Kilimo kinahitaji uwekezeji mkubwa ili uone faida

Kilimo kinahitaji uwekezeji mkubwa ili uone faida

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Kilimo kinahitaji uwekezeji mkubwa, nikiangalia wale settlers wa Zimbabwean na South Africa waliweka pesa nyingi kwenye kilimo na wanazalisha vyakula kwa wingi. Wakati wa British East Africa, wazungu waliopenda kulima walipewa ardhi lakini kwa masharti ya kuonyesha bank statement inayoonyesha una pesa ya kutosha kuendeleza ardhi.

Anza na heka 20 tu lakini uwe na nyumba bora ya kuishi, ghala la chakula, ukiwa kwenye remote area ambako ndiko kwenye ardhi ya kutosha ni muhimu uwe na wafanyakazi wawili wa kukusaidia. Hawa wanajitaji nyumba zao, licha ya kuwa na uhakika nao kila siku, pia watasaidia ulinzi.

Kwa ufupi tu, uwe na tractor, wheel barrow moja au zaidi, majembe, mapanga, nyundo, shoka, tree chainsaw kwa kukatia miti, usafiri hata Rav4 old model inatosha.

Tunaposema vijana wajiajiri ardhi tunayo, tuyafikirie haya pia.
1613522682811.jpeg

1613522757562.jpeg

1613523012587.jpeg
 
Kijana asie na ajira ambaye ndie kwanza ametoka chuo anataka kujishughulisha na kilimo unamshauri aanze na hekari 20? awe na nyumba na wafanyakazi wawili!

Kwanini asianze na hekari moja au nusu hekari kisha awe anajiendeleza na hekari zaidi kwa kadri anavyovuna na kuuza mazao yake?

Hii thread umewaandikia wafanyakazi wa sekta binafsi, na serikalini may be tena sio wote, lakini haipo kwa wale wanaotaka kuanza kutafuta kupitia kilimo.
 
Mkiwa nje mnaota ndoto za mchana kwa kutheorize fanya utafiti kwanza kabla ya kuandika. Kwa taarifa yako chainsaw hairuhusiwi hapa Tanzania.
 
Kijana asie na ajira ambaye ndie kwanza ametoka chuo anataka kujishughulisha na kilimo unamshauri aanze na hekari 20? awe na nyumba na wafanyakazi wawili!..
Kilimo cha hekari moja siyo kilimo cha kibiashara.

Najua utakuja na mifano ya WhatsApp groups, please don't. Tanzania kuna wakulima wengi mno na hilo ni tatizo kubwa.

Kamwe kama nchi hatutaendelea tukiwa na asilimia 67 ya watu wote wanajihusisha na kilimo, we will never develop that way.
 
Mkuu umeandika vitu vya maana sana! Kongole kwako watu wanafikiri kulima ni umaskini!
 
Mkiwa nje mnaota ndoto za mchana kwa kutheorize fanya utafiti kwanza kabla ya kuandika. Kwa taarifa yako chainsaw hairuhusiwi hapa Tanzania
Inaruhusiwa...ila nilazima uwe na kibali.
Au unamaana tofauti.
Huku kwetu Njombe zipo nyingi tu.
 
Bila shaka hapa unawalenga watu walio na mtaji mkubwa.

Inategemea unalima zao lipi pia.

Mfano:
Ili ulime hekari 20 za mahindi, kwa uchache andaa 8M au 10M kulingana na eneo.

Maharage hekari 20 andaa 10M au zaidi kulingana na eneo.

Na hapo si kilimo cha umwagiliaji, unategemea mvua au ni unalima mabondeni ambapo kuna unyevunyevu mwingi but ni ngumu kupata eneo la kutosha.

Ila kama hauna majukumu (yaani, ni wewe tu na hakuna mtu yeyote ambaye ana kutegemea), kama unaweza anza kidogo kidogo hata na 1, 2, 3 nk huku ukiwa na lengo la kuongeza kila msimu unapofika.

Usisahau hasara na wala usiogope hasara ila jitahidi kufuata taratibu za kilimo ili upunguze uwezekano wa kupata hasara.
 
Mbona zipo na zinatumika au wew upo kenya.
Acha mihemko soma mwenzako
 
Kilimo cha hekari moja siyo kilimo cha kibiashara.
Najua utakuja na mifano ya WhatsApp groups, please don't. Tanzania kuna wakulima wengi mno na hilo ni tatizo kubwa.
Kamwe kama nchi hatutaendelea tukiwa na asilimia 67 ya watu wote wanajihusisha na kilimo, we will never develop that way.
Tutafute kwanza namna ya kupandisha bei ya mazao hasa mahindi vinginevyo hakuna haja ya Kulima
Kwa Hali ilivyo sasa Wakulima wanawafanyia kz makampuni Mbegu Na pembejeo
 
TUTAFUTE KWANZA NAMNA YA KUPANDISHA BEI YA MAZAO HASWA MAHINDI vinginevyo hakuna haja ya Kulima
Kwa Hali ilivyo sasa Wakulima wanawafanyia kz makampuni Mbegu Na pembejeo
Unarudi palepale, wakulima wadogo wapo wengi mno na wametapakaa hawapo organized.

Inakuwa kazi ku-bargain.

Mkulima mkubwa anaweza ku-bargain, usipotaka anaweza ku-process na kuuza end product.

Mkulima mkubwa anaweza ku-buy out kiwanda and viceversa.
 
Kijana asie na ajira ambaye ndie kwanza ametoka chuo anataka kujishughulisha na kilimo unamshauri aanze na hekari 20? awe na nyumba na wafanyakazi wawili!..
Uanze na heka moja na nusu usipate faida uishie ku give up!, i agree though kupata heka 20 kwa recent graduates ni ngumu,labda serikali ifanye ku facilitate
 
TUTAFUTE KWANZA NAMNA YA KUPANDISHA BEI YA MAZAO HASWA MAHINDI vinginevyo hakuna haja ya Kulima
Kwa Hali ilivyo sasa Wakulima wanawafanyia kz makampuni Mbegu Na pembejeo
Umeongea point kubwa sana. Ikiwepo bei ya uhakika ya mazao watu watalima vzuri sana. Wapo watu wanauwezo wa kulima hata hekari Mia lakn kutokana na changamoto ya bei anawekeza kidogo kwa kulima hekari chache
 
Kilimo cha hekari moja siyo kilimo cha kibiashara.
Najua utakuja na mifano ya WhatsApp groups, please don't. Tanzania kuna wakulima wengi mno na hilo ni tatizo kubwa.
Kamwe kama nchi hatutaendelea tukiwa na asilimia 67 ya watu wote wanajihusisha na kilimo, we will never develop that way.
Kama mmeamua kujifurahisha sawa, lakini kama mnazungumzia reality kwa wahusika hii kitu ya 20 acres kwa wengi haitekelezeki, tena mbaya zaidi hata kwa wenye ajira, wafanyakazi wengi wanalia mishahara duni, bila mikopo hapa mnapiga story tu, na usilete habari ya whatsap ambazo hata sizijui zikoje.

Kama hutaki Tanzania iwe na wakulima wengi ni kwasababu ya ubinafsi wako, watu wanatafuta namna ya kutoka haijalishi wanatokaje bora watoke kihalali, na zaidi nikuulize wewe umeajiri wangapi kuwaondoa walipo? umepunguza wangapi kwenye hiyo 67% au unatembea na namba za kwenye vitabu tu ulizotoka nazo chuo?

Badala useme serikali itengeneze mazingira ya watu kujiajiri unataka watu wenyewe wajitengenezee mazingira!
 
Unarudi palepale, wakulima wadogo wapo wengi mno na wametapakaa hawapo organized.
Inakuwa kazi ku-bargain.
Mkulima mkubwa anaweza ku-bargain, usipotaka anaweza ku-process na kuuza end product.
Mkulima mkubwa anaweza ku-buy out kiwanda and viceversa.
Wakulima wadogo wapo na wengi wamejenga, wanasomesha watoto kwa kazi hiyo ya kilimo, usiwadharau hata kidogo, na zaidi ningekuona wa maana uilaumu serikali kuwaacha waendelee kuwa walivyo, badala ya hiki unachoandika hapa ni sawa na kuwataka wakae tu wasijishughulishe na chochote mpaka watakapopata mitaji mikubwa.
 
Back
Top Bottom