Kilimo kinahitaji uwekezeji mkubwa ili uone faida

Kilimo kinahitaji uwekezeji mkubwa ili uone faida

Mkiwa nje mnaota ndoto za mchana kwa kutheorize fanya utafiti kwanza kabla ya kuandika. Kwa taarifa yako chainsaw hairuhusiwi hapa Tanzania.
Siyo Mikoa yote imeweka katazo la kutumia Chainsaw.
 
Sky soko likiwa zuri na uhakika hata ukilima ekari moja tu kwa mkono unatoboa.
 
Mimi ni mkulima wa miti ya mbao. Nakueleza kitu cha uhakika. Kama unapinga muulize Afisa misitu ili upate ukweli. Aidha uliza watu wa kutoka Moshi wakueleze kuwa mlio tu wa chain saw ni hatari mpaka watu wanawashia ndani ya ndoo.
mlio wa chainsaw Kilimanjaro ni kisanga mkuu, lazima uwe na kibali cha kuimiliki kutoka maliasili, na hata miti utakayoenda kuikata mwenye miti awe ameomba kibali cha kukata hiyo miti pia. Vinginevyo Chainsaw inataifishwa na unafungwa pamoja na faini Juu
 
Nazungumzia reality.
Karibu asilimia 90 au zaidi ya watanzania wana angalau ndugu anayeishi kwa kutegemea peasantry. Wazazi wangu pia wamesomeshwa na kukuzwa na kilimo hicho kidogo.
Ila hali yao kimaisha ilikuwa ya tabu sana na ni hali ambayo siyo lengo la mwanadamu kuishi hasa wakati huu. Kwa hiyo kuendelea na kilimo kidogo hakutainua hali ya maisha ya mtanzania au binadamu kwa ujumla.
Kilimo inatakiwa kiwe kikubwa na kiwe industrialized ili wananchi waweze kunfaika either directly au indirectly. Otherwise wewe utakuwa unapiga hatua mbili mbele na mbili nyuma at the same time.
Hayo mambo ya ubinafsi wangu sijui nini, sidhani kama nina muda au haja ya kujadili.

Kuhusu serikali kutengeneza mazingira, hizo ni ndoto za alinacha ambazo zimepandikizwa vichwani mwenu. Haitatokea serikali itakayokutengenezea mazingira bila wewe kutengeneza mazingira ya serikali kukutengenezea mazingira.

Labda serikali za Ulaya na America ziwatengenezee mazingira, na watakuomba usiwafokee tafadhali.
Tusichielewa ni kwa nafaka ni utajiri wa kwanza duniani. Katika heka 20 unaweza kuacha heka mbili za chakula chako cha ziada kama mihogo, migomba na viazi vitamu. Ukiacha heka 18 kwa nafaka kama mpunga au mahindi.

Ukiyahifadhi vizuri ghalani unaweza kusikilizia soko kabla hujauza.
 
Kilimo kinahitaji uwekezeji mkubwa, nikiangalia wale settlers wa Zimbabwean na South Africa waliweka pesa nyingi kwenye kilimo na wanazalisha vyakula kwa wingi. Wakati wa British East Africa, wazungu waliopenda kulima walipewa ardhi lakini kwa masharti ya kuonyesha bank statement inayoonyesha una pesa ya kutosha kuendeleza ardhi.

Anza na heka 20 tu lakini uwe na nyumba bora ya kuishi, ghala la chakula, ukiwa kwenye remote area ambako ndiko kwenye ardhi ya kutosha ni muhimu uwe na wafanyakazi wawili wa kukusaidia. Hawa wanajitaji nyumba zao, licha ya kuwa na uhakika nao kila siku, pia watasaidia ulinzi.

Kwa ufupi tu, uwe na tractor, wheel barrow moja au zaidi, majembe, mapanga, nyundo, shoka, tree chainsaw kwa kukatia miti, usafiri hata Rav4 old model inatosha.

Tunaposema vijana wajiajiri ardhi tunayo, tuyafikirie haya pia.
View attachment 1704212

View attachment 1704214
View attachment 1704217

Hitimisho
Tutaongea yote mwisho wa siku pesa tunatoa wapi kwa hayo
 
Afadhali wewe umeuliza ili upate ufahamu. Si hao mahoka wanahemka tu. Kwanza kuna vi chain saw vidogo vya kukata kama matawi au miti havikatazwi. Chain saw zinazokatazwa ni za kuchana mbao.

Chain saw hairuhusiwi kwa sababu inaharibu mbao. Mti ambao ukitumia msumeno wa kawaida unatoa mbao 10, ukitumia chain saw utapata mbao 7 au pungufu hivyo ni hasara kwa mkulima wa miti ya mbao. Ndiyo maana inakatazwa ili kumlinda mkulima
Sio kweli mwaka jana mwezi wa 11 tumenunua chain saw kariakoo tena mpya kabisa
 
Kilimo kinahitaji uwekezeji mkubwa, nikiangalia wale settlers wa Zimbabwean na South Africa waliweka pesa nyingi kwenye kilimo na wanazalisha vyakula kwa wingi. Wakati wa British East Africa, wazungu waliopenda kulima walipewa ardhi lakini kwa masharti ya kuonyesha bank statement inayoonyesha una pesa ya kutosha kuendeleza ardhi.

Anza na heka 20 tu lakini uwe na nyumba bora ya kuishi, ghala la chakula, ukiwa kwenye remote area ambako ndiko kwenye ardhi ya kutosha ni muhimu uwe na wafanyakazi wawili wa kukusaidia. Hawa wanajitaji nyumba zao, licha ya kuwa na uhakika nao kila siku, pia watasaidia ulinzi.

Kwa ufupi tu, uwe na tractor, wheel barrow moja au zaidi, majembe, mapanga, nyundo, shoka, tree chainsaw kwa kukatia miti, usafiri hata Rav4 old model inatosha.

Tunaposema vijana wajiajiri ardhi tunayo, tuyafikirie haya pia.
View attachment 1704212

View attachment 1704214
View attachment 1704217
Ukweli kabisa
 
Hitimisho
Tutaongea yote mwisho wa siku pesa tunatoa wapi kwa hayo
Bahati mbaya wengi wanasubiri pesa ya mafao baada ya kustaafu ndiyo wanaingiza kwenye kilimo. Kilimo kinahitaji nguvu, ukianza ukiwa 25-30 mpaka ukifika 50-55 mashamba yanajiendesha yenyewe wewe uangalizi wako uko kwenye pesa
 
Wakulima wadogo wapo na wengi wamejenga, wanasomesha watoto kwa kazi hiyo ya kilimo, usiwadharau hata kidogo, na zaidi ningekuona wa maana uilaumu serikali kuwaacha waendelee kuwa walivyo, badala ya hiki unachoandika hapa ni sawa na kuwataka wakae tu wasijishughulishe na chochote mpaka watakapopata mitaji mikubwa.
Asante pia ingesaidia Serikali ingekuwa na vituo vya ku service na vya kukodisha matractor na ushauri .kilimo iwaachie wafanye wananchi binafsi ,yenyewe ijikite kwenye uwezeshaji tuu.
 
Msipende kujikweza, nimewazungumzia wadogo ambao ndio wapo wengi, hiyo 20 mil. wengi wenu bila mikopo hamna, ni ndoto mnaota, kila mtu ana namna yake ya kutoka, msiwakaririshe watu wajione wana mzigo mzito mbele yao wakate tamaa kabla hata ya kuanza, na wengi humu mitandaoni hata hamlimi, huwa mnachati tu kuhusu kilimo kwenye smartphone zenu.
Unachoongea ni sawa na kusema watu wasifikirie kuendelea na elumu ya juu, mbona darasa la saba tena wapo we
 
Kijana asie na ajira ambaye ndie kwanza ametoka chuo anataka kujishughulisha na kilimo unamshauri aanze na hekari 20? awe na nyumba na wafanyakazi wawili!

Kwanini asianze na hekari moja au nusu hekari kisha awe anajiendeleza na hekari zaidi kwa kadri anavyovuna na kuuza mazao yake?

Hii thread umewaandikia wafanyakazi wa sekta binafsi, na serikalini may be tena sio wote, lakini haipo kwa wale wanaotaka kuanza kutafuta kupitia kilimo.
Iyo ni subsistence farming
 
Kilimo cha hekari moja siyo kilimo cha kibiashara.

Najua utakuja na mifano ya WhatsApp groups, please don't. Tanzania kuna wakulima wengi mno na hilo ni tatizo kubwa.

Kamwe kama nchi hatutaendelea tukiwa na asilimia 67 ya watu wote wanajihusisha na kilimo, we will never develop that way.

Acha kupotosha jamii, usi-generalize mambo. Vp kama ni kilimo cha umwagiliaji hekari moja? Tena cha horticultural crops.
 
Acha kupotosha jamii, usi-generalize mambo. Vp kama ni kilimo cha umwagiliaji hekari moja? Tena cha horticultural crops.
Kitakuwaje?
Si uelezee tuone mchanganuo wako kuliko kuongea maneno yasiyo na namba hata moja.
Nielezee hekari moja ya zao fulani, nitawekeza kiasi fulani na nitaingiza kiasi fulani katika kipindi cha mwaka mmoja.
C'mon lets go ....
 
Kweli tupu hii,kama mpunga ukitaka ukulipe ufanye through umwagiliaji ambayo ni gharama kuanzia mbolea,kuandaa shamba,upate pump na mengineyo!Bila hivi huambulii kitu
 
Back
Top Bottom