Naona mwaka huu umegeuka ghafla kuwa mbaya Kwa wakulima wengi wa vitunguu. Huwezi kuamaini mtu anakuja shambani anataka anunue lumbesa ya madebe 8 Kwa elfu 40 ili hali unaona sokoni debe moja ni Tshs. 20,000 Kwa uchache. Hivyo anapata 160,000 Kwa gunia ukiondoa gharama zake za usafiri, magunia upakiaji na upakuaji anapiga si chini ya laki Kwa gunia kama faida, mbaya sana hii. Vya kwangu nauza rejareja sasa na naanza kutafuta wenye vigenge niwapelekee, hii najua itanitoa tu. Ila kiukweli huko nilikolimia sitakaa nilime vitunguu huko tena. Gharama kubwa sana na mavuno ni kidogo. Labda naweza kujaribu kwingineko kama Iringa au Mbeya.