Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Kwa dodoma ni mbegu zipi bora na vipi kuhusu upatikanaji wake
 
Brother bei ya kitunguu hubadirika kulingana msimu, mfano msimu wa mvua bei huwa nzuri zaidi na wakati wa kiangazi has a September to November ni kipindi ambacho kitunguu huwa na bei mbaya zaidi hufikia hata chini ya 40,000/= na premium price hupatikana mwezi march to may mfano Soko la Makambako mwezi April plastic yenye ujazo wa Lita 20 ilikuwa inauzwa 28,000 zidisha Mara 7
 
Naulizia bei ya vitunguu jamani. Mimi nimelimia Ruaha Mbuyuni, hapa bei haimlipi mkulima kwa sasa, gunia linauzwa shs 55,000 mpaka 60,000. Naambiwa Makambako ama Mbeya bei ni nzuri. Sijui Dar imekaaje, maomba msaada.
 
Naulizia bei ya vitunguu jamani. Mimi nimelimia Ruaha Mbuyuni, hapa bei haimlipi mkulima kwa sasa, gunia linauzwa shs 55,000 mpaka 60,000. Naambiwa Makambako ama Mbeya bei ni nzuri. Sijui Dar imekaaje, maomba msaada.
Mkuu mimi nililima Ruvu-Gange,nimeungua moto sana neti ya kilemba nimeuza kwa 23000 na kila neti inachukua debe nne.

Afu niliuziwaga mbegu fake vitunguu vyangu havikua vyekundu....so nilipata hasara sana
 
Wadau msaada wenu mimi nina nia ya kuanza kilimo..nimevutiwa na vitunguu wasiwasi wangu ni kuanza ndani ya kipindi hiki cha mwezi wa tisa ilhali wakulima wengi hulima mwei wa 5 - 8! Naomba muongoZo wenu wa maeneo na mbinu!!
 
Mimi pia nimelima kitunguu ndg yng,mbegu ndio kwanza ina wiki moja chini,nimesia tar 24/08,nafikiri ndio kipindi chake mkuu.
 
Mwenye kuwa na majibu yanayobainisha juu ya huu mda kulima kitunguu tunaomba aje atueleze. Ila kwa mimi hofu kubwa ni kukutwa na mvua kikaharibiwa na maji ya mvua maana ukisia mbegu saiv September kutoka ni kwenye January, February.

Pia kuhusu soko. Naona kitunguu kimelimwa kila kona ya nchi, hapo sasa cjui itakuwaje, yaweza kuja kuporomoka bei. But, by the way ni kujipa moyo na kufanyia kazi changamoto ambazo unauwezo wa kuzikabiri.
 
Umeshawahi kulima vitunguu ama unaongea kinadharia.

Normally kitunguu kinachukua siku 45 kutoka kusia kitaluni mpaka kuhamishia shambani then give it 90 days kukupa kiazi cha kuchuma. Jumla unaongelea around 135days from seeding to harvest.
 
nilipokuwa TZnimewah lima na kunitoa saana maeneo ya sanawali ya juuu. cha muhim cheza na soko pia tafta mbegu nzurikama RED CREOLE F1 japo ina gharama ila mbegu hii inazaa saana na pia inavumilia saana magonjwa na ukame. fanya ufanyavyo ila jitahid mwez wa tatu au wa nne uwe umepeleka kitunguu sokoni hapo utapiga hela mwana waneee balaa.

ila kinachangamoto saana aisee saana saana, ndio maana na recommend hyo mbegu kwa wale beginners. all the best.
kumbuka usi focus kweny nini utapata ila i tune akili yaako i focus kwenye changamoto za HYO KITU ni boraa kabala ya kuanza ukamtafta mtaalamu akakusaidia na akakueleza changamoto kwaanza kabla hajakueleza mafanikio.
 

Asante sana mkuu
 
Kama hilo eneo unalima lina vuli kumbuka kutengeneza matuta ya juu,kama hakuna vuli kiangazi hiki lazima uwe na hakika ya maji otherwise utaliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…