Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Oky, thanks very much Indeed!!
 
Habari Wana jamii
Nina uhitaji wa Miche ya vitunguu maji kwa ajili ya kuotesha shamba la ekari 2. Miche ikiwa Arusha itakuwa vizuri zaidi
 
Mkuu ulifikia lengo la kuteka soko? Maana bei ya kitunguu masokon haishikiki kwa sasa
 
Kipatimu ipo mkoa gani?
 
Ruaha Mbuyuni.
Nililima mang'ola kijiji cha kisiriri mwaka 2010 mzee mmoja akaniambia mwanangu umetoka chuo huku hatulimagi kwa kufuata elimu njoo nyumbani nikupe dawa uwekee uzio shamba lako na kwa vile shamba lako liko njiani watu wenye macho mabaya watahamisha mazao hutopata kitu, basi nikamshirikisha jamaa yangu tuliyekua tunafanya naye hiyo project akaniambia nimesomea kilimo Mimi ni mtaalamu hapo tuzingatie madawa, mbolea maji hachana na mambo ya kishirikina basi mzee nikamtolea nje akaniambia hili shamba mkilikinga mtatoa scania mbili na nusu ila mkipuuza hamtopata kitu, ebwana we kuja kuvuna tulipata gunia kumi, next year nikasema sikubali nikaenda kwa mzee mmoja milimani huko akanipa dawa nililima mahindi sio vitunguu manake kule ilikua ukikodisha shamba la kulima vitunguu unapovuna unaweka mahindi, nilfuata vigezo na masharti aisee alikuja jamaa na fuso nikamuuzia mahindi mabichi ekari sits, nilivyokunja pesa nilisepa nimevaa pensi na vesti niliacha begi na kila kitu, manake kule walikua na msemo kua mgeni hata aje na mil 500 tutamfirisi hadi akose nauli ya kurudi alikotoka so nilisepa kama nipo around vile sikubeba chochote zaidi ya mapene, mang'ola wale wambulu, mang'ati na wanyiramba Wa kitongoji cha kisiriri niliwavulia kofia kwa uchawi, na historian ya hicho kitongoji cha kisirri ni kijiji kipo iramba huko so wale wachawi waliofukuzwa iramba ndo wakaja kukaa hapo mang'ola na kuliita hill eneo kisiriri.
 
Kilimo bila uchawi unacheza
 
Hii mada ni njema sana, kama kuna mtu ana taarifa ya kilimo cha vitunguu Dodoma, Wilaya ya Mpwapwa akoje inbox tuyajenge, nimesikia kuna pesa hapo.
 
Hii mada ni njema sana, kama kuna mtu ana taarifa ya kilimo cha vitunguu Dodoma, Wilaya ya Mpwapwa akoje inbox tuyajenge, nimesikia kuna pesa hapo.
mpwawa wanalima vitunguu? Dawa ni kwenda tu mzee. Taarifa za mtandaoni accuracy yake mara nyingi si nzuri sana.
 
Mimi nahitaji Msada wa kuhusu kilimo cha kitunguu swaumu Masada please
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…