Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Hilo la mvua inaweza kuwa kweli kak..
Nilipanda kitunguu heka 5, nilipo anza kuvuna siku hiyo hiyo ilinyesha mvua kiangazi nikala hasara sikupata kitu
Mkuu hiyo ilikuwa ni kipindi gani
(Mwezi wa ngapi)..?
 
Ndio kitunguu hakipatani na mvua haswa kikiwa kimekomaa,kikiwa kichanga hakuna shida hvyo zingatia kukilima kikomae kiangazi,pia ardhi yako iwe na matoleo ya maji maana kama.maji si ya kusimama pia hakitoharibika ,na kuna variety mfano tajirika ya east west vinavumilia maji mengi hata vikiwa vimekomaa,lazima utazame shamba kwanza .kulima eka haizidi milioni mbili kwa kila kitu yaani from kukodi shamba mpaka mavuno
 
Jamani mm nimelima vitunguu mkoani mbeya katika kijiji cha igawa natarajia kuvuna jumatatu tarehe 18/7/2016 tatizo ni bei imeshuka mno. Gunia huku watu wananunua kwa shilingi elfu sitini tu (60) je, wapi nitapata soko zuri naombeni ushauri wana jamvi
 
Jamani mm nimelima vitunguu mkoani mbeya katika kijiji cha igawa natarajia kuvuna jumatatu tarehe 18/7/2016 tatizo ni bei imeshuka mno. Gunia huku watu wananunua kwa shilingi elfu sitini tu (60) je, wapi nitapata soko zuri naombeni ushauri wana jamvi
 
Vitunguu na hoho vyote vinahitaji udongo tifutifuti, au tifutifu kichanga,USIWE MFINYANZI, muda mzuri wenye bei nzuri ya kitunguu na hoho ni November- May, Kitunguu by November huanza na bei ya 100,000-150,000 tsh.

Mavuno kwa eka moja ya kitunguu wastani ni gunia 70 kama mbegu ni OPV,kama mbegu ni local mavuno ni gunia 50@ kilo 120. Kama mbegu ni hybrid F1/ Chotara mavuno maximum kwa eka 1 ni gunia 120.

AGRONOMY YA KITUNGUU.KIASI cha mbegu cha kutosha eka 1.

Kitunguu maji utahitaji kilo 1 na ziada ya gram 200 kama imergency cost ya mbegu ni kuanzia 180,000-460000 kutegemea na mbegu/ aina ( Hybrid au OPV).

Ni vyema ukaanza na mbegu aina OPV kama vile Red Cleore,au Red Bombay anza na hizi OPV coz si gharama sana hyo mbegu kiasi cha 1.2 kgs zaweza uzwa maximum tsh 360000 zatosha eka1, utahitaji mifuko 2 ya Mbolea ya kupandia mbolea kama DAP au Yara Miller Winner au NPK utahitaji hizo mbolea wakati ukisia mbegu kitalu na wakati wa kutransplant cost ya mifuko 2 ni 180,000 kama siyo mbolea za Yara, coz mbolea za Yarra ni ghari zaidi, miche ya kitunguu hukaa kitaluni wiki6-8.

Shambani itakaa siku 90, utahitaji mifuko 3 ya mbolea ya kukuzia CAN, cost ni kama tsh 240,000, utahitaji booster pia lita 2 kama super grow etc utahitaji dawa za wadudu kama decis, imidaclopid au duduall etc utahitaji dawa 2 za wadudu tofauti angalau lita 2, gharama ya booster na dawa za wadudu ni kama tsh 120,000, SOKO zuri la kitunguu ni mwezi November- May,bei hufika tsh 150,000 - 250,000tsh by May kwa gunia 1.

JUMLA KUU YA gharama ya kuzalisha kitunguu kwa eka 1 ni wastani wa 1.8 -2.5 Million.


[/COLOR][/SIZE]
aani wachangiaji wengi hapa, sio wakulima nahisi ni watu wakusikia kuhusu kilimo, sijaona mchango wowote unaoweza kumsaidia mleta mada pamoja na mimi, @kilimomaarifa, tunakuomba huku.
 
Maeneo Mengi ya Morogoro yanafaa kwa kilimo cha vitunguu. maarufu sana ni eneo la Ruaha mbuyuni mpakani mwa Morogoro na Iringa. Maji ni ya kutosha maana mto Ruaha upo karibu.

Eneo ni tambarare power tiller inweza tembea vema bila kutumia mafuta mengi na wala kuharibika mara kwa mara. Unaweza punguza matumiz ya maji kwa kutumia mfumo wa umwagiliaji kwa matone (drip irrigation).

Ukilima kitunguu au nyanya kwenye tent (screenhouse) ni bora zaidi kwa matumizi ya maji, nafasi na unaweza zalisha mwaka mzima kwa kupanga unataka kumata soko la wapi, wakati gani ambao wazalishaji wa kawaida hawana cha kuvuna, then bei yako itakuwa juu, na faida tele.

Njoo tuongee kwa utani.
 
hi
hiyo bei ni kwa mikoa ipi...au soko lipi?..
 
IRINGA-RUAHA MBUYUNI, DAR-ES-SALAAM-KARIAKOO, NA ZANZIBAR-MWANAKWEREKWE
Mkuu naomba kujua kampuni zenye uhakika wa mbegu bora ya kitunguu, nina ekari 2 pale kijiji cha Kware Ruaha nataka nikaweke mbegu mwezi huu wa nane japo sijui msimu utanibeba, kwani nilitaka kupanda mwezi wa nne nikastukia bei ilibidi nipige tikiti kuzuga
 
HESABU ZA KUPANDA KITUNGUU KWA SASA ZINAGOMA, MAANA ILITAKIWA UKIVUNE NOVEMBER, HIKI UNACHOPANDA UTAKIVUNA JANUARY AU FEBRUARY, BEI NI NZURI LAKINI HUTOKIVUNA COZ MASIKA ITAKUWA IMEANZA KITAOZA.

MAKAMPUNI YA MBEGU WAPO BALTON TANZANIA-WANAOFISI ZAO PALE KISOLANZA NEAR MAFINGA BARABARANI KABISA, WAPO KIBOSEED, AFRI ASIA, WAPO SEEDCOL, TRY KUTAFUTA OPV VARIETIES TU KWANZA USIANZE NA HYBRID F1 KAMA WAKINA NEPTUNE ETC, TAFUTA RED CLEORELE AU RED BOMBAY, KWA EKA UNAHITAJI KILO 1.5, ANDAA KATI YA 250,000 HADI 380, 000TSH.



E
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…