiangazi na wakati utaalamu unaonyesha kuwa ili kitunguu swaumu kikue vyema kinahitaji jua lililopoza.
Je, Kuna namna yoyote Naweza kucontroll jua ili mimea istawi vyema? Natanguliza shukrani