Kilimo kinahitaji uwekezeji mkubwa ili uone faida

Mkiwa nje mnaota ndoto za mchana kwa kutheorize fanya utafiti kwanza kabla ya kuandika. Kwa taarifa yako chainsaw hairuhusiwi hapa Tanzania
Mbona naziona na kwanini zisiruhusiwe
 
Kwa level ya umegraduate SUA kwahyo bajeti ni expensive
 
Wewe ndio unayajua haya mambo in practice, naona wengine huku wanaleta theories walizosoma madarasani.
 
Mbona ameeleweka vizuri? Wewe anza na hata robo ekari,lakini utafanikiwa miaka kumi ijayo tofauti na aliyeanza kwa style aiyosema.
Msipende kujikweza, nimewazungumzia wadogo ambao ndio wapo wengi, hiyo 20 mil. wengi wenu bila mikopo hamna, ni ndoto mnaota, kila mtu ana namna yake ya kutoka, msiwakaririshe watu wajione wana mzigo mzito mbele yao wakate tamaa kabla hata ya kuanza, na wengi humu mitandaoni hata hamlimi, huwa mnachati tu kuhusu kilimo kwenye smartphone zenu.
 
Mkiwa nje mnaota ndoto za mchana kwa kutheorize fanya utafiti kwanza kabla ya kuandika. Kwa taarifa yako chainsaw hairuhusiwi hapa Tanzania
Kwanini haziruhusiwi? Mbona huku nilipo naziona.
 
Ndiyo maana yake, watu 25 kila mwaka wakilima kwa kiwango hiki watazalisha ajira kuanzia shambani mpaka kwa mchuuzi mpaka chakula kunamfikia mlaji.


Kuendeleza kilimo cha heka moja mbili utaishia kulimia tumbo. Kwakifupi kilimo cha jembe la mkono kimepitwa na wakati.
 
Kilimo cha hekari moja siyo kilimo cha kibiashara.
Najua utakuja na mifano ya WhatsApp groups, please don't. Tanzania kuna wakulima wengi mno na h
Ukiona wewe ni mdogo amua moja kati ya haya: acha ufanye mengine au unganisha nguvu na wenzako.
 
Kwa level ya umegraduate SUA kwahyo bajeti ni expensive
Tufikirie jinsi ya kutatua hili. Manaweza kucha ga pesa watu watano katika Wilaya moja mkanunua trekta na kila mtu akalitumia kwa wiki moja msimu wa kilimo.
 
Hapana sio ki hivyo.

Kwa mimi ambaye ni mkulima mwenye naona cha muhimu ili uone mafanikio ni

Kwanza weka degree na kiingereza pembeni ukiwa huko site wote mue level moja wakulima wenzako unaweza kuta wanajua kulima ila shule ndio kama hivyo, halafu;

1. Ardhi nzuri yenye rutuba ambayo unamiliki mwenyewe.

2. Hiyo ardhi ni bora iwe jirani na chanzo cha maji cha uhakika(,msimu wote)

3. Soko la uhakika la utakacholima.

4. Bila kusahau eneo lako liweze kufikika kama sio kwenye plot kabisa hata jirani tu.

Kwa kuanzia inatosha sana. Ila itategemea hayo mazao utayagharimia kupeleka sokoni au anaenunua atafuata mzigo hapo.

Hivi hapo juu vinatosha utoboe, sababu hutegemei mvua.

Ila pia inategemea kama shamba umelikuta liko imesafishwa ukikikuta pori ndio mambo ya kutumia chainsaw na ujue kuitumia. Mafundi chainsaw wana bei mbaya utalizwa. Kama umepata pori

Chainsaw ni bora kuwa nayo. Mi ninayo

Kwa sisi ambao hatutegemei mikopo n.k unaanza mdogo mdogo na unakuwa.
 
Mbona naziona na kwanini zisiruhusiwe
Afadhali wewe umeuliza ili upate ufahamu. Si hao mahoka wanahemka tu. Kwanza kuna vi chain saw vidogo vya kukata kama matawi au miti havikatazwi. Chain saw zinazokatazwa ni za kuchana mbao.

Chain saw hairuhusiwi kwa sababu inaharibu mbao. Mti ambao ukitumia msumeno wa kawaida unatoa mbao 10, ukitumia chain saw utapata mbao 7 au pungufu hivyo ni hasara kwa mkulima wa miti ya mbao. Ndiyo maana inakatazwa ili kumlinda mkulima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…