Kaveli
KARIBU SANA
Sasa mkuu, naomba pia unifahamishe kuhusu MADAWA & SUMU za kupulizia ili kukinga na kuzuia magonjwa mbali mbali, i.e kuanzia mmea unapoota mpaka kuanza mavuno.
1. MADAWA au/na SUMU sahihi kwa zao la Bamia ni yepi? na utaratibu wa kupulizia upoje, yaani nipulizie kila baada ya muda gani? in preventive basis (nisingependa mmea uugue hata kidogo).
DAWA NZURI ZA KUTUMIA NI ZILE ZENYE SUMU (YAANI ACTIVE INGREDIENT YA CYPERMETHRIN,
PROFENOFOS,
IMIDACLOPLID, CHROLOPHYIVOS, NA ABAMECTIN) TRADE NAME ZA HAYO MADAWA NI KAMA BLAST, BUFFALO, DUDUALL, DURSBAN ETC. NI VYEMA KUPIGA HIZI DAWA KILA BAADA YA SIKU 14 KAMA KINGA, NA NI VYEMA UKAWA NA DAWA ZENYE SUMU MBILI TOFAUTI UKAWA UNAZIPIGA KWA KUPISHANISHA , ILI KUEPUKA USUGU KWA WADUDU, YAANI WIKI HII UKIPIGA SUMU YENYE CYPERMETHRIN MPIGO UJAO UNAPIGA YENYE CHOLOPHOVIVOS ETC, HAKIKISHA UNAPIGA DAWA JIONI AU ASUBUHI SANA, USIPIGE DAWA MCHANA WA 6-9, HAPO UNAUA NYUKI
Kwa jinsi nilivyoona huku field (mashambani), matatizo/magonjwa yanayosumbua sana Bamia ni manne:
A) PANZI... hawa ni wadudu fulani hivi wanaotafuna shina la mmea. Yaani mmea unapoota na kuanza kuweka shina, unakuta mmea umeanguka kwa kukatwa shina pale chini kabisa karibia na udogo. Sijawaona live wadudu hao, ila nimeelezwa kuwa ni 'PANZI wakata shina'.=
HAO TUNAWIATA SOTA/CUTWORM, TUMIA SUMU (ACTIVE INGREDIENT/GUARENTEE) YOYOTE YENYE IMIDACLOPLID, ABAMECTIN AU CYPERMETHRIN ITAMALIZA (KAMPUNI YA SYNGENTA WANA DAWA YENYE TRADE NAME YA MATCH-HII HUUA SANA HAO FUNZA)
B) CHAWA wekundu... hawa nimewaona live kwa macho. Wapo kama utitiri hivi. Hawa huanza kushambulia pale mmea unapoanza kukua, mmea unapoanza kuweka jani la tatu na kuendelea. Hawa wanakaa nyuma ya jani lenyewe, hulifanya jani lijikunje hivi.=HAO TUNAWAITA RED SPIDER MITES, NI WASUMBUFU MNO, NA UKICHEZA WANAMALIZA SHAMBA, HAO HUWA TUNAWAMALIZA KWA KUTUMIA DAWA YENYE SUMU YA DIMETHOATE NA UNAPISHANISHA NA NYINGINE YENYE
IMIDACLOPLID AU ABAMECTIN AU CYPERMETHRIN,
ILA KUMBUKA HIYO DIMETHOATE (MFANO MADUKANI INAUZWA KAMA DIMATE, AU DUME AU HIVYO HIVYO DIMETHOATE, HIYO NI SUMU KALI SANA UNAPOPIGA USIZIDISHE ZAIDI YA MLS 10 ZA DAWA KWA MAJI LITA 15. UKIZIDISHA DOZI NA MCHE UKIWA NA MAUA , YATAKAPUKUTIKA YOOTE
C) UKUNGU... hii husababisha madoa madoa meusi kwenye majani.
HAPO TAFUTA SUMU YENYE MANCOZEB NA METALAXYL NDANI YAKE (MADUKANI UTAZIPATA ZIKUUZWA KAMA IVORY, AU VICTORY AU EBONY AU RIDOMIL GOLD, AU EUREKA, AU SUCCESS AU MISTRESS) MASHAMBULIZI YAKIZIDI TAFUTA ZINGINE ZENYE NGUVU ZAIDI ZINAUZWA KWA BRAND/TRADE NAME YA SCRORE, AU NATIVO (SUMU NI AZOXTROBIN) AU MULTI POWER PLUS 78 WP
D) WADUDU watoboa tunda... hawa nao nimewaona live. Hawa wapo kama kiwavi hivi au kama funza. Wanatoboa tunda lenyewe kabisa, yaani unakuta bamia imetobolewa na mdudu yupo ndani.
HAO TUNAWAITA FRUIT BORER, HAO TUNAWADHIBITI KWA KUTUMIA ILE DAWA YA SYNGENTA YENYE TRADE NAME YA MATCH, AU NOVATHION, AU KARATE, AU ABAMECTIN
Huku nilipo, changamoto hizo wanasema wanazikabili kwa
SUMU na
DAWA. SUMU wanayotumia ni '
MUPA FORCE 720EC' ambayo wanapulizia mara baada tu ya mmea kuanza kuweka shina ili PANZI asiukate, sumu hii wanaipuliza kila week. Na mavuno yakianza, sumu hii hupulizwa kila week pia ili kuzuia wale WADUDU watoboa tunda.
DAWA wanayotumia ni '
ATTAKAN C 344SE' kwaajili ya kuzuia CHAWA wekundu na kuzuia UKUNGU. Kabla ya matunda/mavuno kuanza, dawa hii hupulizwa kila week. Matunda/Mavuno yakianza, hupulizwa kila siku mbili.
JE, hizo SUMU/DAWA ni sahihi? na huo utaratibu wa kupulizia ni sahihi? Mkuu naomba muongozo wako, coz now mmea wangu tayari ushaota.=
HIZO DAWA NI SAHIHI, KIKUBWA NI KUJUA TU SUMU ILIYOMO NDANI, KWA MFANO HIYO MUPA FORCE SUMU YAKE NI PROFENOFOS , HIYO ATTAKAN SUMU YAKE NI
IMIDACLOPLID. MUDA WA KUPULIZA NASHAURI KWA MWANZONI WAPULIZE KILA BAADA YA SIKU 14, NA MATUNDA YAKIANZA WAPULIZE KILA BAADA YA SIKU 7, NA WAKITAKA KUVUNA WAACHE SIKU 5-10 ZIPITE NDIPO WAVUNE HAYO MATUNDA
2. Tupo kipindi cha masika, mvua ni nyingi sana. Mtu anamaliza tu kupuliza dawa/sumu, ghafla mvua inanyesha! Nakumbuka kuna uzi fulani humu humu JF uliwahi ku-mention kimiminika ambacho ni kinatisha sumu kwenye mmea ili mvua isioshe. Ulitaja kitu kama 'AQUA STICKER' (kama sijakosea spelling). Nimeitafuta sana kwenye maduka mengi ya kilimo huku nilipo haipo na wala hawaijuwi. Labda nitajaribu kwenda maduka ya K/Koo. Maana pia nimewapigia simu at Balton Tz pale Mwenge, nao hawana hiyo AQUA STICKER, ila wamenambia wanayo inaitwa SUPER LINK for the same function, wanaiuza elfu 20 kwa lita moja.=
PATA HIYO SUPER LINK, ITAKUSAIDIA
3. Uwekaji wa mbolea ya NPK upoje, naiwekaje kwenye ardhi/shimo la mmea?? kwaajili ya kukuzia.
SAWA UNAWEZA TUMIA HIYO NPK (17:17:17) KWA AJILI YA KUKUZIA, UNAWEZA IWEKA INA SOLID FORM, YAANI UNAWEKA PUNJE ZILE GRAM 5=KISODA 1, UNAWEKA PEMBENI KIDOGO KUTOKA SHINA UNAZUNGUSHA KISHA UNAFUKIA NA UDONGO
LAKINI PIA UNAWEZA IWEKA IN FORM OF SOLUTION, YAANI UNAIYEYUSHA KATIKA MAJI KABISA KAMA UNAWATER TANK KISHA UNAPOFUNGULIA YAE MAJI, YANAKUJA MAJI YENYE MBOLEA NDANI YAKE, HAPA KIPIMO NI GRAM 100 YA MBOLEA=KIGANJA CHAKO KIMOJA UNALOWEKA KATIKA MAJI LITA 15, UNAACHA INAYEYUKA NDIPO UNAIAPPLY KATIKA MMEA KWA KUMWAGIA. SO KAMA UNATAKA KUTENGENEZA SOLUTION NYINGI MEANS ITAKUBID UFANYE CONVERSION MATHEMATICS , KUWA KAMA GRAM 100 ZA MBOLEA ZINAKWENDA NA MAJI LITA 15, JE MAJI LITA 1000 LET SAY NI MBOLEA KIASI GANI UTAPATA JIBU. HII WANAITUMIA SANA WALE WENYE DRIP/UMWAGILIAJI WA MATONE.
4. Natarajia kupanda tena Bamia kwa awamu ya pili. Hizi nitazifanya kwa utaratibu huu: Mbolea ya kupandia namix DAP & SAMADI KUKU; Mbolea ya kukuzia naweka NPK (17:17:17) pekee; kisha nacheza na Boosters to finalize. Hii iko poa?
IKO POA KABISA
KARIBU SANA
Ahsante.
-Kaveli-[/QUOTE]
Sasa mkuu, naomba pia unifahamishe kuhusu MADAWA & SUMU za kupulizia ili kukinga na kuzuia magonjwa mbali mbali, i.e kuanzia mmea unapoota mpaka kuanza mavuno.
1. MADAWA au/na SUMU sahihi kwa zao la Bamia ni yepi? na utaratibu wa kupulizia upoje, yaani nipulizie kila baada ya muda gani? in preventive basis (nisingependa mmea uugue hata kidogo).
Kwa jinsi nilivyoona huku field (mashambani), matatizo/magonjwa yanayosumbua sana Bamia ni manne:
A) PANZI... hawa ni wadudu fulani hivi wanaotafuna shina la mmea. Yaani mmea unapoota na kuanza kuweka shina, unakuta mmea umeanguka kwa kukatwa shina pale chini kabisa karibia na udogo. Sijawaona live wadudu hao, ila nimeelezwa kuwa ni 'PANZI wakata shina'.
B) CHAWA wekundu... hawa nimewaona live kwa macho. Wapo kama utitiri hivi. Hawa huanza kushambulia pale mmea unapoanza kukua, mmea unapoanza kuweka jani la tatu na kuendelea. Hawa wanakaa nyuma ya jani lenyewe, hulifanya jani lijikunje hivi.
C) UKUNGU... hii husababisha madoa madoa meusi kwenye majani.
D) WADUDU watoboa tunda... hawa nao nimewaona live. Hawa wapo kama kiwavi hivi au kama funza. Wanatoboa tunda lenyewe kabisa, yaani unakuta bamia imetobolewa na mdudu yupo ndani.
Huku nilipo, changamoto hizo wanasema wanazikabili kwa SUMU na DAWA. SUMU wanayotumia ni '
MUPA FORCE 720EC' ambayo wanapulizia mara baada tu ya mmea kuanza kuweka shina ili PANZI asiukate, sumu hii wanaipuliza kila week. Na mavuno yakianza, sumu hii hupulizwa kila week pia ili kuzuia wale WADUDU watoboa tunda.
DAWA wanayotumia ni '
ATTAKAN C 344SE' kwaajili ya kuzuia CHAWA wekundu na kuzuia UKUNGU. Kabla ya matunda/mavuno kuanza, dawa hii hupulizwa kila week. Matunda/Mavuno yakianza, hupulizwa kila siku mbili.
JE, hizo SUMU/DAWA ni sahihi? na huo utaratibu wa kupulizia ni sahihi? Mkuu naomba muongozo wako, coz now mmea wangu tayari ushaota.
2. Tupo kipindi cha masika, mvua ni nyingi sana. Mtu anamaliza tu kupuliza dawa/sumu, ghafla mvua inanyesha! Nakumbuka kuna uzi fulani humu humu JF uliwahi ku-mention kimiminika ambacho ni kinatisha sumu kwenye mmea ili mvua isioshe. Ulitaja kitu kama 'AQUA STICKER' (kama sijakosea spelling). Nimeitafuta sana kwenye maduka mengi ya kilimo huku nilipo haipo na wala hawaijuwi. Labda nitajaribu kwenda maduka ya K/Koo. Maana pia nimewapigia simu at Balton Tz pale Mwenge, nao hawana hiyo AQUA STICKER, ila wamenambia wanayo inaitwa SUPER LINK for the same function, wanaiuza elfu 20 kwa lita moja.