Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kaka milioni 11 ndogo kwa makisio yangu.
Lakni,pia pamoja na ushirirkiano huu nilionao pamoja na mdau huyu,naona sio mbaya kupata mawazo mazuri juu ya ulimaji huu.Nachoweza kusema tuu kwamba tunategemea kulima hekari 100 na tunategemea kutumia kiasi cha M 9.5-11.
Matumizi bado ni changamoto hasa tunapojaribu kupunguza gharama zaidi ukizingatia tunaanza rasmi mwishoni mwa August mwaka huu
Nachoomba kutoka kwenu ni ;
- Wapi tunaweza kupata mbegu nzuri za ufuta.
- Ushauri gani au utaalamu gani tuzingatie katika ulimaji huu.
- Kama kuna mtu anaweza kutukodisha majembe,au tractor la kulimia;maana tunajaribu kubana matumizi na tunaangalia which avenue ni bora zaid and much efficient tractor au Ng'ombe.
Na mwisho je soko likoje maana hatutakuwa tayari kuuza kwa bei za kutupa na kwa hasara.Gharama hizi ni lazima zirudi na faida juu.
ahsanteni.
Sasa mkuu unataka kulima hekari 100 ya kitu ambacho soko lake hulijui/hauna uhakika wake, na mnaanza mwishoni mwa mwezi huu! Kila la heri
Tunajua soko. Lakni mawazo ya wengine sio mabaya. Na pia kuna watu wako resourceful ndo maana sikuona haja kuweka ujuaji hapa. Ndo maana tunataka maujanja.
The King.
sasa mkuu unataka kulima hekari 100 ya kitu ambacho soko lake hulijui/hauna uhakika wake, na mnaanza mwishoni mwa mwezi huu! Kila la heri
Kwa heka 100 mimi naona kama unalima kwa heka sh 50,000 hapo tayari 5,000,000
Kupalilia kama ukipalilia kwa heka 30,000 hapo tayari 3,000,000
Kupanda kama unapanda kwa hela 30,000 hapo tayari 3,000,000
Kuvuna kama utavuna kwa heka sh 30,000 hapo tayari 3,000,000
Kama utaweka ulinzi wa mali zako shambali kuna gharama
Kama uta pack kwenye magunia ni gharama ya kila gunia na gharama ya labour.Kama ni hatua itabidi usafirishe mzigo uje mjini au kwenye ghala.Kama utaweka manager/Bwana shamba itabidi nae alipwe.Na wewe mwenyewe itabidi ujilipe gharama zako nauli , muda nk.Haya ni makisio yangu tu bro sijui huko kwako Morogoro gharama zipoje ila ningekuwa mimi ndio wewe ningeandaa angalau 20M kwa hiyo project
hakuna mazao ya shambani yenye price garantee tanzania yetu hi,labda shairi na tumbaku.
Kuhusu Mbegu za ufuta nyingi zinatoka Mtwara kwenye kituo cha utafiti Naliendele,wizara ya kilimo ina mawakala nafikiri kila mkoa
ni pm nikuelekeze. Nibiashara nzuri yenye faida kwa sasa
Tumbaku Sijawahi Kulima,,ila Shairi Na Ngano Sawa Nina Uzoefu Nazo