Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Mimi na mwenzangu tushalima vitunguu mara moja tukafanikiwa kurudisha capital na faida juu, japo sio tulitegemea. Na tunajipanga tena. Hii kitu hii sio lelemama. Unapaswa kwenda benet nayo, kuanzia kusia, transplanting, majaruba hakikisha yanawekwa vizuri, umwagiliaji, palizi, madawa etc process zote ushuhudie, shirikisha locals majirani wenye uzoefu wakupe sifa ya udongo wako na hekari zako. Mambo ya kupiga simu, kutuma hela na kuagiza mtu akuangalizie ww upo busy na issue zingine, ninakuhakikishia utapigwa mimba. Ama la weka dogo au mtu una uhakika na yy ana machungu na huo mradi akusaidie kama upo busy sana.

Jambo jingine ninahisi hizi mvua zinazotokeaga from nowhere kipindi cha kuvuna vitunguu ni ndumba na uchawi sometimes, locals wanakuwaga na wivu design. Heard this stories na nimesoma humu. I have confirmed

Kaka nimependa maelezo yako, lakini hapo kwenye ndumba ndio sipati picha hilo jambo la kuleta mvua ni kweli? Na kama ni kweli mbona hiyo mvua wasilete kwenye mashamba yao wakati ukame pia unawapiga wao bao? Mimi nadhani ni mabadiliko ya tabia nchi tu. Naweza kuelimishwa zaidi.
 
MAENEO YA KUKODISHA

ILULA IRINGA- EKA MOJA TSH 150,000 HADI LAKI 3, PEMBENI YA MTO RUVU BEI TSH 100,000-250,000 KWA MSIMU, MOROGORO (DUMILA. DAKAWA,KILOSA ULAYA) EKA MOJA NI TSH 80,000-150,000 KWA MSIMU, IGAWA MBEYA HAPO EKA 1 NI TSH 300,000 HADI 400,000 KWA MSIMU WANALIMA SANAA VITUNGUU, NYANYA NA HOHO KIASI

Mkuu mashamba ya kukodi kwa hiki kilimo yanapatikana mikoa gani.kwa wepesi.?
 
MAENEO YA KUKODISHA

ILULA IRINGA- EKA MOJA TSH 150,000 HADI LAKI 3, PEMBENI YA MTO RUVU BEI TSH 100,000-250,000 KWA MSIMU, MOROGORO (DUMILA. DAKAWA,KILOSA ULAYA) EKA MOJA NI TSH 80,000-150,000 KWA MSIMU, IGAWA MBEYA HAPO EKA 1 NI TSH 300,000 HADI 400,000 KWA MSIMU WANALIMA SANAA VITUNGUU, NYANYA NA HOHO KIASI
Mkuu mimi niko tabora nataka kusia mbegu mwanzoni mwa mwezi wa 8 je nitakutana na soko zuri?

Na je, nitumie mbolea gan wakati wa kupanda na nirudie mbolea gan na kwa muda gan?
Na vipi kuhusu madawa ya wadudu?
 
Hongera sana mtoa mada na utaalamu kweli umebobea..Binafsi ni mnazi wa kulima kitunguu naishi Arusha ila nimeambiwa fursa hii IPO Ruaha mbuyuni iringa
 
KIONGOZI UNATAKA KUSIA MBEGU ZA ZAO GANI??

MBOLEA ZA KUPANDIA KWA MAZAO YANAYOISHA MUDA WA MAISHA YAKE NDANI YA MIEZI 6

DAP, NPK (10:20:20 AU 17:17:17), TSP, YARA MILLER WINNER, SAMADI NA MBOJI

ZA KUKUZIA NI SAMADI, UREA, AU CAN, YARA MILLER WINNER NPK ETC

BOOSTER
KUNA STARTER BOOSTER KAMA POLYFEED STARTER, EASY GROW, VIJIMAX ETC-HIZI HUPIGWA MICHE IKIWA MICHANGA ILI IKUE, NA WAKATI WA MAUA

KUNA FINISHER BOOSTER KAMA VILE POLYFEED FINISHER, POTPHOS, WUXAL MACROMIX, HIZI HUPIGWA WAKATI WA MATUNDA KUNENEPESHA MATUNDA

DAWA ZA WADUDU AMBAZO NI MULTIPURPOSE (CONTACT NA SYTEMIC) NI DUDUALL, BLAST, BUFFALO, DIMETHOATE, SELECRONE ETC


TAKE TIME PITIA UZI HUU,
Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi?? Karibu tushauriane

UNAKILA KITU HUMO (TENGA MUDA WA KUTOSHA UTAJIFUNZA MENGI SANA HUMO


Mkuu mimi niko tabora nataka kusia mbegu mwanzoni mwa mwezi wa 8 je nitakutana na soko zuri?

Na je, nitumie mbolea gan wakati wa kupanda na nirudie mbolea gan na kwa muda gan?
Na vipi kuhusu madawa ya wadudu?
 
POPOTE PENYE JOTO KUANZIA NYUZI 20-30 SENTIGRADE, UDONGO WA KICHANGA TIFUTIFU, AU TIFUTIFU FULL, UWE NA MAJI YA KUTOSHA , UNALIMA KITUNGUU VIZURI KABISA, MAENEO MENGI KITUNGUU KINAKUBARI, ARUSHA HUKO NGALE NA NYUKI, MOSHI KAHE, SAME, MWANGA, MOROGORO (DUMILA, MAGUBIKE, KILOSA), IRINGA-ILULA, RUAHA MBUYUNI, MBEYA-IGAWA, NJOMBE-MAKAMBAKO ETC

Hongera sana mtoa mada na utaalamu kweli umebobea..Binafsi ni mnazi wa kulima kitunguu naishi Arusha ila nimeambiwa fursa hii IPO Ruaha mbuyuni iringa
 
POPOTE PENYE JOTO KUANZIA NYUZI 20-30 SENTIGRADE, UDONGO WA KICHANGA TIFUTIFU, AU TIFUTIFU FULL, UWE NA MAJI YA KUTOSHA , UNALIMA KITUNGUU VIZURI KABISA, MAENEO MENGI KITUNGUU KINAKUBARI, ARUSHA HUKO NGALE NA NYUKI, MOSHI KAHE, SAME, MWANGA, MOROGORO (DUMILA, MAGUBIKE, KILOSA), IRINGA-ILULA, RUAHA MBUYUNI, MBEYA-IGAWA, NJOMBE-MAKAMBAKO ETC


NAONGELEA KITUNGUU MKUU
 
Sina utalamu sana na ardhi ya huko lakini ni mazao mazuri, japo kitunguu maji ningekushauri uje mkoani tupige kazi utafurahi....hila kwa ardhi za kisarawe sina hakina.
6688449c97277c8170e5fec482e2772b.jpg
Wow! Hongera, wapi hapo?
 
Jamani mm nimelima vitunguu mkoani mbeya katika kijiji cha igawa natarajia kuvuna jumatatu tarehe 18/7/2016 tatizo ni bei imeshuka mno. Gunia huku watu wananunua kwa shilingi elfu sitini tu (60) je, wapi nitapata soko zuri naombeni ushauri wana jamvi
Duh....soko ndio huwa majanga. Mwenzio nililima katika kijiji cha Mambi Igurusi mwaka 2014. Niliuza kwa tsh. 30,000/ ilimiuma balaa.
 
Wadau kwa mwenye ufahamu kuhusu ulimaji wa vitunguu maeneo ya bagamoyo kando ya ruvu haswa eneo la mtoni pale anijuze chochte..
1.mbegu sahihi
2.gharama za kukodi shmba
3.muda muafaka wa kulima
4.aina ya umwagiliaji unaotumika etc
 
Milioni moja?
Inategemea unalimia wapi?
Inategemea umwagiliaji kwa pampu au mifereji au mvua
Uzoefu wangu huku Kilosa huu:
Mbegu lita 7 kwa ekari @ 25,000/= jumla 175,000/=
Kuandaa kitalu 20,000/=
Kusia mbegu 10,000/=
kutunza kitalu 30,000/=
kukodi shamba 100,000/=
kufyeka shamba 48,000/=
kukatua udongo 64,000/=
kulainisha udongo 48,000/=
kutengeneza majaruba 25,000/=
kupandikiza 160,000/=
dawa ya kuua magugu 40,000/=
palizi mara mbili 100,000/=
Mbolea mifuko mitatu 210,000/=
Mtu wa kuweka mbolea mara mbili 10,000/=
madawa kuua wadudu na magonjwa 50,000/=
mpiga dawa wiki kumi 50,000/=
kung'oa 50,000/=
kukata vitunguu gunia mia 200,000/=
usafiri 100,000/=
chanja kukodi 100,0000
umwagiliaji petrol 2500 x lita 5 x wiki 10 = 125,000/=
mtu wa kumwagilia 5000 x wiki 10 = 50,000
JUMLA KUU = 1,855,000/=

Kwa wastani ni mil 2

Asante Sana Kwa taarifa hii muhimu
 
Mimi napenda kuwasisitiza mambo makuu matatu katika kilimo hichi kwasababu nimeshuhudia watu wana ingizwa Chaka na kupoteza mamilioni

1. Usianze kulima kabla hujapata ABC kamili za kilimo na changamoto zake. Tembelea watu ambao wana uzoefu Kwenye kitunguu. Jua Majira ya kukilima kitunguu, jua soko lilivyo na linavyo badilika, jua mbegu bora na mahitaji ya kitunguu n.k

2. Kama Ni muajiriwa chonde chonde achana na kilimo cha whasap na simu, yaani usikae ofisini ukawa unatuma tu hela shamba, weka ratiba ya Kwenda shamba at least twice a month ukaone maendeleo

3. Hakikisha hakikisha ndugu unapata mtu mwaminifu wa kusimamia shamba masaa yote. Yani ndio awe project manager wako ambaye kazi Yake Ni kusimamia shamba lako. Awe amesha lima kitunguu au anakijua kilimo

NB: Usiwaze faida kwasasa, achana na habari za kuuliza ekari moja inatoa gunia ngapi na gunia shilingi ngapi. Target yako kwasasa iwe kujifunza hivyo anza na ekari moja au chini ya hapo.
 
Mkuu nina taka kuingia kwenye kilimo target yangu kubwa ni horticulture,sana ni kilimo cha mboga mboga ikiwemo vitunguu nyanya karoti na hoho wazo langu kuu ni kuanza na kitunguu mwakani nifanye deployment ya horticulture kwa kitunguu kwa eka moja.. nimesikia swala la mvua kunyesha na kuozesha vitunguu nataka nipate msaada wa kitaalamu pia na makadirio ya gharama za horticulture kwa hyo eka moja

Matafute huyu mtu 0757 64 05 61
 
Wakuu, mimi nipo interest sana kwenye kujaribu hii kitu kwa mid scale, yaani acre 10 na kuendelea. Naombeni mwenye ujuzi wa juu anipe namba nizungumze nae.

Kwangu mimi masoko sioni kama tatizo. Naona tatizo ni unknown nyingi shambani.
 
Naomba kujua makadirio ya gharama za kulima vitunguu kwa Ekari moja...
images (2).jpg
 
Back
Top Bottom