Kilimo cha zao la Ufuta: Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Kilimo cha zao la Ufuta: Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Mkuu GEBA2013, tikiti linahela pengine ni usimamizi ndio ulikuangusha. Huwezi kulinganisha pato la ufuta na tikiti hata siku moja. Dunia ya sasa unatakiwa ufanye uzalishaji wenye uhakika wa kutoboa. Mi sifanyi kilimo cha kutegemea mvua hicho walifanya mababu!

Ni mara 100 nikalima ekari2 ntakazozimudu na nikawa na uhakika wa mavuno kuliko ekari mia huku nikiumiza kichwa na shingo kila kukicha nikiomba neema ya mvua.

Fanya vzr mahesabu yako na tafakari kwa kina kile nilichokiandika hapo juu kwani nina uhakika wa nisemacho.
Kama huamini kwamba sh milioni3 haiwezi kuzalisha milioni40, basi njoo na hiyo hela shambani kwangu nikupe darasa nakuhakikishia hiyo hela itapatikana ndani ya siku75. Ila sharti utarudi kwenu na sh m15 tu!!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu GEBA2013, Mi sifanyi kilimo cha kutegemea mvua hicho walifanya mababu! Ni mara 100 nikalima ekari2 ntakazozimudu na nikawa na uhakika wa mavuno kuliko ekari mia huku nikiumiza kichwa na shingo kila kukicha nikiomba neema ya mvua.
!

Kisima kati ya vitu ambavyo havipendi mvua ni Ufuta. Ufuta ni zao linalostahimili ukame na halihitaji mvua nyingi. Zile mvua za mwanzo zinatosha kabisa, halihitaji mvua za mfululizo kama mazao mengine.

Ngeba nimeku-pm.
 
KISIMA embu nipe mchangunuo watikiti maji kwa eka,unapata tikiti ngapi kwa eka na utauza kwa sh ngapi?navyojua mm tikiti kwa eka ni tikiti 3500 hadi 4000 ukijitahidi.nabei ya shamban lazima utauza 1000 au km kuna soko nzuri utauza 1500 kwa tikiti nakatika shamba huwezi kupata kubwa zote lazima pawe na mixture KUBWA KATI NA NDOGO SIZE.Na katika hzo eka utapata kubwa CHACHE size yakati NYINGI na ndogo CHACHE.
 
Mkuu Mazengo, sijakataa kwamba ufuta hauihitaji mvua nyingi ila naomba niweke masahihisho kidogo kwa kile ulichosema, kwanza ieleweke kuwa ufuta haupandwi katika mvua za mwanzo bali ni baada ya mvua za kati ambazo kwa kawaida ni nyingi sana, then baada ya hapo ndo unaweza kupanda ufuta. Yaani kwa mikoa ya mwambao wa pwani inatakiwa upande tarehe za mwanzo hadi kati ya MARCH ili kuepuka mvua nyingi.

All in all soko la ufuta linadhibitiwa na walanguzi na linauzwa kwa target, watu wa Bara Asia wakitosheleza shehena yao na soko linakufa hutapata mteja tena.They have mandate to control the market, you will sell whether you like or not.
Ndiyo maana nasita kuliweka in my list of priorite crops to engage with.

Ni bora ukalima maharage ambayo soko lake lina lapse throughout the year na is the most consumable products of all time!
 
Last edited by a moderator:
Kilimo ya kutegemea mvua haina hasara nawala haimizi kichwa km bustani,bustani ina changamoto kubwa sna haswa pale unapokosa msimamizi wa maana lazima ufeli nakuchukia kilimo.

Changamoto nyngne kilimo chochote cha bustani inataka malezi km mtoto mchanga,umakini wa dawa ardhi nzuri,maji ya uhakika,ukibugi hapo unatoka empty.changamoto lingne bei huwa n tatizo kubwa unaweza ukazalisha ukakutana na bei ndogo na umetumia garama kubwa nakuweka STORE haiwezekani.
 
Mkuu GEBA2013, huu ndio mchanganuo halisi kwa haraka zaidi juu ya kilimo cha tikiti.

1)utakubaliana na mimi kuwa ekari moja ina mita za mraba 4000+
2) upandaji; shimo m1, mstari m1.5 au piwa waweza fanya {shimo m1.5, mstari m1.6}
3) katika kila shimo panda miche2 na ruhusu(thinning) matunda3 kila mche ili yapate chakula vizuri.
4) msisitizo: tumia mbegu ya hybrid sukariF1 ambayo ni tamu na matunda yake ni makubwa kupitiliza!
Bei ya shamba ni Tsh1500 bila longolongo.
Hivyo;
Number ya mashimo/acre ni 4000/(1*1.5)=2666.666~
Matunda 2*3*2666.666~=16000
Mauzo: 1500*16000= TSH 24,000,000/=
Usimamizi ndio kila kitu ili uyafikie hayo mahesabu.
Huo mchanganuo ulionao wewe mi siafikiani nao.
Sifikirii kama gharama ya kulima ekari1 ni zaidi ya m4! hata nusu yake haifiki.
Sawa mkuu GEBA2013?
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli soko la ufuta linamilikiwa na watu asia,napia madalali ndyo wanaoharibu soko.hili ni tatizo na uzaifu na ubovu wa viongozi wetu.kuna haja gani ya kuuza ufuta km maligafi nje?hata na hvyo syo suala lakukata tamaa kila ki2 ina mpangilio,soko linamilikiwa na waasia sbb kuu NI WAKULIMA WALIKUWA WACHACHE WANAOZALISHA,ndyo mana maeneo wanaozalisha ufuta kwa wingi bei iko juu,maeneo wanaozalisha ufuta mchache bei iko chini.kadiri tunavyozidi kuzalisha ufuta mwngi NAAMINI WAWEKEZAJI WATAJENGA VIWANDA HAPA SBB WANAKUWA NA UHAKIKA WA UFUTA NA HAWATASAFIRISHA KM RAW MATERIAL.
 
KISIMA huo mchanganuo kwa ulivyoandika uko sahihi,,je mm nilikosea wapi au wezangu wanaolima wamekosea wapi?labda kwenye mbegu?sababu nimewahi kulima nikapata tikiti makadirio yetu ni tikiti 3500 hadi 4000 pamoja nawakulima wengne.na ukimwuliza mkulima yeyote wa tikiti atakujibu nitikiti 4000 au 3500.nakatika hzo kuna kubwa size yakati na ndogo.sijawahi kutumia hyo mbegu yako.SIKUBISHII SNA.LABDA WAJE WAKULIMA WA TIKITI WALETE MREJESHO WANAPATA NGAPI KWA EKA
 
Mkuu GEBA2013 nafikiri mpaka hapo tupo pamoja!

Mlipokuwa mnaanguka nyinyi ni spacing ya miche, selection ya mbegu na usimamizi madhubuti.

Just imagine umenunua mbegu za Tsh520k kwa ekari1 then niache kukomaa ili izalishe!

Mimi kwenye shughuri zangu msimamizi ni mimi mwenyewe muda wote jembe na spray tank nashika mwenyewe. Wasaidizi wangu nachagua sio kila ajaye kuomba kazi ntampatia. Nishaangushwa sana na nshatimua sana. Nipo friendly but very serious and fame on issues!

I dont give a damn negotiation when it comes to money blowing.
Hii ndio kazi niliyochagua sihitaji kusimamiwa na mtu m the boss himself!
 
Last edited by a moderator:
Asanten wadau mmenipa mwanga mkubwa juu ya hiki kilimo. Inshaallah najiandaa nilime mwaka huu panapo majaaliwa ntawapa mrejesho.
 
Mkuu GEBA2013 nafikiri mpaka hapo tupo pamoja!
mlipokuwa mnaanguka nyinyi ni spacing ya miche, selection ya mbegu na usimamizi madhubuti.
Just imagine umenunua mbegu za Tsh520k kwa ekari1 then niache kukomaa ili izalishe!
Mimi kwenye shughuri zangu msimamizi ni mimi mwenyewe muda wote jembe na spray tank nashika mwenyewe. Wasaidizi wangu nachagua sio kila ajaye kuomba kazi ntampatia. Nishaangushwa sana na nshatimua sana. Nipo friendly but very serious and fame on issues!
I dont give a damn negotiation when it comes to money blowing.
Hii ndio kazi niliyochagua sihitaji kusimamiwa na mtu m the boss himself!

Plz mkuu I need your help
 
Last edited by a moderator:
Bustani inaumiza sna kichwa inatakiwa umakin.garama yake ni kubwa sana na huwezi kulima large scale, ina tabia ya kamari.
 
Mkuu gwijimimi ni vizuri ukaeleza shida yako hapa hapa jukwaani ili kila mtu apate wasaa wa kuchangia na kunufaika kutokana na michango na ufafanuzi utakaotolewa na wadau.
Naona simu yangu leo inasumbua kutumia PM.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Ugoro na wengine mnaohofia changamoto za bustani.

Kila kitu ni usimamizi na utazishinda changamoto kwa kuwa knowledgable na kile unachokifanya. Kilimo cha bustani ni kizuri kwasababu kinakulazimu ujipange na ufanye maandalizi ya kutosha kabla hujaattempt. Smtms unaweza ukalima eneo kubwa kwa kutegemea mvua lakini ukakosa nguvu kazi au pengine mvua isiwe ya uwiano unaotatikana kwa zao husika so mwisho wa siku utaambulia majanga na kukata tamaa.

Anza na eneo dogo ili ujifunze kwanza then slowly u will incline to the highest stage of successes.
 
Last edited by a moderator:
Aisee.mmenifunguaaa Macho vibaya sana Geba Na Kisima.

Nimefatiliaaa makala zenu mwanzo mwisho yaaani ni kwere aiseeee....dah
Hongereni sana mko vizuri sana ktk swala la Ulimaji wa mazao.

Mi nilipanga mwaka huu nilime Vitunguu Maji...Ila Sijapata bado machakato wake ulivyoooo Kuanziaa Mbegu gharama na Wakati wa ulimaji.

Napendelea kulima Same au Mpwapwa....
#Kisima embu nidadavulieee...
Ekari moja cost zake na soka la uwakika.....
 
Aisee.mmenifunguaaa Macho vibaya sana Geba Na Kisima.

Nimefatiliaaa makala zenu mwanzo mwisho yaaani ni kwere aiseeee....dah
Hongereni sana mko vizuri sana ktk swala la Ulimaji wa mazao.

Mi nilipanga mwaka huu nilime Vitunguu Maji. Ila Sijapata bado machakato wake ulivyoooo Kuanziaa Mbegu gharama na Wakati wa ulimaji.

Napendelea kulima Same au Mpwapwa....
#Kisima embu nidadavulieee...
Ekari moja cost zake na soka la uwakika.....
 
Nataka kulima dodoma mwez wa kumi na moja kipindi hiki kinafaa kwa kulima kitunguu wadau
 
Back
Top Bottom