Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Mm ni mtaalamu wa kilimo cha nyanya, vitunguu sina uzoefu navyo

Ulikuwa unataka ushauri gani mkuu?
 
Habari zenu wanajanvi, e bhana nahitaji msaada kwa raia wanaojihusisha na kilimo cha vitunguu maji, mim ni mgeni yaani ndio nimeanza hiki kilimo cha vitunguu. Nimeanza na ekari moja ili iwe kama shamba darasa, nimeshapanda mbegu na tayari zimeshaanza kuota.

Kwa wenye uelewa naomba muongozo wa namna ya kuzitunza hizo mbegu kabla hazijafikia mda wa kupeleka shamba maana ninavyojuwa inatakiwa nizisimamie vizuri ili niwe na mbegu bora, nanitakapohamishia shambani ziwe katika hali nzuri.

Natanguliza sana shukran zangu za dhati kwa raia wote watakaonipa darasa.
 
Hata mimi Shida yangu kama yako. Tuwasubiri waje. Msaada jamani unahitajika huku
 
Jaribu kusearch mkuu kuna discussion nyng zilishawah kufanyika kuhus hilo somo ukiptia hzo pamoja na mawazo ya wadau wengne humu yatasaidia saana
 
Habari wakuu, natumaini mnaendelea vizuri na majukumu ya kila siku.

Nataka nilime kitunguu swaumu lakini sijajua ni maeneo gani zao hili linakubali, naomba ambaye anafanya kilimo hiki anisaidie.

Natanguliza shukrani.
 
UDONGO
Vitunguu twaumu vinahimili aina nyingi za udongo, ila vinastawi zaidi katika udongo usiotuamisha maji kabisa na wenye mbolea asili, kama mbolea si ya kutosha kwenye udongo, tumia samadi iliyokwisha oza vizuri usitoe samadi bandani na kuipeleka shambani moja kwa moja kwenye shamba la vitunguu thwaumu, labda kama utaliacha shamba bila kulimwa kwa zaidi ya miezi 6, pia unaweza kutumia mbolea za viwandani kama ammonium nitrate, ammonium sulphate, urea n.k wakati wa kupanda na kila baada ya wiki 4 – 6 mara mbili zaidi

UPANDAJI
Kipindi kizuri kwa upandaji ni kipindi ambacho hakuna joto hasa miezi ya May mpaka August kwa Tanzania, Unachukua kitunguu twaumu na kutenganisha vitunguu kimoja kimoja (bulbs) na kuchagua vile vikubwa maana hivi ndivyo vitakavyo kupa mazao mengi na bora, nafasi kati ya kitunguu na kitunguu ni sentimeta 10 na kati ya mistari ni sentimeta 30. Baada ya kupanda pandishia udongo na uukandamize kuhakikisha kwamba kimekaa vizuri na hakiwezi kuathiriwa na mvua au maji wakati wa kumwagilia ili kisikae upande au kungolewa kabisa. Uotaji mzuri hutegemea pia namna vitunguu thwaumu vilivyo hifadhiwa kabla ya kupandwa, kama vilihifadhiwa sehemu zenye joto na hewa finyu uotaji wake utakuwa duni na dhaifu.


UMWAGILIAJI
Kama kuna upungufu wa mvua au ni kipindi cha kiangazi basi ni vizuri ukamwagilia shamba lako, wakati mzuri wa kumwagilia vitunguu twaumu ni asubuhi na sio jioni au mchana, hii inasaidia vitunguu twaumu kujijengea uwezo wa kupambana na magonjwa, baada ya mizi miwili unaweza kupunguza umwagiliajai huku ukiangalia kwa kuchimba kidogo kama vitunguu twaumu vimezaliana vya kutosha na kuanza kukomaa, ukiona vimekomaa acha kabisa kumwagilia ili visioze

UANGALIZI
Aina nyingi za vitunguu twaumu vitakuwa kama vinatoa mbegu kwenye mmea (angalia picha chini), ingawa kuna nadharia nyingi lakini inashauriwa kukata hizi mbegu chini kabisa kwa kisu kikali na kisafi, usikate mapema mara baada ya kutokeza bali subiri mpaka mmea unapoanza kama kujikunja ndipo ukate, kwa wale wanaoacha mbegu hizi ukiamua kuzipanda kwa msimu wa kwanza zitazaa kitunguu kimoja tu cha duara lakini chenyewe ukikipanda tena kwenye mzunguko wa pili kitazaa vitunguu vingi kama kawaida



Ungoleaji wa magugu na majani ni muhimu muda wote ili kuondoa kugombea rutuba, hewa na maji shambani, kwa wenye mashamba makubwa wanaweza kutumia dawa za kemikali kama ROUNDUP na nyinginezo ili kudhibiti magugu, ingawa mimi sishauri hivyo.

MAGONJWA
Magonjwa kama botrytis (kuoza shingo) blue mould na fusarium (kuoza kwa vitunguu) husababisha hasara kubwa kama hayatadhibitiwa kwa kutumia viuatilifu mara unapoona dalili, pia magonjwa kama white rot huchukua zaidi ya miaka 20 kuondoka kama yatavamia shamba lako, inashauriwa kufanya mabadiliko ya zao kila baada ya miaka mitano kwa kupanda mazao mengine yasiyo jamii moja kama vitunguu maji, unaweza kupanda maharage, mahindi, karoti na kabichi katika mzunguko huo. Pia magonjwa kamakutu ya majani husababisha na unyevu mwingi hasa kama mimea itakuwa kwenye udongo unaotuamisha maji au mimea kumwagiliwa jioni au usiku, kumbuka kumwagilia asubuhi tu Ili kudhibiti ugonjwa huu wa kutu mimea ingolewe na ichomwe au utumie viuatilifu vya kuulia fangasi wa mimea. source mitiki blog
 
asanten sana kwa mnaojitolea kutupa uzoefu wenu ktk kilimo cha kitunguu mwaka huu nakima mwez wa2 tr 15 nasia mbegu nipo simuyu (mkoa mpya kutoka shinyanga) vp huo muda ila nimepanga kutumia.mbegu ya kawaida toka singida kitunguu chekundu nimeshapata eneo nizur kwa maneno ya mzoefu wa kitunguu ni aridhi nyeus unapasuka kuruhusu hewa na haiitaj maj meng sana yan inatunza maj naomba kuwasilisha nimejieleza ili kukosolewa mapema kabla cjaanza kama kunakitu sijakifanyia sahh hapo nitafurai nikisahishwa na wazoef hum au watalam pia namba yangu ni 0717209059 mapokea ushaur zaid hat whatsp nipo
 
Mkuu sheria namba moja ya kilimo ni tafuta soko ndio ulime hiyo mosi ,jingine tumia mbegu bora ndio utaona faida hizo mbegu za kupimiwa kwa ndoo hamna kitu ndg na ni kwa mazao yote ,tumia hybrid utaleta mrejesho mfano neptune nusu kilo mbegu ni 185,000/= eka moaja inahitaj kg1.5-2 ila eka moja ukiitunza hovyo gunia 80 ukiitunza vyema gunia 120,hapo hata ukiuza kwa bei ya elfu 80 gunia unafaida hizi mbegu za kawaida zikipata stress tu kwanza zinaacha kubeba kitunguu zinatoa maua ,kingine soma alama za nyakati ili uwin soko mkuuu
Mkuu nakukubali nilitembelea page yenu aisee mko vyema sana kwenye idara zenu.
Mungu awasimamie siku moja tukijaliwa tutafanya kazi pamoja.
 
Back
Top Bottom