Naomba kujuzwa gharama za kilimo cha vitunguu kwa heka moja wadau, kwa Iringa na Kilimanjaro
Nawasilisha
Kwa kilimanjaro.
Kwanza mbegu kwa eka utatakiwa kusia kilo tatu mpaka nne. Ukinunua mbegu dukani hiyo ni 400,000
Kuandaa kitalu, kusia na kutunza mbegu kwa angalau mwezi mmoja na nusu lazima uwe na angalau 300,000
Kupandikiza ekari moja yenye majaruba yasiyopungua 330= 330,000
Utatakiwa ukishapandikiza uwe na mifuko angalau 12 ya mbolea kila mwezi utatia mbolea (yaani mifuko minne kwa eka) 45,000x12.
Utatakiwa kupiga dawa kila wiki ya kuua wadudu, buster, ya kuondoa baridi etc..dawa pekee itakugharimu si chini ya 80,000 kwa ekari moja kila wiki. Utatakliwa either kupiga dawa ya kuua mbegu za magugu yasiote ambayo ni tsh 17,000-27/ lita kwa ekar unaweza kuhitaji lita mbili. au kungolea majani angalau mara nne tangu kupandikiza mpaka kuvuna.
Kwa eka kila wiki utahitaji kumwagilia. Kwa ekari moja angalau uwe na lita 30 za dizeli/petroli kama pumb unayo.
NB: Omba Mungu utakapovuna Mang'ora au Ngage usiwe msimu wa kuvuna vitunguu maana utapata pressure. wengi wamepata hasara kubwa na wengine wamepoteza maisha. Bei kwa sasa kwa gunia la vitunguu haizidi elfu 60,000. Mimi binafsi nimelima na nimepata hasara isiyo kifani.
Kwa ekar kuanzia kusia mpaka kuvuna angalau uwe na tsh 3mil - 4mil. Lakini usitengee kuwa utavuna upate faida kama story zilivyo. Kama unapesa hivyo nakushauri uiwekeze kwa mambo mengine. Mzunguko wa pesa kwa sasa hakuna. Kitunguu hakilipi kwa sababu kinalimwa kila mahali Tanzania kwa sasa. Weka pesa zako hata fixed deposit.
Nazungumza kutokana na uzoefu. Nitumia zaidi ya mil13 kulima. Nilipovuna nikauza kila gunia kwa 40,000 nikapata hasara zaidi ya milion 10. Usisikie story. The truth is terrifying. Na usije ukachukua mkopo ukitegemea kilimo cha kitunguu kitakulipa. Kabla benki hawajakufikia utakuwa umeshakufa kwa pressure. Nenda ngage, kileo, chekereni, mawala, na sehemu zingine za mkoa wa kilimanjaro utapata story za watu waliokufa kwa pressure mwaka huu kutokana na vitunguu kushuka bei na kutofikia hata gharama za uzalishaji.
unaweza kuja inbox kwa maelezo zaidi. lakini kwa sasa kilimo cha vitunguu is not ideal