Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Mkuu itakuhitaji kuwa na mtaji kiasi gani ili uweze kulimaa heka 2
 
Mwaka huu kitunguu kimelimwa hasa nahisi kutakua na poromoko kubwa la bei hasa ikifika masika maana limelimwa isivo kawaida,me nalimia iringa ruaha mbuyuni
 
Inategemea na soko! Hio elfu 40 ni wapi? Sema hata hivo kipindi iki vitunguu hua vingi sokoni.. Target soko la dec..ingawa si kazi rahisi
Mwaha huu hata dec sidhani kma bei itakua nzuri kitunguu kimelimwa sana hasa huku iringa na bado watu wanaandaa vitalu kwa upande wa bei now n elfu 55 kwa hapa ruaha mbuyuni
 
Mwaka huu sidhani kama mambo yatakua the same lets wait n see maan huku limelimwa sana tofaut na miaka yote nna uzoefu wa miak 4 na hili zao sijawahi kutana na hali hii
 
Kulima kitunguu vitu muhimu kuangalia

Mda utakao vuna bei ikoje?

Hali ya hewa.

Kitunguu kikiaanza kukomaa hakihitaji maji(mvua) hakikisha eneo unalolima kwanzia mwezi 11 mwishoni nakuendelea sio msimu wa mvua.
 
humu naona mnazungumzia vitunguu, in hivi vitunguu maji au saumu.
nahitaji elimu na msaada wa kiushauri juu ya kilimo cha kitunguu saumu!!
 
Salaam wadau wa kilimo,
Naomba kuleta uzi huu nia hasa nikiomba ujuzi wa kilimo cha vitunguu,pilipili au nyanya chungu kwa mkoa wa morogoro au iringa.

Nahitaji kufanya kilimo hicho kwa kukodi shamba, Naomba mwenye uzoefu wa gharama, changamoto za kilimo cha mazao haya, masoko na muda hadi mavuno.

Nawashukuru kwa kila ushauri mzuri toka kwenu.

Ahsanteni sana.
 
ingefaa tumpate mtallaam wa mambo ya kilimo hapa hatusaidie kuhusu msimu wa kuanza kulima zao lolote na atuelezee namna ya kilimo kilivyo itakuwa vyema zaidi maan wengi hata mm nataka kulima na nimeshaanza kuilima

ruvu jkt nalima bamia je kwa kipindi hiki cha mweizi huu September inini kinatakiwa kulimwa zaidi
 
Umenene nami mbegu ya red creole naielewa sana ipo poa na nimeweka shamba
 
Kitunguu heka 2million ukisimamia mwenyewe karibu kwa kujifunza zaidi 0763370175
Hapo inategemea na mbegu gani atatumia ila kwa mbegu bora ni m3 kwa eka

Mbegu kuna red bombay elf 65 per kg na eka ni kg3 ya mbegu unapata from gunia 50 mpaka 70 kwa eka ,wachache wanafika gunia 80,meru super (improved op) kg1 ni tsh 98,000/= eka moja kg 2 na return kwa eka gunia 70 mpaka 100 ,neptune kg 1 tsh 370,000/= na eka moja ni kg1.5 return kwa eka ni gunia 100 mpaka 120 ,jambar kg 1 tsh laki 9 na kwa eka moja ni kg1 ya mbegu return ni gunia 200 mpaka 250 kwa eka .
Hivyo mbegu inaaffect mavuno na gharama ,kilimo bora ni cha hybrid seeds so kuanzia Meru super, neptune, jambar etc

Since mbolea na dawa ni zile zile bora mtu aongeze mavuno kwa mbegu bora
 
Niko Arusha nafahamu sana kwa huku ,msimu huu huwa kinacholipa ni vitunguu,hoho zinazotoka from December
 
Wakuu, mimi nipo interest sana kwenye kujaribu hii kitu kwa mid scale, yaani acre 10 na kuendelea. Naombeni mwenye ujuzi wa juu anipe namba nizungumze nae.

Kwangu mimi masoko sioni kama tatizo. Naona tatizo ni unknown nyingi shambani.
Acre 10 sio kitu kidogo ila ukikifanya vizuri kitakulipa sana ,kwa ushauri wangu lima kitunguu this season sababu unaposhana na wa Singida wale ndio wanalima kutegemea mvua hata elf 30 gunia kwake faida ,lima msimu huu uvune by February gunia huwa hadi laki 2,ila tafuta mtaalam wa kilimo huko unakolima akusimamie na uwe na vibarua u will see the results usifanye majaribio kwa eka kumi bali fanya production ya eka kumi ,kufanikiwa usilime kimazoea vyema ukimpata horticulturist kabisa kila mkoa wapo though huwa sio wengi ila ukiangalia upande wa ngo's na makampuni ya mboga huwa wapo wengi tu na wana experience ya mazao ya mboga
 
Mkuu horticulturist fafanua hiyo milioni tatu kwa kirefu kidogo...Tujue bei ya mbole na inahitajika kiasi gani kulima shamba nk
 
Mkuu horticulturist fafanua hiyo milioni tatu kwa kirefu kidogo...Tujue bei ya mbole na inahitajika kiasi gani kulima shamba nk
Ukitumia neptune mbegu kg 1.5 ni tsh 555,000/=
Kukodi shamba=
Kulima trecta=
Kuandaa kitalu sqm 500=
Kuandaa matuta ya kusia=
Kunyesha ya kwanza=
Kusia=
Kutafuta na kutandika matandizo=
kunyesha kitalu mara 20(mafuta,kibarua etc)=
Kitalu mbolea can kg 1,seedling starter 1=
Dawa ya ukungu 0.5kg na ya wadudu(thrips and red spider)=
Kibarua kitaluni=
Kupiga harrow shamba au kulima na ng'ombe=
Kunyesha ya kwanza na kuandaa matuta=
Kusia shamb eka vibarua=
Mbolea dap kg90 ya eka=
Kunyesha shamba mara 2 kwa wiki kwa mwezi mmoja kisha mara moja kwa mwezi kwa miez 3=
Palizi mbili =
Mbolea shambani urea/can kg 90,yara winner kg 90=
Dawa ukungu kg 1(ivory 72/rido/ebony 72 etc,blue copper),wadudu thrips,red spider,caterpillar(evisect,dynamec,belt)=
Kibarua kupiga dawa=
Kuvuna vibarua=


Hizo general gharama jaza amount kwa uliko uone unapata kiasi gani ,hapo ya kwako au msimamizi nnje ya budget
 
ah
Ahsante mbegu yenye kutoa mazao yanayokubarika sokoni la ndani na la nje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…