Kiongozi niko salama, siyo mwenyeji sana na kibaha, ila jambo la msingi ni kujua kwamba mazao hayo yote yanahitaji udongo kichanga, au tifutifu au kichanga tifutifu, yaani udongo ulio loose, uwe unapitisha maji kwa haraka. Udongo ulio loose husaidia ile build ( tunguu) kutanuta na kukua. Kingine cha kujua ni kuwa kitunguu swaumu hakina mbegu za madukani hivyo utahitaji kununua toka masokoni. Mazao hayo yoote yanachukua wastani wa miezi mitano tangu kupanda mpaka kuvuna. Sasa ni muhimu kupiga hesabu zako vizuri kujua kwa kibaha masika huanza lini? Lengo hasa ni kujipanga uvivune kabla ya masika kuanza! Vikikutwa na mvua shambani vitaoza!!