Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Huko ndio wapi mkuu?

Na bei zikoje kwa kununua ama kukodi?
Na unavyosema maji yapo mengi ni yakisima.,mto ama ni kilimo cha kutegemea mvua?

Swali la nyongeza ni mazao gani yanastawi zaidi eneo hilo?

Ahsanteni wakuu.
 
Wakuu salamu.

Nataka kuanzisha kilimo cha umwagiliaji cha kitunguu. Naomba ushauri wenu ni maeneo gani yanayoofaa kwa kilimo cha kitunguu na hasa ambayo yanaweza kuwa na maji kwa ajili ya umwagiliaji.

Nimenunua power tiller ambayo nategemea itanisaidia sana kwenye kilimo cha umwagiliaji!

Kilimo Kwanza!


hivi dawa gani za wadudu wa kwenye vitunguu zinafaa, dawa zipi za ukungu wa kwenye vitunguu zinafaa, mbolea ipi nzuri kwa kitunguu, booster ipi nzuri kwa kitunguu...
 
  • Thanks
Reactions: DBA
Gharama nilizoingia wakati nalima

[TABLE="width: 877"]
[TR]
[TD]Activity[/TD]
[TD]Elaborations[/TD]
[TD]Calculations[/TD]
[TD]Acre 1[/TD]
[TD]Acre 2[/TD]
[TD]Acre 3[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kukodi [/TD]
[TD] [/TD]
[TD]250000*1[/TD]
[TD="align: right"]250000[/TD]
[TD="align: right"]500000[/TD]
[TD="align: right"]750000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kutifua[/TD]
[TD] [/TD]
[TD]100000*1[/TD]
[TD="align: right"]100000[/TD]
[TD="align: right"]200000[/TD]
[TD="align: right"]300000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Arrow[/TD]
[TD] [/TD]
[TD]70000*1[/TD]
[TD="align: right"]70000[/TD]
[TD="align: right"]140000[/TD]
[TD="align: right"]210000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kutengeneza majaruba[/TD]
[TD] [/TD]
[TD]600*100[/TD]
[TD="align: right"]60000[/TD]
[TD="align: right"]120000[/TD]
[TD="align: right"]180000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kupanda[/TD]
[TD] [/TD]
[TD]500*100[/TD]
[TD="align: right"]50000[/TD]
[TD="align: right"]100000[/TD]
[TD="align: right"]150000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Mbolea[/TD]
[TD] [/TD]
[TD]70000*2[/TD]
[TD="align: right"]140000[/TD]
[TD="align: right"]280000[/TD]
[TD="align: right"]420000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Mbegu[/TD]
[TD] [/TD]
[TD]30000*7[/TD]
[TD="align: right"]210000[/TD]
[TD="align: right"]420000[/TD]
[TD="align: right"]630000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Dawa[/TD]
[TD]Majani (Megasate)[/TD]
[TD]20000*3[/TD]
[TD="align: right"]60000[/TD]
[TD="align: right"]120000[/TD]
[TD="align: right"]180000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] [/TD]
[TD]Wadudu (Profecron)[/TD]
[TD]20000*3[/TD]
[TD="align: right"]60000[/TD]
[TD="align: right"]120000[/TD]
[TD="align: right"]180000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kumwagilia[/TD]
[TD] [/TD]
[TD]200000*1[/TD]
[TD="align: right"]200000[/TD]
[TD="align: right"]400000[/TD]
[TD="align: right"]600000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Palizi (Kupiga Godi)[/TD]
[TD] [/TD]
[TD]700*100[/TD]
[TD="align: right"]70000[/TD]
[TD="align: right"]140000[/TD]
[TD="align: right"]210000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Palizi ya Pili[/TD]
[TD] [/TD]
[TD]700*100[/TD]
[TD="align: right"]70000[/TD]
[TD="align: right"]140000[/TD]
[TD="align: right"]210000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Mlinzi[/TD]
[TD] [/TD]
[TD]700000*1[/TD]
[TD="align: right"]700000[/TD]
[TD="align: right"]700000[/TD]
[TD="align: right"]700000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kung'olea[/TD]
[TD] [/TD]
[TD]600*100[/TD]
[TD="align: right"]60000[/TD]
[TD="align: right"]120000[/TD]
[TD="align: right"]180000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kukata Majani[/TD]
[TD] [/TD]
[TD]700*100[/TD]
[TD="align: right"]70000[/TD]
[TD="align: right"]140000[/TD]
[TD="align: right"]210000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]My travel costs[/TD]
[TD] [/TD]
[TD]100000*5[/TD]
[TD="align: right"]500000[/TD]
[TD="align: right"]500000[/TD]
[TD="align: right"]500000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Emergency[/TD]
[TD] [/TD]
[TD] [/TD]
[TD="align: right"]500000[/TD]
[TD="align: right"]700000[/TD]
[TD="align: right"]900000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Total[/TD]
[TD] [/TD]
[TD] [/TD]
[TD="align: right"]3170000[/TD]
[TD="align: right"]4840000[/TD]
[TD="align: right"]6510000[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
what is this?
 
mimi nataka kulima vitunguu na nyanya nipo kwenye maandalizi by the way ekari moja waweza pata gunia ngapi kwa makadirio
 
mimi nataka kulima vitunguu na nyanya nipo kwenye maandalizi by the way ekari moja waweza pata gunia ngapi kwa makadirio


Me pia nimeufuatilia sana uzi huu.

But for the case of your question, hebu soma uzi huu wote kuanzia mwanzo utapata jibu la swali lako and other more useful information. Kuna wakuu ( Kubota na Bavaria ) kwenye uzi huu wameelezea vizuri sana in details (with experience) kuhusu kilimo cha Vitunguu.

-Kaveli-
 
Tu
mwaka jana baada ya kusoma thread jf na kusisimuka nikaamua kwenda mang'ola karatu arusha yaani wanakodisha shamba kwa 500,000 kwa mwaka ,nikaamua kujifanya mnunuzi nikatembezwa na madalali bei ilikuwa ina range 60000 to 80,000
mwaka huu nataka nikatafiti hukon singida


Tunasubiri mrejesho mkuu
 
Tuache ubinafsi kama wakulima Na kuunganisha nguvu zetu pamoja,Masoko ni mengi hatuja yafikia Na wenzetu Jirani wananunua kwetu Na kupeleka mbali kwa Faida Kubwa.

Mwisho, tufanye mnyororo wa thamani baada ya kuvuna ili vionekane bora Na kuvutia machoni mwa watumiaji
 
Inategemeana na unataka kulima wapi (sehemu utakayoweza ku manage shamba vizuri na kwa ukaribu) , source ya maji (mvua au umwagiliaji) itakayo determine msimu utakaolima (masika au kiangazi ).

Kifupi, bei huwa nzuri kuanzia December mpaka April. Hapa katikati bei zinaathiriwa na uwingi wa kitunguu sokoni. Unaweza ukalima ili uvune mwezi December, au ukalima na kukihifadhi mpaka hiyo miezi bei zikikaa vyema.
 
Inategemeana na unataka kulima wapi (sehemu utakayoweza ku manage shamba vizuri na kwa ukaribu) , source ya maji (mvua au umwagiliaji) itakayo determine msimu utakaolima (masika au kiangazi ). Kifupi, bei huwa nzuri kuanzia December mpaka April. Hapa katikati bei zinaathiriwa na uwingi wa kitunguu sokoni. Unaweza ukalima ili uvune mwezi December, au ukalima na kukihifadhi mpaka hiyo miezi bei zikikaa vyema.
Hapo upo sahihi....Dec mpaka April ni hatari sana
 
Milioni moja?
Inategemea unalimia wapi?
Inategemea umwagiliaji kwa pampu au mifereji au mvua
Uzoefu wangu huku Kilosa huu:
Mbegu lita 7 kwa ekari @ 25,000/= jumla 175,000/=
Kuandaa kitalu 20,000/=
Kusia mbegu 10,000/=
kutunza kitalu 30,000/=
kukodi shamba 100,000/=
kufyeka shamba 48,000/=
kukatua udongo 64,000/=
kulainisha udongo 48,000/=
kutengeneza majaruba 25,000/=
kupandikiza 160,000/=
dawa ya kuua magugu 40,000/=
palizi mara mbili 100,000/=
Mbolea mifuko mitatu 210,000/=
Mtu wa kuweka mbolea mara mbili 10,000/=
madawa kuua wadudu na magonjwa 50,000/=
mpiga dawa wiki kumi 50,000/=
kung'oa 50,000/=
kukata vitunguu gunia mia 200,000/=
usafiri 100,000/=
chanja kukodi 100,0000
umwagiliaji petrol 2500 x lita 5 x wiki 10 = 125,000/=
mtu wa kumwagilia 5000 x wiki 10 = 50,000
JUMLA KUU = 1,855,000/=

Kwa wastani ni mil 2
Asante
 
Mimi na mwenzangu tushalima vitunguu mara moja tukafanikiwa kurudisha capital na faida juu, japo sio tulitegemea. Na tunajipanga tena. Hii kitu hii sio lelemama.

Unapaswa kwenda benet nayo, kuanzia kusia, transplanting, majaruba hakikisha yanawekwa vizuri, umwagiliaji, palizi, madawa etc process zote ushuhudie, shirikisha locals majirani wenye uzoefu wakupe sifa ya udongo wako na hekari zako. Mambo ya kupiga simu, kutuma hela na kuagiza mtu akuangalizie ww upo busy na issue zingine, ninakuhakikishia utapigwa mimba. Ama la weka dogo au mtu una uhakika na yy ana machungu na huo mradi akusaidie kama upo busy sana.

Jambo jingine ninahisi hizi mvua zinazotokeaga from nowhere kipindi cha kuvuna vitunguu ni ndumba na uchawi sometimes, locals wanakuwaga na wivu design. Heard this stories na nimesoma humu. I have confirmed
 
Back
Top Bottom