Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Milioni moja?
Inategemea unalimia wapi?
Inategemea umwagiliaji kwa pampu au mifereji au mvua
Uzoefu wangu huku Kilosa huu:
Mbegu lita 7 kwa ekari @ 25,000/= jumla 175,000/=
Kuandaa kitalu 20,000/=
Kusia mbegu 10,000/=
kutunza kitalu 30,000/=
kukodi shamba 100,000/=
kufyeka shamba 48,000/=
kukatua udongo 64,000/=
kulainisha udongo 48,000/=
kutengeneza majaruba 25,000/=
kupandikiza 160,000/=
dawa ya kuua magugu 40,000/=
palizi mara mbili 100,000/=
Mbolea mifuko mitatu 210,000/=
Mtu wa kuweka mbolea mara mbili 10,000/=
madawa kuua wadudu na magonjwa 50,000/=
mpiga dawa wiki kumi 50,000/=
kung'oa 50,000/=
kukata vitunguu gunia mia 200,000/=
usafiri 100,000/=
chanja kukodi 100,0000
umwagiliaji petrol 2500 x lita 5 x wiki 10 = 125,000/=
mtu wa kumwagilia 5000 x wiki 10 = 50,000
JUMLA KUU = 1,855,000/=

Kwa wastani ni mil 2
Na hapo unaweza kupata gunia ngapi?
 
Upepo wa Pesa
ASANTE MKUU

Kwa mujibu wa ndugu
Lucky01
alipambana na magonjwa ya rust (Kutu ya majani/Fangasi ), kwenye bursting hapo sijampata vizuri kama anamaanisha vitunguu kupasuka (pacha) hiyo si fangasi bali ni upungufu wa lishe ya Calcium (ALipaswa ahakikishe pale kilipoanza kufunga mbolea za Calcium kama CAN/Yara Nitrabor hazikosi) na huku juu akiendelea kusparay booster hasa zenye Sulphur (S) KWA WINGI ili kuongeza ile Aroma (Harufu)

SULUHU. Kwa matatizo ya kutu ni vyema kufanya yafutayo ili kujikinga na hizo shida

1.Epuka kumwagia maji jioni, yakatuama na yaka lala shambani, baadhi ya wakulima hufanya hivi. Hii huleta umande mwingi wakati wa usiku, na umande/unyevu ni mazingira rafiki ya fangasi kumea, hivyo mwagia mapema kama ni asubuhi mwagia kuanzia hata sa 12 hadi sa 5 hivi inatosha, kama ni jioni anza mapema ili kufika sa 12 jioni uwe umemaliza maji yasituame

2. Kwa upande wa dawa za kujikinga na ukungu, ni dawa zooote zenye viambata vifuatavyo (Propneb-Mfano ipo inayoitwa Milraz), Copper (Mfano Bluue Copper/Nordox/Fungurani), Mancozeb (Mfano Farmazebo), Cholothalonil (Mfano-Damka/Banko/Odeonetc) , Hexaconazole (Mfano Xantho); Kipimo ni mls /gram 30-60 kwa maji lita 15, kama kuna ukungu mwingi piga kila baada ya siku 7

3. Za kutibu ukungu. Ni Amista extra (Kiambata-Azoxtrobin +Hexaconazole), Multi power 78 PLus WP (Kiambata Myocin), Agrifos 400 (Kiambata PAS-Phosporic Acid Salt-Di-Mo Potassium Phosphate). Nativo, etc


====================================


Mkuu kilimomaarifa.tajiri, niaje kiongozi.

Ebana naomba utalaamu/uzoefu wako katika hili:

Ili kupata mavuno MENGI yenye ubora (katika kilimo chochote kile), je mkulima atumie mbolea ipi.... ya kienyeji (samadi) ama ya kiwandani (DAP, CAN, NPK, n.k) ama achanganye/atumie zote awamu kwa awamu?

Huku mashambani kumekuwa na mkanganyiko mkubwa. Baadhi ya wakulima wanasema kuwa mbolea ya kienyeji ndo inafaa kuanzia kupanda mpk mwisho mavuno, ila ya kiwandani inaharibu rutuba ya asili (inaua ardhi). Wengine wanasema ya kiwandani ndo inafaa zaidi kuanzia kupanda mpk mwisho kuvuna, inatoa best results (mavuno mengi sana). Wengine pia wanasema ukizitumia zote (I.e ya kienyeji na ya kiwandani, awamu kwa awamu) ndo utapata best results ktk mavuno.

Ni mkanganyiko mkubwa. Hebu wataalamu wa mambo haya tupeni ushauri wenu katika hili.

-Kaveli-
 
Wenzako tunapiga hela ww endelea kuwa na mashaka ulizia kilo moja sahiv sh ngapi sokoni
Sasa izo milion saba ni pesa za kujisifia na wewe. Nikiigawa kwa miezi mitano ni kama vile ulikuwa unafanyia m1 kwa mwezi. Sasa unajisifu kupata m1 kwa mwezi. Au ulikuwa hujashika pesa ya namna iyo.

Wewe kwanza muongo tu. Upo hapa unajikanyaga kanyaga tu. Mara nilikodi shamba ka m1, mara nililipa msimamizi laki tano jumla 1.5 ndyo cost. Huoni hata aibu. Cost za mbegu, umwagiliaji, uandaaji wa shamba, mbolea, vibarua, ulinzi etc umemuachia nani.

Nyie ndyo tunawaitaga wakulima wa internet.
 
Sasa izo milion saba ni pesa za kujisifia na wewe. Nikiigawa kwa miezi mitano ni kama vile ulikuwa unafanyia m1 kwa mwezi. Sasa unajisifu kupata m1 kwa mwezi. Au ulikuwa hujashika pesa ya namna iyo.

Wewe kwanza muongo tu. Upo hapa unajikanyaga kanyaga tu. Mara nilikodi shamba ka m1, mara nililipa msimamizi laki tano jumla 1.5 ndyo cost. Huoni hata aibu. Cost za mbegu, umwagiliaji, uandaaji wa shamba, mbolea, vibarua, ulinzi etc umemuachia nani.

Nyie ndyo tunawaitaga wakulima wa internet.
Ww Kama ni mkulima si ulete data zako
 
Hapo inategemea na mbegu gani atatumia ila kwa mbegu bora ni m3 kwa eka
Mbegu kuna red bombay elf 65 per kg na eka ni kg3 ya mbegu unapata from gunia 50 mpaka 70 kwa eka ,wachache wanafika gunia 80,meru super (improved op) kg1 ni tsh 98,000/= eka moja kg 2 na return kwa eka gunia 70 mpaka 100 ,neptune kg 1 tsh 370,000/= na eka moja ni kg1.5 return kwa eka ni gunia 100 mpaka 120 ,jambar kg 1 tsh laki 9 na kwa eka moja ni kg1 ya mbegu return ni gunia 200 mpaka 250 kwa eka .
Hivyo mbegu inaaffect mavuno na gharama ,kilimo bora ni cha hybrid seeds so kuanzia Meru super,neptune,jambar etc
Since mbolea na dawa ni zile zile bora mtu aongeze mavuno kwa mbegu bora

ipi namna bora ya kitaalamu kuzuia kitunguu kisiharibiwe na mvua??
 
Kitunguu chenye bei nzuri kinaanzia december to april, wakati huo wanaotamba na mzigo sokoni ni wale wenye uwezo wa kumwagilia tu. Lakini ukilogwa ukalima wakati wa masika may to september sokoni mzigo huwa mwingi kupita kiasi na bei yake hudondoka sana. Soko la kuanzia december to april wateja wanafuata mzigo wenyewe shambani tena kwa bei ya juu. Ukiwa na mzigo njoo tu hata hapa jukwaani uache namba ya simu uone huo usumbufu wa madalali.
Mkuu naomba number yako ya simu unaonekana una utaalamu wa kulima kitunguu,na mm nataka kuanza kulima mwaka huu
 
Jamani bei ya kitunguu maji ipo chini huku Iringa hadi majanga. Gunia Tsh 35000/= asalale!
 
Jamani bei ya kitunguu maji ipo chini huku Iringa hadi majanga. Gunia Tsh 35000/= asalale!
Shambani au sokoni?

Mwaka wetu huu,na wale waliolima hyprid akina neptune hasa hasa wenye degree wataisoma..
 
Habari wana jf, naombasaaada kwa MTU ambaye ameshawahi kulima vitunguu maeneo ya njiapanda au kileo kama unaenda mwanga. Kuanzia gharama za kukodi shamba palizi mbegu na kiss cha mavuno...asante
 
Habari zenu wanajukwaa!!!!

Sticking to the point:

Nimejaribu ku search na ku google kuhusiana na hiki kilimo cha vitunguu saumu nimepata kuhusu yafuatayo:
1. Udongo unaofaa kukilima
2. Maeneo kinapolimwa
3. Hali ya hewa inayofaa

SIJAPATA YAFUATAYO:
A. Ain a za vitunguu saumu
B. Mbolea zinazotumika kukilima na jinsi ya kuzitumia kutegemea umri wa kitunguu hicho
C. Madawa yanayotumika na kwa muda gani.
D. Utofauti wake na vitunguu maji kwenye taratibu za kukilima
E. Aina za mbegu, gharama zake na zinakopatikana
F. Kiasi gani cha mbegu kwa ekari moja
G. Taratibu za nyongeza kukihusu katika mchakato wa kukitunza.

NAWAKARIBISHA WABOBEZI WOTE KATIKA KUTUDADAVULIA kinagaubaga ya hii kitu.
Maofisa kilimo wote tusaidieni hapa tujikwamue kwa maana no way out AJIRA HAKUNA. Inabidi tujiajiri katika kilimo.
Yeyote mwenye utaalamu wa kilimo cha vitunguu Saumu atusaidie.

SHUKRANI NAWEKA MBELE!!!
KARIBUNI.
 
Wakuu mwezi nne nahitaji kuanza heka 1 ya kulima kitunguu maji maeneo ya Moro, naomba utaalamu wenu kuhusu mbegu bora ni ipi? Dawa kwa ajili ya kinga na soko la uhakika napataje. Au ushauri wowote utaonifaa kwa sabab ndio mara yangu ya kwanza kulima.
Asanteni.
 
Habari ndugu zangu,

Naomba mwenye uzoefu na kilimo cha vitungu maji tusaidiane na nia ya kulima mwaka huu zao hilo 0717 209059 pia whatsap ipo hiyo namba.

Natanguliza shukrani kwa mtakaojitolea.
 
Back
Top Bottom