Habari zenu magwiji wa kilimo!
Wakuu mwaka jana {2020} nililima ufuta ekari 12 Katika wilaya ya Handeni mkoa wa Tanga, kwa bahati mbaya mvua zilizidi sana kuliko kawaida na kufanya ufuta kuwa mrefu sana, hivyo haukuweza kuzaa vizuri nikaambulia gunia moja moja kwa kila ekari sawa na gunia 13 za kilo miamoja kwa kila gunia moja.
Kwakua sina kawaida ya kukata tamaa licha ya kupata hasara, nimeamua kubadili zao na kulima vitunguu swaumu mkoa wa Iringa nimelima eneo lenye ukubwa wa ekari mbili na nusu, niliweza kukodi shamba, kuandaa shamba na kupanda kupitia kusoma nyuzi za wadau mbalimbali JamiiForums, nashukuru vitunguu vimeota vizuri sana na vina hali nzuri sana vina mwezi sasa tangu vimeota na vinakua kwa speed ya 4G.
Naishukuru JamiiForums na wadau wake kwa kuwa mwanga bora kwa jamii, ila kwa sasa nimeamua kumshirikisha Bwana shamba ili niweze kupata mavuno mazuri. Changamoto niliyo nayo ni kuhusu soko bado sijui.
Nitaleta mrejesho baada ya mavuno.