Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Haswa vinapendwa vitunguu vyekundu so meru super,neptune,jambar ziko poa ,hata red bombay ina vitunguu vyekundu sema tatizo ni vinatoa mabomba (boltingl sana tatizo ambalo kwenye improved na hybrid hakuna so kila mbegu inakua kitunguu
i prefer hiyo Neptune japo ni ghali ila kizuri huwa na gharama, kama naweza nunua smartphone hata hizo mbegu ni muhimu kununua yenye quality ambayo hutajuta kuitumia.
 
Jaman ndo napandikiza kitunguu hapa nadhan naweza toa mzigo May!!!
 
Kitunguu kimekuwa cha kisenge mno this time, nililima msimu wa mwezi wa 9 mpaka mwezi huu nimevuna sokoni hamna bei. Naskia harufu ya loss tu bora ningefungua car wash tu!
 
wadau najiandaa kusia mbegu mwez2 tr15 shamba nitapeleka mwez wa4 mavuno wa7 wataalam hapo vp nipe simiyu (MKOA MPYA JIRAN NA SHINYANGA NA MWANZA ) kwa wale wagen wa mikoa midogo. wataalam vp hapo taming ya soko!?
 
Milioni moja?
Inategemea unalimia wapi?
Inategemea umwagiliaji kwa pampu au mifereji au mvua
Uzoefu wangu huku Kilosa huu:
Mbegu lita 7 kwa ekari @ 25,000/= jumla 175,000/=
Kuandaa kitalu 20,000/=
Kusia mbegu 10,000/=
kutunza kitalu 30,000/=
kukodi shamba 100,000/=
kufyeka shamba 48,000/=
kukatua udongo 64,000/=
kulainisha udongo 48,000/=
kutengeneza majaruba 25,000/=
kupandikiza 160,000/=
dawa ya kuua magugu 40,000/=
palizi mara mbili 100,000/=
Mbolea mifuko mitatu 210,000/=
Mtu wa kuweka mbolea mara mbili 10,000/=
madawa kuua wadudu na magonjwa 50,000/=
mpiga dawa wiki kumi 50,000/=
kung'oa 50,000/=
kukata vitunguu gunia mia 200,000/=
usafiri 100,000/=
chanja kukodi 100,0000
umwagiliaji petrol 2500 x lita 5 x wiki 10 = 125,000/=
mtu wa kumwagilia 5000 x wiki 10 = 50,000
JUMLA KUU = 1,855,000/=

Kwa wastani ni mil 2
 
nataka lima heka moja nipo singida......samahani naomba kujuzwa nasikia kitunguu kikinyeshewa kimeharibika
 
Jamani habarini. Huu mjadala nimeupenda sana unaonekana kua mzur sana kwangu naomba uendelee haswa kwa kujibiwa ni mwez gani ambao nikivuna nakuta gunia liko juu?
 
Back
Top Bottom