Kilimo cha zao la Ufuta: Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Kilimo cha zao la Ufuta: Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Ngano haina tofouti na shairi kwnye cost of production sbb procedure ni zile zile.tofouti ni mavuno na bei. Mavuno ya ngano yapo chni kidogo na bei yake pia.
 
Nimeanza kuvuna ufuta shambani kwangu, kwa sasa nafanya comparison ya bei na wanunuzi. JF ni jungu kuu naombeni member wenye kujua wanunuzi mbali mbali wanipe contacts zao ile nilinganishe bei nifanye right choice ktk kuuza mzigo.
Thanks wadau wote.

Mrejesho:

  • kati ya eka 30 nilizopanda ufuta ulistawi vzuri na kuvunwa eka 17..hii ilisababishwa na uangalizi mbovu wa aliyekuwa ananisimamia shamba.
  • kila eka nilivuna wastani wa kilo 350, kipindi hiki ( july 2011-2012) wanunuzi binafsi hawakuruhusiwa lindi kununua ufuta, so niliuza kwa utaratibu wa stakabadhi ghalani @ 1200/= kwa kilo jumla nilipata kama milion 7 kwa msimu mmoja (gharama za kusafisha msitu wa eka 30, mbegu na malipo ya wafanyakazi zilikuwa ni 3.5 milion), sikuingia gharama ya kusafirisha kwa kuwa walinifata shambani.
  • Mwaka 2013 sikulima nilipumzisha shamba kwa kulisafisha eka zangu zote 50 na kutanua kidogo (hili shamba lilikuwa ni msitu wakati nalichukua)
  • mwaka huo wa 2013 ulikuwa ni mzuri sana kwa upande wa bei, chomachoma (wanunuzi binafsi) waliruhusiwa na ufuta ulipanda bei hadi kufikia 2500 kwa kilo na unalipwa cash hapo hapo. waliolima walipata pesa nzuri tu.
  • mwaka huu vijana wanamalizia kupanda shamba nimelima ekari 35, nilibadili team ya wafanyakazi wa shamba kwa kuwa wengi walinikwamisha kwa kuendekeza starehe badala ya kazi. natumaini wanunuzi binafsi wataruhusiwa.
  • watu wengi kutoka mikoa mbali mbali (wachaga kibao) wameanza kuvamia misitu na kuiuza au kulima so kwa sasa kumechangamka sana tofauti na 2011 wakati naanza.
  • expectations zangu mwaka huu ni ........35(eka) x 400(kg) x 2500(bei/kg)=35,000,000.
  • NB: 400kg kwa eka ni kiwango cha chini cha mavuno, wataalamu wa chuo cha naliendele waliniambia kwa mbegu zao za lindi 2002 na malada natakiwa nipate 1200kg kwa eka. Vijana wapo shamba wanachakarika na mi nipo mjini namtumikia mkoloni (ajira).
Thanks kwa wote:

UKITAKA KUUJUA UTAMU WA NGOMA .......UINGIE UCHEZE.

Nitakuomba mawasiliano yako kwa ufafanuzi zaidi
 
Nitakujibu vichache navyojua bila kufuatisha namba zako lakini.

1) Ufuta unaanza kulimwa January, na mwezi May watu wanavuna.

2) Roughly kulima Kwa heka moja kuanzia kuvunja msitu (lindi wanaita kukata useng-) mpaka kuotesha na kuvuna andaa kama kilo 4 au 5.

3) Kuvuna kwa heka kama una bahati waweza kupata labda gunia 7.

4) Mwaka huu tuneuza kilo Tshs 2,500/- kijijini,na ukiweza kuuleta mjini unapiga kama Tshs 4,000/- kwa kilo.

5)..........

Mbona wanasema ni miezi mitatu hadi minne?
 
Mazao mengi bado hatujayachambua na kuyaweka hapa jamvini mfano;

Ulezi sijawahi ona uzi wake,
Njegere mbichi za kilolo/Uluguruni sijaona humu,
Pilipili mtama za milima ya Matombo bado,
Sijaona wazee wakisema cho chote kuhusu Pareto huko Iringa,njombe na mby,
Sijaona hoja za mtama mweupe na biashara huko TBL,
Je Viazi vikuu tumevichambua?,
Kuna Iriki huko Tanga,
Kuna watu hawajui Choroko na dengu kwamba ni dili kubwa huko India,
Kuna watu wanadhani apples zote zinatoka nje,kumbe zinalimwa hapo Njombe,
Je unayajua marejea na kilimo chake huko Songea enzi zile?

jioni njema.

Naomba tuanzishie topic moja moja, wengine tutamalizia
 
Kwa ekari moja unawe\za kupata kilo 300-500, kilo moja inauzwa 2000/=-2500/=
Gharama zote za kulima, madawa na kuvuna inaweza kufikia laki moja kwa ekari moja

Mashamba yanakodishwa au kununuliwa?
 
Hongereni wakuu ila mkumbuke UFUTA hauhitaji maji mengi mi nalima eka 10 Januari. Mwaka huu nilikuwa 88 nimepata utaalam wakutosha sana khs zao hili mi natumia Mbegu inaitwa LINDI 2002 Eka 1 gunia 8 hdai 12! Tutakuwa tunapeana uzoefu kadri cku zinavyokwenda!

Tunaomba feedback mkuu.
 
Ufuta unalipa sana ndugu zangu.. mwaka huu June nilikuwa na nunua kwa wakulima wadogo na kuleta Dar ni superprofit. Lkn sasa nimeumua kulima eka 5 na mimi..

Wakati unaleta dar, unakuwa tayari na wateja au unaleta ili uje kutafuta wateja???
 
Mkuu mbimbinho,km shamba halijalimwa cdhani km kuna umuhim wa Mbolea ila ikiwa una mashaka cvibaya kuweka km kujilidhisha2 Manake hii mambo ya KILIMO haitaki kujaribu! na khs MVUA nunua MBEGU ya muda mfupi kisha vizia Mvua zinapoanza km mwisho wa Mwezi wa PILI hv zikichanganya kufikia Mwezi wa 4 mwishoni zinakatika, Haitakiwi MVUA za masika zikute UFUTA umeshaanza hakika utajuta! cha muhimu nikufanya TIMMING ya MVUA2!

Kwahyo hakuna msimu maalumu wa kuanza na kuisha? Kwa lindi msimu unaanza lini na unaisha lini?

Na mbolea unatumia ya aina gani?
 
Mbegu ya muda mfupi na yenye maVUNO mengi Kutokana na Maelezo ya wataalam ni hiyo LINDI 2002,Bei wanauza elf 5 kwa 1kg.Mbegu za UFUTA ni ndogo sana so kwenye kupanda ni Lazima kuchanganya na Mchanga. Ukishaota unapunguza miche kila shimo unabakisha miche miWILI au mi3. Ukishaota huwa unaharufu yakuvuta wadudu,ni muhimu kupiga DAWA!

Dawa gani inapigwa? Inapigwa baada ya muda gani wa kupanda?

Samahani unaweza nikadiri gharama za kuhudumia ufuta kwa eka 1 toka kupanda hadi kuvuna? Kila kitu ikiwemo dawa, vibarua, mbegu, dawa nk
 
Wana jf,
Kwa wale unaolima ufuta au mnaonunua kwa wakulima wadogo,projection inaonyesha kutakuwa na soko zuri la ufuta mwaka huu.
Nimekuwa approached na mfanya biashara mwenye partnership na mchina anaehitaji tani 200,000 mwaka huu wakati wa kuvuna.
Ufuta unahitajika ni lindi 2002. Tupo kwenye maongezi ya awali na nampelekea sample this weekend.
Kwa wenye interest stay in touch. Usiulize bei at this stage kwa maana ni mapema mno ila itakuwa nzuri

Ulete feedback mkuu, itatupa mwanga.
 
Umeainisha vizuri lakini hujasema soko likoje na wateja wapo au hawapo baada ya kuvunwa na zao likisha ingia kiwandani na kuwa product yakuuzika international pia soko liko vipi, eb jaribu kuchunguza utuambie mkuu.
 
UNALOONGEA NI KWELI MKUU UFUTA UNALIPA SNA TATIZO NI MADALALI.EMBU ANGALIA BEI ZA MAENEO HAYA morogoro gunia LAKI NA THEMANINI HADI LAKI2.sumbawanga laki2,TANGA laki2 PWANI laki nathemanini,MANYARA hawa majamaa walianza na laki5 gunia na sahvi wanauza laki3.hawa wenzetu wa manyara wanafanikiwa kuuza kw bei kubwa sbb wanalima maeneo makubwa nawamezibiti madalali,kuna makampuni ya wahndi toka arusha ndyo wananunua hapo manyara.wakulima wa manyara wako makini kila idara kuanzia uzalishaji wako juu kwa pato kwa eka,mbegu bora napia wanazalisha ufuta wenye kiwango.HAYO MAENEO YOTE NILIYOTAJA NIMEFANYA UTAFITI MM MWENYEWE NILIANZIA MOROGORO PWANI NA TANGA,sumbawanga nilichukua tarifa kwa wadau sijafika,MANYARA nawaelewa tangia mwanzo na sahv ndyo naelekea MANYARA kuchukua data nzuri kwnn wao wamefanikiwa kuliko mikoa mengine

Naomba uniPM number zako mkuu.
 
Nimeanza kuvuna ufuta shambani kwangu, kwa sasa nafanya comparison ya bei na wanunuzi. JF ni jungu kuu naombeni member wenye kujua wanunuzi mbali mbali wanipe contacts zao ile nilinganishe bei nifanye right choice ktk kuuza mzigo.
Thanks wadau wote.

Mrejesho:

  • kati ya eka 30 nilizopanda ufuta ulistawi vzuri na kuvunwa eka 17..hii ilisababishwa na uangalizi mbovu wa aliyekuwa ananisimamia shamba.
  • kila eka nilivuna wastani wa kilo 350, kipindi hiki ( july 2011-2012) wanunuzi binafsi hawakuruhusiwa lindi kununua ufuta, so niliuza kwa utaratibu wa stakabadhi ghalani @ 1200/= kwa kilo jumla nilipata kama milion 7 kwa msimu mmoja (gharama za kusafisha msitu wa eka 30, mbegu na malipo ya wafanyakazi zilikuwa ni 3.5 milion), sikuingia gharama ya kusafirisha kwa kuwa walinifata shambani.
  • Mwaka 2013 sikulima nilipumzisha shamba kwa kulisafisha eka zangu zote 50 na kutanua kidogo (hili shamba lilikuwa ni msitu wakati nalichukua)
  • mwaka huo wa 2013 ulikuwa ni mzuri sana kwa upande wa bei, chomachoma (wanunuzi binafsi) waliruhusiwa na ufuta ulipanda bei hadi kufikia 2500 kwa kilo na unalipwa cash hapo hapo. waliolima walipata pesa nzuri tu.
  • mwaka huu vijana wanamalizia kupanda shamba nimelima ekari 35, nilibadili team ya wafanyakazi wa shamba kwa kuwa wengi walinikwamisha kwa kuendekeza starehe badala ya kazi. natumaini wanunuzi binafsi wataruhusiwa.
  • watu wengi kutoka mikoa mbali mbali (wachaga kibao) wameanza kuvamia misitu na kuiuza au kulima so kwa sasa kumechangamka sana tofauti na 2011 wakati naanza.
  • expectations zangu mwaka huu ni ........35(eka) x 400(kg) x 2500(bei/kg)=35,000,000.
  • NB: 400kg kwa eka ni kiwango cha chini cha mavuno, wataalamu wa chuo cha naliendele waliniambia kwa mbegu zao za lindi 2002 na malada natakiwa nipate 1200kg kwa eka. Vijana wapo shamba wanachakarika na mi nipo mjini namtumikia mkoloni (ajira).

Thanks kwa wote:

UKITAKA KUUJUA UTAMU WA NGOMA .......UINGIE UCHEZE.

daaah japokuwa nalima ekari 5 tu lakini umenipa lesson 0652112026 tutaftane kaka unipe mautundu
 
Nimependa comment za wadau wa jf juu ya kilimo cha ufuta ukweli ni kwamba ufuta ni biashara nzuri na sio kilimo kizuri sana. ninasema hivi sababu nimefanya kilimo hiki lakini katika kufanya analysis ya kukodi shamba(pori) kufyeka kuunguza nyasi kwa dawa kung'oa visiki
 
Sorry kwa thread yangu kukatika. kwa hiyo kwa maelezo hayo na mengine mengi sio kilimo kizuri sana lakini ni biashara nzuri sana na hio inatokana na kwamba inahitaki mtaji mkubwa ili kufanya kwa hiyo competition kwa watamyabiashara wadogo inakuwa ndogo mimi nilianza na mtaji wa 6m lakini ndani ya mwezi mmoja nina faida ya 6m nilifarijika sana so kama mtu anataka kujua namna ya biashara ya mazao naweza msaidia lakini kilimo chake hapana maana sikupata matarajio niliotaka.
 
Ulifanyia wapi mkuu, ingekuwa bora nichangamoto zp ulizokukutanazo embu funguka natupate mawazo mapya kutoka kwako.
 
Back
Top Bottom