bintimzalendo
Member
- Feb 27, 2014
- 74
- 30
Ni kilimo cha kawaida na rahisi kama kuna usimamizi wa karibu. Mi nina kampuni ya ushauri wa mambo ya kilimo na ufuta ni mojawapo ya mazao tunayoyashughulikia, hivyo twaweza kuwasiliana kwa ushauri zaidi.
Upo Kisarawe ipi?
Wazo njema,jaribu kuandaa shamba mapema,tumia mbegu nzuri yakisasa panda kwa mstari palilizi ni muhimu nadawa pia. KUHUSU SUALA LA SOKO,madalali ni tatizo kubwa,ndyo waliyoua soko la ufuta,mwakajana ufuta ulikuwa nabei nzuri mwaka huu bei imeshuka,kutokana na madalali na baadhi ya wakulima waliweka mchanga kwenye ufuta ili kuzidisha kilo,matokeo yake baadhi ya makampuni toka nje hawakufika kununua ufuta sbb ufuta ni mchafu hauko kwenye viwango vizuri vya soko,hayo makampuni yaliyokuja kununua tna wananunua ufuta kwa bei isiyoridhisha,napia wamekuwa makini ktk kukagua km una mchanga nakm una mchanga unauchekecha hapohapo kwenye kampuni ndyo waupime nakununua.
Ni kilimo cha kawaida na rahisi kama kuna usimamizi wa karibu. Mi nina kampuni ya ushauri wa mambo ya kilimo na ufuta ni mojawapo ya mazao tunayoyashughulikia, hivyo twaweza kuwasiliana kwa ushauri zaidi.
Habar za asubuh wadau!
Nimepata mashamba maeneo ya kisarawe na ninataka mwaka huu nilime ufuta. Nimesikia ufuta una soko zuri na uhitaji wake ni mkubwa.
Naombeni taarifa sahihi juu ya ulimaji, upatikanaji wa mbegu, soko na msaada wa kitaalamu juu ya kilimo cha ufuta.
Pia ntashukuru kama kunasehemu (kampuni/mtu binafsi anaeweza kunipa msaada wa kitaalamu.
Nawatakia jumatatu njema na swaumu njema kwa wafungaji.
Wenu katika ujenzi wa taifa Bintimzalendo
asante mkuu, inaonyesha unataarifa za kutosha kuhusu hiki kilimo na masoko yake. Naomba kukutafuta kama hutojali
Wazo zuri sana, ufuta una lipa sana na una soko kubwa sana! Kila la heri dada
Kuna ufuta wa kijani na ufuta mwekundu.
1. Ufuta wa kijani mazao yake ni hafifu na hushambuliwa sana na magonjwa.
2. Ufuta mwekundu huzaa sana na hutoa matawi mengi yalijaza mbegu za ufuta, na ni nadira sana kushambuliwa na magonjwa, kwa sasa hivi ni maarufu Kisarawe katika vijiji vya Mwanzomgumu, Mbezi na Bwama.