sweetdada
JF-Expert Member
- Feb 17, 2011
- 517
- 169
Sweetdada,
Lets share ideas, mimi nasikia vitunguu vinahitaji sana maji sasa hapo kwako upo karibu na kijito?
Ndio kuna bwawa lina maji mengi tu karibu na shamba. Je una interest ya kulima na wewe?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sweetdada,
Lets share ideas, mimi nasikia vitunguu vinahitaji sana maji sasa hapo kwako upo karibu na kijito?
Ndio kuna bwawa lina maji mengi tu karibu na shamba. Je una interest ya kulima na wewe?
Wakuu naombeni mnipatie uzoefu wenu katika kilimo cha vitunguu ruaha mbuyuni, jmosi natarajia kwenda ruaha kutafuta shamba eli ni jaribu hichi kilimo cha vitunguu, kwa yoyote aliyenauzoefu kwenye kilimo hichi naomba mchango wake.
Nasikitika umri ulikuwa mdogo sikuwa najua jf hapo nyuma!
Naomba kuuliza kwa maeneo ya songea(katikati ya njombe na songea) pana kubali hiki kilimo ukiwa na mashine yako ya umwagiliaji???
Nafurahi sana kuwa na wazee wa jf.
ningependa kushiriki pia namba yng 0717410406 nichek plsAsante ndugu yangu.
Kama uko DSM niambie ili siku nikifika dar nikutafute, leo niko nje ya dar. Unaweza kushiriki vikao vyetu bila taabu. Hakuna kiingilio na hatumfichi mtu kitu tunachofanya. Tunajadili namna ya kushiriki uchumi wa nchi yetu na sio kuwa watazamaji.
Jaman natka kushiri kikao namba yng 0717410406 mie sio mtu wa mtandao sana so nichek kwenye simu direct bip tu
Sikiliza Dangote hebu usikatishwe tamaa sijui umesha surrender tayari, ujue wengine ndiyo tunaona thread yako hapa si unajua ndiyo bado hatujasettle humu JF macho ya ugeni bado tunashangaa shangaa!
Ni hivi Dangote, humu humu jamvini kuna watu wameshasema kuwa kule Ruvu wanastawisha sana vitunguu!! Mbona naona ni ukanda huu huu wa pwani kwenye joto hili hili la Dar? Tatizo mimi sifahamu location ya Chamazi! Nikwambie ndugu yangu, watu tunapoongea hatuongei kitaalamu, tunasema sehemu fulani ina joto sana haifai kwa hiki au kile lakini hatusemi joto kiasi gani? Na ni majira gani? Utakubaliana nami kuwa kunamajira hata ukanda wa pwani huwa kuna baridi! Uongo? Sasa nikuleze kuwa hata Kilosa ambako kuna joto sana majira ya joto kitunguu swaumu kinalimwa sana lakini kinalimwa majira ya baridi kuanzia mwezi wa nne hadi mwezi wa nane watu wanaanza kuvuna safi kabisa!
Kwa hiyo ninachokushauri kwa vile nchi yetu haina utafiti wa kutosha uliofanyika kila eneo kujua kuwa linafaa kwa zao gani au halifai kwa zao gani na pia kwa kuwa unashauku sana kulima kitunguu na kwa kuwa shamba ni lako lima kitunguu swaumu hapo Chamazi majira ya baridi! Ukanda wa pwani wote ninaimani joto hushuka sana kuanzia mwezi wa nne pia! Tafuta aina mbili au tatu tofauti za vitunguu swaumu ili uweze kujua aina gani itakubaliana na mazingira hayo! Jambo moja ukae ukijua kuwa kila mahali penye zao linalostawi kuna mtu alijaribu kwanza likastawi ndiyo wengi wakafuata. Hakika nakuhakikishia utaweza kupata matokeo ya kushangaza na kukusisimua sana kwa sababu ninauhakika utafiti wa mboga mboga tanzania ni kama hakuna kabisa wamekaa wanategemea takwimu za kiujumla jumla tu kwamba Pwani kuna joto ilihali kuna majira Kisarawe huwa kunabaridi kama uko bara kabisa!! Kwa hili nakutia moyo na kama unamaswali mengine uliza tu, ila tafadhari matokeo yote utakayopata leta tumwagie hapa hapa kama wakubwa wetu Malila, El nino n.k. walivyotuonyesha njia!
Samahani kwa maelezo marefu namimi nami sinaga dogo mweeeee!!
Heshima sana kwa MALILA na EL Nino you are my Heros and the reason to be here!
Jaman nina shamba eneo la kitonga mbele kidogo ya chamanzi dar es salaam nauliza eneo hilo na hali ya hewa ya joto ya dar vitunguu swaum vinakubali? Wenye ujuzi na uzoefu naombeni msaada wenu wa mawazo.
asanteni kwa ushauri, natanguliza shukrani
Mkuu mimi nalima Kigonga maeneo hayo kupita kidogo kwa Mboma upande wa kushoto. Kimsingi vitunguu swaumu vinakubali lakini lazima kujua muda upi uweke dawa ipi na wadudu gani wanashambulia wakati gani. Mimi niliandaa water melon (matikiti maji) lakini mfanyakazi hakuya-treat vizuri yakawa yanapasuka kabla ya kukomaa! Ilinikatisha tamaa sana!
Watermelon kupoasuka kabla ya kukomaa, nadhani umelima kipindi cha mvua au maji yalikuwa mengi sana?