Mkuu wale madalali wa kariakoo ni jibu, mil 10 niliteketeza pale , wana hila usiombeungetueleza ilikuwaje hd ukapata hasara ingetusaidia sana
Mkuu mashamba ya kukodi kwa hiki kilimo yanapatikana mikoa gani.kwa wepesi.?IRINGA-RUAHA MBUYUNI, DAR-ES-SALAAM-KARIAKOO, NA ZANZIBAR-MWANAKWEREKWE
Mimi na mwenzangu tushalima vitunguu mara moja tukafanikiwa kurudisha capital na faida juu, japo sio tulitegemea. Na tunajipanga tena. Hii kitu hii sio lelemama. Unapaswa kwenda benet nayo, kuanzia kusia, transplanting, majaruba hakikisha yanawekwa vizuri, umwagiliaji, palizi, madawa etc process zote ushuhudie, shirikisha locals majirani wenye uzoefu wakupe sifa ya udongo wako na hekari zako. Mambo ya kupiga simu, kutuma hela na kuagiza mtu akuangalizie ww upo busy na issue zingine, ninakuhakikishia utapigwa mimba. Ama la weka dogo au mtu una uhakika na yy ana machungu na huo mradi akusaidie kama upo busy sana.
Jambo jingine ninahisi hizi mvua zinazotokeaga from nowhere kipindi cha kuvuna vitunguu ni ndumba na uchawi sometimes, locals wanakuwaga na wivu design. Heard this stories na nimesoma humu. I have confirmed
Mkuu mashamba ya kukodi kwa hiki kilimo yanapatikana mikoa gani.kwa wepesi.?
Mkuu mimi niko tabora nataka kusia mbegu mwanzoni mwa mwezi wa 8 je nitakutana na soko zuri?MAENEO YA KUKODISHA
ILULA IRINGA- EKA MOJA TSH 150,000 HADI LAKI 3, PEMBENI YA MTO RUVU BEI TSH 100,000-250,000 KWA MSIMU, MOROGORO (DUMILA. DAKAWA,KILOSA ULAYA) EKA MOJA NI TSH 80,000-150,000 KWA MSIMU, IGAWA MBEYA HAPO EKA 1 NI TSH 300,000 HADI 400,000 KWA MSIMU WANALIMA SANAA VITUNGUU, NYANYA NA HOHO KIASI
Mkuu mimi niko tabora nataka kusia mbegu mwanzoni mwa mwezi wa 8 je nitakutana na soko zuri?
Na je, nitumie mbolea gan wakati wa kupanda na nirudie mbolea gan na kwa muda gan?
Na vipi kuhusu madawa ya wadudu?
Hongera sana mtoa mada na utaalamu kweli umebobea..Binafsi ni mnazi wa kulima kitunguu naishi Arusha ila nimeambiwa fursa hii IPO Ruaha mbuyuni iringa
POPOTE PENYE JOTO KUANZIA NYUZI 20-30 SENTIGRADE, UDONGO WA KICHANGA TIFUTIFU, AU TIFUTIFU FULL, UWE NA MAJI YA KUTOSHA , UNALIMA KITUNGUU VIZURI KABISA, MAENEO MENGI KITUNGUU KINAKUBARI, ARUSHA HUKO NGALE NA NYUKI, MOSHI KAHE, SAME, MWANGA, MOROGORO (DUMILA, MAGUBIKE, KILOSA), IRINGA-ILULA, RUAHA MBUYUNI, MBEYA-IGAWA, NJOMBE-MAKAMBAKO ETC
Wow! Hongera, wapi hapo?Sina utalamu sana na ardhi ya huko lakini ni mazao mazuri, japo kitunguu maji ningekushauri uje mkoani tupige kazi utafurahi....hila kwa ardhi za kisarawe sina hakina.
Duh....soko ndio huwa majanga. Mwenzio nililima katika kijiji cha Mambi Igurusi mwaka 2014. Niliuza kwa tsh. 30,000/ ilimiuma balaa.Jamani mm nimelima vitunguu mkoani mbeya katika kijiji cha igawa natarajia kuvuna jumatatu tarehe 18/7/2016 tatizo ni bei imeshuka mno. Gunia huku watu wananunua kwa shilingi elfu sitini tu (60) je, wapi nitapata soko zuri naombeni ushauri wana jamvi
Milioni moja?
Inategemea unalimia wapi?
Inategemea umwagiliaji kwa pampu au mifereji au mvua
Uzoefu wangu huku Kilosa huu:
Mbegu lita 7 kwa ekari @ 25,000/= jumla 175,000/=
Kuandaa kitalu 20,000/=
Kusia mbegu 10,000/=
kutunza kitalu 30,000/=
kukodi shamba 100,000/=
kufyeka shamba 48,000/=
kukatua udongo 64,000/=
kulainisha udongo 48,000/=
kutengeneza majaruba 25,000/=
kupandikiza 160,000/=
dawa ya kuua magugu 40,000/=
palizi mara mbili 100,000/=
Mbolea mifuko mitatu 210,000/=
Mtu wa kuweka mbolea mara mbili 10,000/=
madawa kuua wadudu na magonjwa 50,000/=
mpiga dawa wiki kumi 50,000/=
kung'oa 50,000/=
kukata vitunguu gunia mia 200,000/=
usafiri 100,000/=
chanja kukodi 100,0000
umwagiliaji petrol 2500 x lita 5 x wiki 10 = 125,000/=
mtu wa kumwagilia 5000 x wiki 10 = 50,000
JUMLA KUU = 1,855,000/=
Kwa wastani ni mil 2
Mkuu nina taka kuingia kwenye kilimo target yangu kubwa ni horticulture,sana ni kilimo cha mboga mboga ikiwemo vitunguu nyanya karoti na hoho wazo langu kuu ni kuanza na kitunguu mwakani nifanye deployment ya horticulture kwa kitunguu kwa eka moja.. nimesikia swala la mvua kunyesha na kuozesha vitunguu nataka nipate msaada wa kitaalamu pia na makadirio ya gharama za horticulture kwa hyo eka moja
kaka mi nipo interested na nipo moshi muda mwingi. tuwasiliane kama utaona inafaa.na mm nipo interested na hii kitu nipo moshi..........kama uneza taka partnership npo tayar
what is this?