chalii wa ara
JF-Expert Member
- Sep 30, 2013
- 1,063
- 931
Wakuu ni wapi naweza pata mbegu halisi ya Red Bombay yenye warranty? maana kumekuwa na mbegu fake zikiwa labeled as Red bombay while th'r not kitu ambacho kina athiri sana wakulima wa zao hili
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nenda katika taasisi zilizothibitishwa kama Balton,East Africa seed etc sasa inategemea na eneo ulilopo .Ila kama kweli ni chalii wa ara Balton wana Brach hapoWakuu ni wapi naweza pata mbegu halisi ya Red Bombay yenye warranty ??? maana kumekuwa na mbegu fake zikiwa labeled as Red bombay while th'r not kitu ambacho kina athiri sana wakulima wa zao hili
Utapata Arusha, kwenye kibo seed company....Wakuu ni wapi naweza pata mbegu halisi ya Red Bombay yenye warranty ??? maana kumekuwa na mbegu fake zikiwa labeled as Red bombay while th'r not kitu ambacho kina athiri sana wakulima wa zao hili
uko sawa mkuu watu wanaelezewa faida tu bila changamoto
Asiyefanya kazi na asile, ndiyo neno sahihi hapa hilo uliloliweka haliendani na maudhui.Mathayo 6:33 Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
33 Lakini utafuteni kwanza Ufalme wa mbinguni na haki yake, na haya yote mtaongezewa.
you need a revelation to understand that word!Asiyefanya kazi na asile, ndiyo neno sahihi hapa hilo uliloliweka haliendani na maudhui.
Kumbuka habari ya Isaka kuchimba visima kwa umwagiliaji na ufugaji enzi hizo na huyu ni mtoto wa ahadi. Maombi bila matendo ni zero.
msweet vpMathayo 6:33 Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
33 Lakini utafuteni kwanza Ufalme wa mbinguni na haki yake, na haya yote mtaongezewa.
Message yote ndefu ya nini kwenye post ya kilimo?you need a revelation to understand that word!
to help you: biblia inaposema utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake na hivi vyote mtazidishiwa
kwanza unatakiwa uelewe; ufalme wa mbinguni nini? na kuutafuta ufalme wa mbinguni ni kufanya nini?
ufalme wa mbinguni ni ule ufalme wa Mungu Muumba wa mbingu na nchi, kumbuka kuna ufalme wa kuzimu,wa shetani
kuutafuta ufalme wa mbinguni ni kujitoa katika ukuaji wa ufalme wa mbinguni hapa duniani,
tunajitoaje katika ukuaji wake?
kupitia kuombea watu kuokoka,kushuhudia watu waokoke,kuchangia katika ueneaji wa injili kwa nguvu,akili,na mali zetu,
ukuaji wa ufalme wa mbinguni ni injili kuenea na kuwafikia watu wengi zaidi na kuwatoa kutoka kwenye ufalme wa mbinguni
Yesu alitufundisha namna ya kuomba ktk Mathayo6:9-15
9In this manner,therefore,pray: Our Father in heaven, hallowed be thy name
10 Your kingdom come.......
watu wengi hawajui kuomba, ndio maana maombi hayajibiwi,Ni lazima uombee ufalme wa mbinguni kwanza kabla ya kuleta maombi yako, kwa maelekezo zaidi kuhusu namna ya kuomba kutokana na jinsi Yesu alivyofundisha nitafute
kwahiyo, biblia inaposema kuutafuta ufalme wa mbinguni kwanza haimaanishi usifanye kazi, bali kazi uifanyayo iwe kwaajili ya ukuaji wa ufalme wake, then utapokea baraka zake kupitia kazi yako,maana kazi yako inamtukuza yeye na inasaidia ukuaji wa injili yake
MF:unapoomba Mungu akupatie Pesa, mke nk...Ili isaidie nini kwenye ufalmewake? hujaona watu wanapata pesa wanakuwa walevi wa kutupwa na kufa? wengine wamepata wake kwa hisia zao wamepata stress mpaka wamejiua!
Lakini unapoomba unamwambia Mungu, naomba ubariki kazi ya mikono yako ili nikutumikie kwa pesa zako katika kuupeleka mbele ufalme wako au nipatie mke mwema ili niweze kukutumikia wewe nikiwa nae! God will answer you immediately according to His time
This is the mystery of the kingdom of God
It is a revelation
Note: This is not applicable to anyone who is not righteous before God
halafu hiyo sijaweka hapo, ni signature yangu, ila pata mafunuo hayo
msweet nadhani na wewe umeelewa sasa
sitaki kuamini kama na wewe ni mzembe wa kufikiriMessage yote ndefu ya nini kwenye post ya kilimo
msweet vp
Endelea na injili maana tutaharibu Uzi bure by the way posting a wrong comment in unrelated post is spamming.sitaki kuamini kama na wewe ni mzembe wa kufikiri
asante rafki anguPowas....!!!!! Mie ninakuelewa vizuri sana ndugu yangu chief1.... Ni lazima tuifanyie kazi Mathayo 6:33 na kuwa our life style/ our way of life.... Tupo pamoja sana.
sawa boss, nimekoseaEndelea na injili maana tutaharibu Uzi bure by the way posting a wrong comment in unrelated post is spamming.
Unadhani kwanini kuna neno la wakati? Maneno yote ktk Biblia ni muhimu lakini neno la kumfaa mtu katika jambo fulani mara nyingi ni neno la WAKATI.
Uwe na amani ndugu na hii umeonyesha hekima sana.sawa boss, nimekosea
Yani Lita ishirini kwa heka 1 duu unapandaje iyo mbegu na km ni kitalu si utapiga kitalu kwenye shamba zima la heka 1Wakuu salamu.
Nataka kuanzisha kilimo cha umwagiliaji cha kitunguu. Naomba ushauri wenu ni maeneo gani yanayoofaa kwa kilimo cha kitunguu na hasa ambayo yanaweza kuwa na maji kwa ajili ya umwagiliaji.
Nimenunua power tiller ambayo nategemea itanisaidia sana kwenye kilimo cha umwagiliaji!
Kilimo Kwanza!
Milioni moja?
Inategemea unalimia wapi?
Inategemea umwagiliaji kwa pampu au mifereji au mvua
Uzoefu wangu huku Kilosa huu:
Mbegu lita 7 kwa ekari @ 25,000/= jumla 175,000/=
Kuandaa kitalu 20,000/=
Kusia mbegu 10,000/=
kutunza kitalu 30,000/=
kukodi shamba 100,000/=
kufyeka shamba 48,000/=
kukatua udongo 64,000/=
kulainisha udongo 48,000/=
kutengeneza majaruba 25,000/=
kupandikiza 160,000/=
dawa ya kuua magugu 40,000/=
palizi mara mbili 100,000/=
Mbolea mifuko mitatu 210,000/=
Mtu wa kuweka mbolea mara mbili 10,000/=
madawa kuua wadudu na magonjwa 50,000/=
mpiga dawa wiki kumi 50,000/=
kung'oa 50,000/=
kukata vitunguu gunia mia 200,000/=
usafiri 100,000/=
chanja kukodi 100,0000
umwagiliaji petrol 2500 x lita 5 x wiki 10 = 125,000/=
mtu wa kumwagilia 5000 x wiki 10 = 50,000
JUMLA KUU = 1,855,000/=
Kwa wastani ni mil 2
serikali haiwezi wasaidia. njia pekee ni wakulima kuungana na kutafuta soko kwa pamoja.Mkuu Kubota nimependa mchanganuo wako, mimi niliwahi kulima vitunguu misimu miwili, msimu wa kwanza nilipata hasara ya shilingi laki tatu kwa kilimo cha heka moja. Msimu wa pili ndio ilikuwa funga kazi maana nilipata hasara ya 2 million kutoka kilimo cha heka mbili!! Changamoto nilozokutana nazo huku Arusha, bei ya kukodisha shamba ni kubwa, tulikuwa tunakodisha shamba sh 300,000 kwa heka. Bei ya pembejeo nayo iko juu sana kulinganisha na soko. Kuuza mazao wakati mzigo umejaa sokoni, yaani mali kuzidi mahitaji (demand na supply). Mwanzoni niliambiwa naweza kupata gunia 70-100 kwa heka, lakini sikuwahi kupata idadi hiyo ya magunia japo niliweka mahitaji yote kama inavyotakikana na kitunguu kilitoka vizuri sana kwa misimu yote. Tatizo kubwa nililiona wakati wa mauzo, hapa ndio mahali nilijua kilimo ni mwanaharamu na wakulima wataendelea kuwa maskini mpaka mwisho wa maisha yao kwa mtindo huu. Kitunguu hakipimwi kwa kilo huku bali kwa mtindo wa rumbesa. Unakuta gunia moja linabeba mpaka kilo 150. na bei yake haivuki 60,000 kwa gunia. Na mazingira yalivyo huuzi bila dalali, yaani pale ndio nilijua kwanini watu wengi wanalazimisha kubakia kwenye ofisi za kuajiriwa kuliko kujichanganya na kilimo. Na viongozi wetu hawana msaada wowote kwa huu uhuni tunaofanyiwa wakulima hasa wakati wa mauzo. Tatizo hili ni sugu na litaendelea kumfanya mkulima wa nchi hii kuwa maskini na kudharaulika daima (nadhani mmewahi kusikia msemo wa kejeli kama maisha yamekushinda kalime) Yaani kilimo kimegeuzwa kama sehemu ya kumkomoa mtu, eti utasikia ili kumkomoa mtu inabidi arudhishwe akalime, na ukijaribu kuangalia kama kweli mimi katika misimu yangu miwili ya kilimo cha kitunguu nimepata hasara unategemea nini?
Nini kifanyike, kama tunataka kweli kilimo iwe ni sehemu ya ajira inayolingana na jasho unalovuja ni lazima serekali iingilie kati na kusiwepo tena na manunuzi ya mazao ya mkulima kwa njia ya rumbesa bali kipimo iwe ni kwa kilo. Pembejeo zishushwe bei hata kama ni kwa ruzuku toka serekalini japo sidhani kama hili linawezekana kwani watunga sera za kilimo wao sio wakulima bali wafanya biashara. Iwapo sera haziboreshwa na kusimamiwa kwa umakini ni dhahiri wakulima hasa wadogo wadogo wataendelea kuwa maskini na mimi sintowashauri watu waache kazi za ajira huko maofisini hata kama wananyanyasika kwani huku kwenye kilimo ni kutafuta kufa siku si zako.
CC: Bavaria