Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Mbona huku Mang'ola bado hawatulipi bei hiyo?

Duuuuuuuuuu! Mkuu nilikuwa huko mwezi wa 9, umenikumbusha mbali sana kamanda. Nna ndugu yangu anaishi hapo magereza mang'ola
 
kwanini isiunganishwe na hii iliyokwishaanza kuchangiwa tangu jana? Au huna haja ya kujua masoko yanapatikana wapi?
Mods naomba muunagsnishe hii na ile yangu.ili tuchangie mawazo kwa uzuri zaidi
 

At least leo nimesoma habari tofauti na zile nilizozoea kuzisoma. Hii ikipigiwa debe kubwa inaweza kuwasaidia wale ndugu zangu wanaolima vitunguu vijijini kuamka na kuchangamkia biashara. Tuwaache wanasiasa waendelee kuvuana magamba kadri wanavyoweza.
 

Iko Arusha - Karatu
Ekari inategemea eneo na msimu na ni kati ya 180,000 -250,000 hivi
Mavuno yanategemea matunzo, mbegu na kama mvua haitakuua, pia wadudu. Siwezi kutoa estimate hapa ila gunia 100 ni possible hata zaidi
Ekari moja ni "jaruba" 250 hivi, utahitaji angalua 2 mil. za matunzo.
Bei inategemea nyie wa mjini, demand and supply. Huwezi kuhifadhi kwa zaidi ya miezi 4 hivi.
Kupata gunia hata 1000 inategemea na hali ya msimu na hali ya soko, kwa gunia 250 utahitaji hadi siku tatu hivi.
 

Sharing is caring, karibu JF
 
 
Apa kuna akili sana, vitunguu mara nyungi vinakubali sehemu mbalimbali jaribu mahala popote ata matuta mawili ivi, nunua miche iliyokwisha oteshwa weka mboji nyingi. alafu shida yake ni utunzaji baada ya kuvuna.
 
Mwezi wa 9 mwaka huu nilikuwa pale Tarakea border ya Tz na kenya ambayo ndiyo border post kubwa kuliko zote Afrika mashariki kwa upande wa kenya, niliona takriban fuso nane zinapita kwenda kenya from Tz zikiwa zimepakia vitunguu aina ya 'red bombay' wamepack 15kg kwenye mesh bags

Niliuliza bei nikaambiwa na dereva kuwa hata wao hawamjui mteja

Hivi vitunguu vinastawi sana moshi maeneo ya chekereni na uwanda wa lower moshi, mandaka n.k, one acre yield 60 - 90 bags (appr. 100kg bag) almost up to two or three seasons

Vijana wengi sasa hivi wapo safi kwa kilimo hiki
 
Apa kuna akili sana, vitunguu mara nyungi vinakubali sehemu mbalimbali jaribu mahala popote ata matuta mawili ivi, nunua miche iliyokwisha oteshwa weka mboji nyingi. alafu shida yake ni utunzaji baada ya kuvuna.

Hata Dodoma vinakubali. Nimejribu kwa ajili ya kula sasa najipanga zaidi, changamoto ya Dodoma ni maji ya kutosha!
 
hongera sana mkuu, niliwahi tembelea dodoma maeneo ya mpwapwa kijiji kimoja kinaitwa kitati. Wanalima sana vitunguu na karanga.......tatizo lipo kwenye usafiri, kwani barabara ni mbovu sana. Pia kuna eneo lipo mpakani mwa dodoma na morogoro kilosa ...linaitwa lumuma, kitunguu kinastawi sana. Napanga kwenda huko mwezi december Mungu akinijaalia uzima.
Hata Dodoma vinakubali........................nimejribu kwa ajili ya kula sasa najipanga zaidi, changamoto ya Dodoma ni maji ya kutosha!
 
Wadau naombeni ushauri wa kulima kitunguu kwa yoyote mwenye uzoefu na hiki kilimo. Napenda nijue mahitaji na gharama kwa heka 1
 

Attachments

Wadau naombeni ushauri wa kulima kitunguu kwa yoyote mwenye uzoefu na hiki kilimo.napenda nijue mahitaji na gharama kwa heka 1

Pamoja na kupitia link hizo hapo juu, kuna mtu mmoja kama sijakosea anaitwa Njowepo, yuko humu jamvini, kuna wakati alikuwa analima pale mahenge wilayani Kilolo Iringa, Mpe-PM anaweza kukupa majibu.
 
Kinalipa. Heka Moja ni wastani wa 1 million mpaka unavuna. Kinahitaji maji na uangalizi wa karibu. Msimu nao ni wa kuzingatia ili uvune wa kati demand ni kubwa kama mwaka huu Jan/Feb.

binafsi nimepoteza million 6 katika kilimo cha kitunguu. huko Maeneo ya Marwa Same. Mto Ruvu unapoanzia. Wadudu wa ajabu walishambulia mara baada ya kuhamisha baada ya mbegu kukua. Nilisia hapo hapo shambani. mbegu ikaota vizuri sana. nilipopanda baada ya wiki 2 ikaharibika.
 
Natarajia desember tuwe na trip mbili za Iringa, ya mwisho itakuwa baada ya x-mass hivi,naamini hii utashiriki mkuu. Nitakuwa na vijana wa jf baadhi.

Mkuu hizi Trip au ushirikiano huu wa wana jf unakuaje ,nijuze mkuu maana ugeni wa jukwaa hili nadhani unachangia,nitashukuru pia (ngataabel@yahoo.com )
 
Mkuu hizi Trip au ushirikiano huu wa wana jf unakuaje ,nijuze mkuu maana ugeni wa jukwaa hili nadhani unachangia,nitashukuru pia (ngataabel@yahoo.com )

baadhi ya jf members tunafanya projects zetu pamoja lakini kila mtu anamiliki kivyake. Unakuta kwa mfano huko kwenu Iringa tunawekeza pamoja kila mtu kwa kadri ya uwezo alio nao. Lakini kuna mambo tunashirikiana ili kupunguza gharama fulani fulani.

Na sio kwenu tu, hata huku Pwani pia tunashirikiana ktk miradi mingine. Nakuletea mail.
 


Kanyagio brother. Nitwangie kwa namba yangu tafadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…